• ePaper
Saturday, October 24, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SANGU : TUJENGE MADARAJA YA AMANI NA MARIDHIANO NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 19, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SANGU : TUJENGE MADARAJA YA AMANI NA MARIDHIANO NCHINI
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amezitaka taasisi za dini nchini kuendelea kujenga madaraja ya amani, umoja na maridhiano badala ya kuta zinazoweza kugawa jamii, akisisitiza kuwa uzalendo wa kweli unaoneshwa kwa vitendo vinavyolinda amani na kuimarisha mshikamano wa kitaifa.

Sangu ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam, alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ibada ya kuwekwa wakfu Askofu John Jumanne Wambura wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Amesema falsafa ya 4R inayohusu Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Ujenzi Mpya inapaswa kuendelezwa kama sehemu ya utamaduni wa Taifa, huku akizitaka taasisi za dini kuendelea kuhimiza upendo, kuheshimiana, mazungumzo na utatuzi wa tofauti kwa amani ili kuimarisha umoja wa Watanzania.

Aidha, Sangu amesisitiza kuwa Serikali inatambua mchango wa taasisi za dini katika kuimarisha maadili, kutoa huduma za kijamii, elimu na afya, pamoja na kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu. Ameahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hizo katika kuimarisha mahusiano mema na ustawi wa wananchi.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Nelson Kisare, ameishukuru Serikali kwa kushiriki katika ibada hiyo, akieleza kuwa Kanisa litaendelea kuliombea Taifa, kuenzi upendo, kulinda amani na kuwa wajumbe wa amani. Aidha, ameahidi kuendeleza falsafa ya 4R katika Kanisa na kuhimiza uzalendo unaodhihirishwa kwa matendo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ameahidi ushirikiano wa Serikali ya Mkoa na taasisi za dini, akieleza kuwa mafanikio ya huduma za Kanisa yana mchango katika ustawi wa jamii na maendeleo ya Mkoa, hususan kupitia maombi, malezi na huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Katika ibada hiyo, Sangu amempongeza Askofu Wambura kwa kuaminiwa kuongoza Dayosisi ya Kaskazini, inayohusisha mikoa ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha, huku akimtaka kutekeleza majukumu yake kwa hekima, unyenyekevu na upendo. Amewahimiza Watanzania kuendelea kulinda amani na kujenga madaraja ya maridhiano kwa manufaa ya Taifa na vizazi vijavyo.

Previous Post

NDEJEMBI AWEKA MSIMAMO

Next Post

TASAF YAINUA UCHUMI, YABORESHA HUDUMA ZA JAMII

Next Post
TASAF YAINUA UCHUMI, YABORESHA HUDUMA ZA JAMII

TASAF YAINUA UCHUMI, YABORESHA HUDUMA ZA JAMII

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WADAU WAMPA TANO RAIS SAMIA TUZO ZA CAF 2025

WADAU WAMPA TANO RAIS SAMIA TUZO ZA CAF 2025

11 months ago
USHIRIKIANO WA CHINA NA AFRIKA KATIKA UJENZI WA RELI YA TAZARA

USHIRIKIANO WA CHINA NA AFRIKA KATIKA UJENZI WA RELI YA TAZARA

7 months ago

Popular News

  • TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAASISI 2,682 ZAANZA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA, SERIKALI YALENGA TAASISI 30,000

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KUWA KITOVU SOKO LA KABONI AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UKURASA MPYA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?