• ePaper
Monday, November 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 30, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

WAZIRI MKUU Dk. Mwigulu Nchemba amewataka viongozi wa Afrika kwa umoja wao waangalie mustakabali wa vijana wa bara hilo kwa vile wana uwezo mkubwa licha ya kuwa wanakosa fursa kwenye soko la ajira.

“Muhimu kwetu sote kwa pamoja ni mustakabali wa vijana wetu kutokana na uwezo mkubwa walionao. Afrika inasimama kama bara changa zaidi duniani; hata hivyo, kila mwaka, mamilioni ya vijana wa kike na wa kiume huingia kwenye soko la ajira kutafuta fursa ambazo hazipo,” amesema.

“Ili kukabiliana na changamoto hii, ushirikiano wetu lazima ulenge kuwa na ubunifu wa hali ya juu. Ushirikiano katika masuala ya akili unde na teknolojia za kidijitali lazima uwe mahsusi ili tuweze kutoa mafunzo kwa kizazi kijacho cha wahandisi wa Kiafrika ambacho kitahakikisha kuwa data za Kiafrika zinasalia chini ya udhibiti wa Afrika, kwa kuzingatia Mkakati wa Umoja wa Afrika wa Akili Unde (African Union Continental AI Strategy),” alisema.

Ametoa wito huo jana (Alhamisi, Oktoba 29, 2026), wakati akitoa hotuba kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kikao kilichofanyika Ikulu ya Kremlin, jijini Moscow, Urusi, ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliomalizika jana.

Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo, Dkt. Mwigulu alisema Tanzania inatoa shukrani zake za dhati kwa ufadhili wa masomo uliotolewa na Shirikisho la Urusi kwa wanafunzi wa Kitanzania. “Ili kuimarisha zaidi uendelezaji wa rasilimali watu, tunatamani kuongezewa mgao kwa kuzingatia zaidi nyanja muhimu za uhandisi, tiba na sayansi za hali ya juu.”

Katika hatua nyingine, Dk. Mwigulu amemuomba Rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin, pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye, wakubali Kiswahili kiwe miongoni mwa lugha zinazotumiwa na jukwaa hilo ili kuimarisha uelewa miongoni mwa washiriki.

“Kiswahili siyo tu kwamba ni lugha rasmi ya kazi katika mikutano ya Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki, SADC, UNESCO na taasisi nyingine kubwa za kimataifa bali kwa miongo kadhaa, imekuwa ikifundishwa kwa ufahari katika taasisi za kitaaluma za hapa Urusi. Ili kuimarisha uelewa wetu, Tanzania inapendekeza rasmi kwamba Kiswahili kijumuishwe katika mipango ya kitamaduni na kielimu ya Jukwaa la Ushirikiano wa Urusi na Afrika,” alisema.

“Ninawapongeza Mheshimiwa Rais wa Mali na wenzake katika shirikisho hili walioamua kufanya mabadiliko ya kizalendo na kutumia lugha zao. Ninawaalika wabadilishe matumizi ya lugha za kikoloni na sasa watumie Kiswahili, na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itawapatia walimu, vitabu vya kufundishia na kamusi. Huo utakuwa ndiyo mwanzo wa kuileta Afrika nzima kuimiliki lugha hii badala ya kujivunia lugha hizo za kikoloni.”

Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Ole Millya; Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Frederick Kibuta, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wa Serikali.

Previous Post

VYAMA VYA SIASA VYAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UJENZI MJI WA SERIKALI

Next Post

WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

Next Post
WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RONALDO KUTUNDIKA DALUGA

RONALDO KUTUNDIKA DALUGA

12 months ago
MWAKINYO KUPIMA UZITO LEO

MWAKINYO KUPIMA UZITO LEO

10 months ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYAMA VYA SIASA VYAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UJENZI MJI WA SERIKALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?