• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 8, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imeeleza kuwa, uwekezaji wa gharama kubwa, ndiyo sababu za msingi utoaji huduma bora katika Bandari ya Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, alisema serikali inagharamia miradi mikubwa bandarini kwa sababu, inataka bandari iwe ya kisasa, ifanye kazi kwa ufanisi na kutoa huduma shindani duniani.

 “Lengo ni kujiridhisha kwamba, bandari yetu inafanya kazi kwa ufanisi, inatoa huduma shindani na bora kwa wateja wetu,” alisema Mbossa.

Mbossa alisema kaulimbiu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja isemayo; “Hatua ya Ziada,” itakuwa mwongozo wa utendaji wa mamlaka katika kuhakikisha wateja wanapata huduma na bidhaa bora.

Alifafanua kuwa, mamlaka imeweka mkazo kuboresha huduma kwa wateja na kuongeza uwezo wa bandari zake kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu huku ikilenga kuhakikisha wafanyabiashara wanachukua mizigo yao kwa wakati.

Mbossa, alisema mafanikio ya TPA yanaonekana ndani ya nchi na kimataifa, akibainisha kuwa Bandari ya Dar es Salaam, imepanda kutoka nafasi ya 360 na kufikia 255 katika viwango vya ubora duniani. 

Aliishukuru serikali kwa kuiruhusu TPA kukopa dola milloni 500 za Marekani kwa ajili ya kuendelea kuboresha bandari nchini.

Miongoni mwa miradi inayoendelea ni ujenzi wa matanki 15 ya kuhifadhi mafuta katika eneo la Kigamboni, Dar es Salaam, ambao umefikia asilimia 52 ya utekelezaji.

Alisema miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa Bandari Kavu ya Kurasini na upanuzi wa Bandari ya Mtwara, unaolenga kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena kama saruji, makaa ya mawe na bidhaa nyingine zinazofanana.

“Pamoja na maboresho hayo, tunafanya pia ujenzi wa Gati la Malindi iliyopo Dar es Salaam, mbele ya Makao Makuu ya Mamlaka,” alisema.

Kwa upande wa Bandari ya Dar es Salaam, Mbossa alisema TPA ina mpango wa uboreshaji kwa kujenga gati namba 12 hadi 15 na kuimarisha gati namba 8 hadi 11, hatua inayolenga kuongeza uwezo wa bandari hiyo kuhudumia meli na mizigo kwa ufanisi zaidi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Balozi Ernest Mangu, ameipongeza  Bandari ya Dar es Salaam kwa utendaji mzuri unaodhihirika hivi sasa, akawaomba  wadau wa usafirishaji wa mizigo, kuhakikisha wanachukua mizigo yao kwa wakati kupunguza msongamano.

Balozi Ernest Mangu, ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu, amewataka wafanyakazi kufanya kazi kwa ufanisi ili kuendelea kuimarisha imani ya watumiaji wa huduma za bandari.

“Ongezeko la mizigo limeibua changamoto nyingine, ukiwemo msongamano wa malori katika barabara zinazoelekea bandarini na katika vituo maalumu vya kuhifadhia na kusafirishia mizigo (ICDs),” alisema Balozi Mangu.

Aliitaka TPA, kampuni za usafirishaji wa mizigo na wadau wengine katika sekta hiyo, kushirikiana kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo, ili kuhakikisha ongezeko la shughuli za bandari haliathiri ufanisi wa huduma kwingineko.

Balozi Mangu, alisema TPA inapaswa kutumia ubunifu na kubaini upungufu wa kiutendaji ndani ya taasisi hiyo, badala ya kutegemea kutafuta wateja wapya, akisisitiza kuwa ufanisi wa huduma ndiyo msingi wa kuvutia na kuwahifadhi wateja katika soko lenye ushindani mkubwa.

“Lengo letu ni kuhakikisha bandari zinaendelea kuwa kiungo muhimu katika kukuza uchumi na kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

“Sekta ya umma inahitaji kushirikiana na sekta binafsi katika kufikia uchumi wa dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050,” alisema.

Katika hafla hiyo, Balozi Mangu alitoa tuzo kwa wafanyakazi 12 waliofanyakazi vizuri kutoka idara mbalimbali za TPA, huku akiwataka kuendelea kuongeza bidii na ubunifu kudumisha kiwango cha utendaji na kuwa mfano kwa watumishi wengine.

Previous Post

WASOMI WAELEZA FAIDA MKUTANO WA IPU NCHINI

Next Post

SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

Next Post
SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DEPU, OKELLO WAMOTO, YANGA IKISHINDA 6-0

DEPU, OKELLO WAMOTO, YANGA IKISHINDA 6-0

9 months ago

Uchumi wa Tanzania unaendelea kukua kwa asilimia 6.8

1 year ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?