• ePaper
Monday, November 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 1, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Dk. Mwigulu Nchemba amemwelekeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, kuandaa mpango wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za dini katika elimu, kwa kuzingatia uzoefu wa ushirikiano uliopo katika sekta ya afya.

Ametoa maelekezo hayo leo (Jumapili, Novemba 1, 2026), akimwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika ibada ya uzinduzi wa nyumba mpya ya ibada ya Bethel ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Nshara, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

“Waziri, utaenda ukae na wenzako. Kaa na Waziri wa Afya,” amesema.

Dk. Mwigulu ameelekeza wataalamu wa wizara hizo kuangalia namna ya kuimarisha ushirikiano katika elimu na kuandaa mpango utakaowasilishwa kwa Mheshimiwa Rais kwa ajili ya kupata ridhaa ya Serikali.

Maelekezo hayo yamefuatia maelezo kuhusu ujenzi wa kampasi ya Machame ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo), kinachomilikiwa na KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, pamoja na ombi la kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa katika kutoa elimu.

Akifikisha salamu za Rais, Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa taasisi za dini katika maendeleo ya Taifa na itaendelea kushirikiana nazo katika kutoa huduma kwa wananchi.

Amesema historia ya maendeleo ya Tanzania haiwezi kutenganishwa na mchango wa Kanisa, hususan katika elimu na afya, ambako taasisi za dini zimekuwa zikihudumia wananchi bila kujali imani zao.

“Hauwezi ukayataja maendeleo ya nchi yetu hii kwa ustadi wowote ule bila kutaja mchango wa Kanisa,” amesema.

Dk. Mwigulu amewapongeza washarika wa Nshara, viongozi wa Kanisa, kamati ya ujenzi na wadau wote waliofanikisha ujenzi wa nyumba hiyo ya ibada, akisema wamefanya kazi kubwa inayostahili kupongezwa.

Kuhusu mazingira, Waziri Mkuu amehimiza wananchi kuchukulia kwa uzito utunzaji wa miti na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amemwelekeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, kufuatilia hoja ya ukataji miti iliyowasilishwa katika ibada hiyo, kwa kushirikiana na viongozi na wadau husika.

Aidha, amemwelekeza Mkuu wa Mkoa kufanyia kazi ombi la kufungwa taa za barabarani katika eneo la kanisa na kufuatilia hoja za miundombinu zilizowasilishwa na Mbunge wa Hai.

Kwa upande wake, Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Alex Malasusa, amewapongeza washarika na wadau waliofanikisha ujenzi huo, huku akisisitiza umuhimu wa malezi bora, mazungumzo katika familia na upatanishi katika jamii.

Naye Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dk. Fredrick Onael Shoo, ameomba ushirikiano wa Serikali na Kanisa katika elimu na afya uendelezwe. Amesema uzoefu huo ni msingi wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP), unaolenga kutoa huduma kwa wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Ujenzi, Mjumbe wa Kamati hiyo, Freeman Mbowe, amesema wananchi walitenga eneo la ekari 50 kwa ajili ya maendeleo ya elimu na kulikabidhi kwa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini. Ameeleza matarajio yao ya kuona chuo hicho kinatoa elimu bora inayozingatia sayansi na teknolojia.

Kwa mujibu wa risala ya Usharika wa Nshara, nyumba hiyo ya ibada imejengwa kwa zaidi ya miaka kumi kwa gharama zinazokadiriwa kufikia Sh. bilioni 6.5 na ina uwezo wa kuketisha waumini 2,000 kwa ibada.

Ibada ya uzinduzi na kubariki nyumba hiyo imeongozwa na Askofu Dkt. Shoo, huku Askofu Dkt. Malasusa akitoa mahubiri.

Previous Post

WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

7 months ago
 KOCHA SIMBA AITISHA DODOMA JIJI

 KOCHA SIMBA AITISHA DODOMA JIJI

7 months ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYAMA VYA SIASA VYAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UJENZI MJI WA SERIKALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?