• ePaper
Saturday, October 24, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NDEJEMBI AWEKA MSIMAMO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 19, 2026
in Habari, Kitaifa
0
NDEJEMBI AWEKA MSIMAMO
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

MAKAMU wa Rais Deogratius Ndejembi, ameweka wazi msimamo wa serikali kuhusu shamba la Highland Estate wilayani Mbarali, mkoani Mbeya, lililofanyiwa uthamini wa sh. bilioni 30.

Ndejembi alisema fedha hizo zinazotolewa na serikali hazipaswi kugeuka fursa ya kujinufaisha watu wachache wenye nguvu za kiuchumi, huku wakulima wadogo waliokusudiwa kusaidiwa wakiendelea kuteseka.

Akiwasilisha salamu za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akiwa ziarani Rujewa mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki, Ndejembi, alisema serikali imetoa sh. bilioni 10 za malipo ya shamba hilo lenye ukubwa wa takriban hekari 6,000, kwa lengo la kulirejesha chini ya usimamizi wa serikali na kuwawezesha wakulima wadogo kulikodi kwa gharama nafuu, badala ya kuendelea kulipa sh. 600,000 au 700,000 kwa ekari katika maeneo mengine.

Makamu wa Rais Ndejembi alimwelekeza Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, kushirikiana na viongozi wa mkoa, wilaya, vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi za serikali, kuwajua wakulima halisi wanaostahili kunufaika na shamba hilo.

Pia, alitaka hatua zichukuliwe dhidi ya yeyote atakayebainika kuhujumu mchakato huo.

Alisisitiza hakuna sababu ya kuwaonea huruma watu wanaotumia nafasi zao kujinufaisha wakati wananchi wa kawaida wanaendelea kuteseka, akionya pia dhidi ya watu wanaoweza kukodi mashamba hayo kwa bei nafuu kutoka serikalini kisha kuwakodisha wakulima wadogo kwa gharama kubwa.

Makamu wa Rais alimuelekeza Waziri wa Kilimo kuweka ukomo wa muda wa kukamilisha ugawaji wa maeneo hayo, akisisitiza wakulima wana familia za kuhudumia, watoto wa kusomesha na maisha yanayohitaji kuendelea.

WAZIRI CHONGOLO

Aidha, Chongolo alimhakikishia Makamu wa Rais Ndejembi serikali imekamilisha awamu ya kwanza ya malipo ya shamba hilo na inatarajia kukamilisha awamu mbili zilizobaki ndani ya miezi miwili.

Alisema shamba hilo halitagawiwa kwa wananchi kama umiliki wa moja kwa moja, bali litaendeshwa kwa mfumo wa ukodishaji wa msimu kwa gharama nafuu chini ya usimamizi wa serikali.

Hata hivyo, Makamu wa Rais alisisitiza kasi ya utekelezaji lazima iendane na uadilifu, dhamira ya Rais Dk. Samia ya kusaidia wakulima waliopoteza maeneo yao kufuatia mabadiliko ya mipaka ya hifadhi isitekwe na watu wenye maslahi binafsi, na kuwaacha walengwa halisi wakiendelea kusubiri haki yao.

JIWE LA MSINGI

Pia, Ndejembi ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa majengo mapya ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE), mkoani Iringa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali kuchochea mageuzi elimu ya juu kupitia uwekezaji unaolenga kupanua fursa za elimu, kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuzalisha wataalamu wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika hafla hiyo jana, Makamu wa Rais alisema serikali, kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, imewekeza takribani sh. trilioni moja, kuimarisha elimu ya juu nchini kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), MUCE kikinufaika na uwekezaji wa zaidi ya sh. bilioni 30.

Alisema uwekezaji huo ni kielelezo cha dhamira ya serikali ya kuhakikisha ongezeko la wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi na sekondari, linaendana na upatikanaji wa nafasi za elimu ya juu, akibainisha tangu mwaka wa fedha 2021/2022, mkoa wa Iringa umepokea zaidi ya sh. bilioni 175 kuboresha miundombinu ya elimu katika ngazi hizo.

Ndejembi aliuagiza uongozi wa chuo hicho kusimamia kwa umakini, uwazi na uadilifu wa fedha zote zinazotolewa kwa miradi ya maendeleo, huku akisisitiza umuhimu wa kukamilisha ujenzi kwa wakati na kuzingatia ubora.

WAZIRI MKENDA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, alieleza kupitia mradi wa HEET, taasisi 20 za elimu ya juu nchini zimenufaika na ujenzi wa maabara 309, hosteli 26, maktaba, kafeteria na ofisi 1,177 na ukarabati wa majengo 48, hatua inayoboresha mazingira ya ufundishaji, ujifunzaji, tafiti na ubunifu.

Alisema mafanikio hayo yameambatana na upanuzi wa wigo wa elimu ya juu kwa kuanzishwa kampasi mpya katika mikoa ya Manyara, Kagera, Lindi, Njombe, Katavi, Kigoma, Mwanza, Rukwa, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Tanga, Singida, Mara, Ruvuma pamoja na Zanzibar.

DK. KIKWETE

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, alisema MUCE chuo hicho kimeendelea kupiga hatua kubwa katika kuimarisha miundombinu ya elimu kupitia utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa majengo saba yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 30.4, inayojumuisha majengo ya sayansi, maabara ya fizikia, midia anuwai na elimu maalumu, hosteli za wanafunzi na maktaba.

Alieleza hadi kufikia Septemba 30, mwaka huu, ujenzi wa majengo manne yanayofadhiliwa kupitia mradi wa HEET ulikuwa umekamilika asilimia 100, hatua inayotarajiwa kuongeza uwezo wa chuo kupokea wanafunzi wengi na kuimarisha ubora wa elimu.

Previous Post

YANGA YAIDUWAZA CFFA 

Next Post

SANGU : TUJENGE MADARAJA YA AMANI NA MARIDHIANO NCHINI

Next Post
SANGU : TUJENGE MADARAJA YA AMANI NA MARIDHIANO NCHINI

SANGU : TUJENGE MADARAJA YA AMANI NA MARIDHIANO NCHINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MSIGWA : DK. SAMIA AMETHIBITISHA UWEZO WAKE WA UONGOZI

MSIGWA : DK. SAMIA AMETHIBITISHA UWEZO WAKE WA UONGOZI

1 year ago
ULEGA AAGIZA KUVUNJWA MKATABA WA MKANDARASI

ULEGA AAGIZA KUVUNJWA MKATABA WA MKANDARASI

9 months ago

Popular News

  • TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAASISI 2,682 ZAANZA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA, SERIKALI YALENGA TAASISI 30,000

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KUWA KITOVU SOKO LA KABONI AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UKURASA MPYA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?