MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema chama hicho kimepanga kuboresha huduma za afya wilayani Kwimba, mkoani Mwanza, kwa kujenga zahanati 20 mpya.
Aidha, amesema serikali itakayoongozwa na CCM itaendeleza ujenzi wa zahanati nne ambazo zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi, sambamba na kujenga vituo vitano vya afya katika wilaya hiyo.

Balozi Dk. Nchimbi ametoa ahadi hizo wakati wa ziara yake ya kampeni wilayani Kwimba, akiwataka wananchi kuendelea kuiamini CCM kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha yao.