• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAKAZI WA RUKWA WAAHIDI ‘MITANO TENA’ KWA DK. SAMIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 10, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
WAKAZI WA RUKWA WAAHIDI ‘MITANO TENA’ KWA DK. SAMIA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NJUMAI NGOTA, 

Rukwa

BAADHI ya wakazi wa Mkoa wa Rukwa, wameahidi kumpatia kura za kishindo Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, kutokana na kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025, hasa katika sekta za afya, elimu, miundombinu na maji safi na salama.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano ya kampeni za CCM iliyofanyika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini na Kalambo, wananchi hao, walionesha kuridhishwa na kasi ya maendeleo yanayotekelezwa chini ya uongozi wa Dk. Samia.

 Mkazi wa Kalambo, Khadija Selemani, alisema miaka mitano iliyopita, kulikuwa na changamoto kubwa katika upatikanaji huduma za kijamii, hivi sasa, hali imebadilika kwa kiasi kikubwa, kutokana na msukumo wa Serikali ya Awamu ya Sita.

 “Hivi sasa huduma ya maji safi na salama inapatikana. Dawa zinapatikana hospitalini na watumishi wa afya, wanawahudumia wagonjwa kwa upendo. “Hatuna cha kumlipa Mama Samia zaidi ya kumpigia kura nyingi za kishindo Oktoba 29,” alisema.

 Alieleza kuwa, barabara nyingi zimeboreshwa kwa kiwango cha changarawe na nyingine kuwekwa lami, hivyo wanaamini wagombea wa CCM wataendelea kukamilisha maeneo machache yaliyosalia.

 “Dk. Samia anatatua matatizo ya wananchi kwa vitendo, tunamwomba aendelee na kazi hii nzuri ya kulijenga taifa na kukuza uchumi wetu,” alisema.

 Naye, mkazi wa Laela, John Sangu, aliwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 na kumpigia kura Dk. Samia pamoja na wabunge na madiwani wa CCM, huku akisema maendeleo yaliyopatikana Rukwa ni dhahiri na hayahitaji maelezo marefu.

 “Barabara hivi sasa zinapitika muda wote, huduma za afya, zimeboreshwa na shule nyingi zimejengwa. Watoto wetu wanakaa katika madawati na ufaulu umeongezeka, hiyo inatokana na dhamira ya dhati ya Dk.Samia, kutoa elimu bure,” alisema Sangu.

Kabula Mashimo, alisema amejiandaa kushiriki uchaguzi huo kwa kuwapigia kura wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi.

 “Tunahitaji kila Mtanzania atoke Oktoba 29 akakipigie kura Chama chetu ambacho kimeendelea kutupatia maendeleo kupitia utekelezaji wa Ilani ya CCM,” alisema.

Alisema wanawake nchini, wana kila sababu ya kumuunga mkono Dk. Samia kutokana na jitihada zake katika kuwaondolea adha ya kubeba ndoo za maji kichwani kwa kuwasogezea huduma karibu na makazi yao na kuwawezesha kupata nishati safi ya kupikia.

Previous Post

FIDIA YANUKIA WANANCHI WALIOPISHA MRADI SGR

Next Post

CCM YATAJA VIPAUMBELE VYAKE WILAYA YA KALAMBO

Next Post
CCM YATAJA VIPAUMBELE VYAKE WILAYA YA KALAMBO

CCM YATAJA VIPAUMBELE VYAKE WILAYA YA KALAMBO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAELFU YA WAGONJWA KUTOKA NJE YA NCHI WAMIMINIKA KUPATA HUDUMA

MAELFU YA WAGONJWA KUTOKA NJE YA NCHI WAMIMINIKA KUPATA HUDUMA

1 month ago
REKODI MPYA ZANZIBAR

REKODI MPYA ZANZIBAR

3 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?