• ePaper
Saturday, March 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

FIDIA YANUKIA WANANCHI WALIOPISHA MRADI SGR

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 10, 2025
in Habari, Kitaifa, Uchaguzi
0
FIDIA YANUKIA WANANCHI WALIOPISHA MRADI SGR
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA MUSSA YUSUPH,

Bahi

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali inafanya uhakiki wa madai ya fidia kwa wananchi waliopisha mradi wa reli ya mwendokasi (SGR) na miradi mingine ya maendeleo wilayani Bahi, mkoani Dodoma.

Dk. Samia aliyasema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani hapo, alipokuwa njiani kwenda mkoani Singida.

“Ninatambua kuna madai ya fidia kwa waliopisha mradi wa SGR, lakini na miradi mingine. Madai yenu tunayafanyia uhakiki na tutakapomaliza, fidia zinakwenda kulipwa,” alisema Dk. Samia.

Kuhusu ujenzi wa reli hiyo, alieleza katika awamu ya pili kutajengwa kituo cha abiria na bandari kavu.

Alisema ujenzi wa kituo na bandari kavu utaongeza kasi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

“Ujenzi wa kituo na bandari kavu unakwenda kuibadilisha Bahi kwa sababu vitavutia uwekezaji, biashara na kuchochea ongezeko la ajira.

“Miaka mitano mbele tunakokwenda yanakuja makubwa zaidi na wanasema yajayo yanafurahisha. Hiyo ndiyo dhamira yangu ya kusimama kuwaomba ikifika Oktoba 29, mwaka huu, wote tukapige kura,” alieleza.

Akizungumzia huduma za afya, Dk. Samia alisema serikali imejenga hospitali ya wilaya, vituo vya afya na zahanati.

Kwa upande wa elimu, alisema katika kipindi cha miaka mitano, serikali imejenga shule mpya za msingi 14, hivyo jumla kufikia 86.

Alieleza kwa shule za sekondari, serikali imejenga shule tatu mpya hivyo kufikisha 25 katika wilaya hiyo huku akisisitiza mpango uliopo kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike.

“Pamoja na hayo, tumejenga vyuo viwili vya VETA vyenye wanafunzi 156 ambao wanakwenda kujifunza fani za ujenzi, ushonaji, kompyuta, ufundi umeme wa majumbani na magari.

“Na hizi ndizo kazi zitakazowatoa vijana wetu kwa sababu wapo mijini na katika njia kubwa. Tutafikiria baadaye kuanzisha fani ya kilimo na ufugaji,”aliongeza Dk. Samia.

Previous Post

SERIKALI IMEIMARISHA BARABARA – DK. SAMIA

Next Post

WAKAZI WA RUKWA WAAHIDI ‘MITANO TENA’ KWA DK. SAMIA

Next Post
WAKAZI WA RUKWA WAAHIDI ‘MITANO TENA’ KWA DK. SAMIA

WAKAZI WA RUKWA WAAHIDI ‘MITANO TENA’ KWA DK. SAMIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KICHEKO WAKANDARASI WANAWAKE

KICHEKO WAKANDARASI WANAWAKE

3 months ago
TCU YAFUNGUA DIRISHA UDAHILI AWAMU YA PILI

TCU YAFUNGUA DIRISHA UDAHILI AWAMU YA PILI

6 months ago

Popular News

  • SALOME AIBANA KAMPUNI YA DONGFANG KWA KASI ISIYORIDHISHA MRADI WA UMEME MALAGARASI

    SALOME AIBANA KAMPUNI YA DONGFANG KWA KASI ISIYORIDHISHA MRADI WA UMEME MALAGARASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AZINDUA BODI YA KABONI, AIPA MAAGIZO MATANO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • FCC, TCRA KUCHUNGUZA GHARAMA ZA BANDO NCHINI 

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AIPA HESHIMA DIPLOMASIA YA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULINZI, USALAMA KUIMARISHWA AFCON

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?