• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WASOMI WAELEZA FAIDA MKUTANO WA IPU NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 8, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WASOMI WAELEZA FAIDA MKUTANO WA IPU NCHINI
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na REHEMA MAIGALA

BAADHI ya wachumi na wasomi, wamesema mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unatoa fursa kwa nchi kushirikiana na mabunge mengine kujadili masuala yanayohusu maendeleo, amani, demokrasia na ustawi wa wananchi.

Pia, wamesema wabunge wa Tanzania, watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na nchi nyingine kuhusu namna ya kuimarisha utendaji wa Bunge, uwakilishi wa wananchi na ushiriki wa makundi mbalimbali katika shughuli za kitaifa.

Wakizungumza na UHURU kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wadau hao, walisema mkutano huo pia utafungua mijadala ya maendeleo endelevu nchini.

PROFESA KINYONDO

Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Abel Kinyondo, alisema mkutano huo ni wa kujivunia kwa sababu unatoa fursa mbalimbali.

“Tunatakiwa kwa pamoja tujivunie uhusiano mzuri tulionao na nchi nyingine, kwa sababu tunajua Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya kazi kubwa kujenga uhusiano na hali inayojidhiririsha kuwa, Tanzania hivi sasa inajulikana na mataifa mbalimbali duniani.

 “Idadi ya watalii hadi kufika mwakani itaongezeka, nina imani hawa wageni waliopo katika mkutano huu, lazima mwakani watarudi kutembelea vivutio vilivyopo na hata kufanya uwekezaji ,”alisema.

Vilevile Profesa Kinyondo, alisema kupitia mkutano huo, sekta mbalimbali zitafaidika zikiwemo za usafirishaji, mawasiliano na utalii.

Dk. DANINGA

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, Dk. Philip Daninga, alisema mkutano huo, utafungua fursa nyingi za maendeleo.

Dk. Daninga, alisema kuna sababu nyingi mkutano huo kufanyika nchini ukiwemo usalama wa nchi na ulinzi imara uliokuwepo.

“Hawakukurupuka tu mkutano kufanyika nchini kwetu, wamepima vitu vingi vikiwemo, usalama na utulivu wa nchi, ndiyo maana mkutano huo umefanyika.

 “Nina imani kubwa baada ya mkutano huo kumalizika, uchumi utaongezeka kwa wananchi, hata serikali kwa ujumla kuna baadhi ya wananchi watakuwa wakiuza bidhaa zao maeneo ya mkutano huo.

“Bidhaa zitakazouzwa ni zile za ndani, vikiwemo vinyago, mavazi na mapambo ya kujipamba ambayo yatakuwa yametengenezwa na vitu vya asili kama shanga, nina uhakika bidhaa hizo zitapendwa zaidi na wafanyabiashara hao, watapata fedha kutoka kwa wageni waliohudhuria mkutano huo,” alisema.

DK. MAGUO

Naye, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Huria Tanzania (OUT), Dk. Mohamed Maguo, alisema ujio wa mkutano wa IPU, utatoa fursa nzuri za kidiplomasia.

Alisema Tanzania itaimarisha uhusiano na ushirikiano kwa nchi zilizohudhuria mkutano huo, utasaidia kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya maendeleo.

Pia, alisema mkutano huo, utaiwezesha Tanzania kuendelea kujenga uhusiano wa kimataifa na kuonesha fursa zilizopo nchini katika nyanja za biashara, uwekezaji na utalii.

“Mkutano huu ni fursa nzuri kwetu, ujio huu, unaonesha nchi yetu ni ya amani na ina utulivu wa hali ya juu, tunaamini ujio wa wageni hawautasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu, kutokana na fedha za kigeni zitakazotumika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi wa kati wa mkutano huu,” alisema.

Oktoba 5, mwaka huu, mkutano wa IPU, ulizinduliwa na Rais Dk. Samia, ambapo unawakutanisha wabunge, maspika, makatibu wa mabunge na viongozi wengine kutoka mabunge wanachama duniani.

Previous Post

MA- HR WANAOKOPA KIJANJA WASHTUKIWA

Next Post

TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

Next Post
TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

5 months ago
MSAFARA WA RAIS DK. SAMIA KIVINGINE

MSAFARA WA RAIS DK. SAMIA KIVINGINE

6 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?