NA ABDURAHMAN JUMANNE
Mgombea Mmwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema yupo tayari na kuzitafuta kura za ushindi wa Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29. mwaka huu.
Dk. Nchimbi ameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha utekelezaji wa Ilani ya Chama unafanikiwa kwa manufaa ya wananchi.
Ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam. viwanja vya Tanganyika Packers, katika uzinduzi wa kampeni za CCM. Tukio hilo limehudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanachama kutoka mikoa mbalimbali.
Akizungumza baada ya kukaribishwa na Mgombea Urais wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Balozi DK. Nchimbi amesema atashirikiana kikamilifu kuhakikisha Chama kinashinda kwa kishindo na kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzu ya mwaka 2025–2030.