• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MASHABIKI WA MWAKINYO WATULIZWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 3, 2025
in Burudani, Michezo
0
MASHABIKI WA MWAKINYO WATULIZWA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

AMINA KASHEBA 

KOCHA wa ngumi za kulipwa, Kanda Kabongo amewataka mashabiki wa bondia, Hassan Mwakinyo kuwa na imani naye kuelekea katika pambano la ‘Boxing On Boxing Day’.

Mwakinyo atapanda ulingoni Desemba 26, mwaka huu, ukumbi wa Superdome, Dar es Salaam katika pambano hilo ambalo mpinzani wake bado hajawekwa hadharani.

Akizungumza Dar es Salaam, Kabongo alisema asilimia kubwa ya mazoezi ya Mwakinyo yamekamilika, hivyo aliwaomba Watanzania wategemee mambo mazuri kutoka kwake.

“Mwakinyo kila siku anafanya mazoezi ndiyo maana sina wasiwasi na yeye kwa sababu mimi ndiye napanga programu nzima ya mazoezi yake.

“Pia, tumekuwa tukifanya mazoezi kabla ya kutangazwa pambano hilo kwa sababu ngumi ndiyo mchezo wake, hivyo Watanzania wategemee mambo mazuri kutoka kwa Mwakinyo,” alisema.

Kocha huyo alisema mbali ya mpinzani wake kutofahamika hadi leo, bado ana imani atapambana na b ondia mwenye uwezo mkubwa.

Mkurugenzi wa Peak time Media, Meja Selemani Semunyu ambao ni waandaji wa pambano hilo, alisema mpinzani wa Mwakinyo atafahamika muda wowote ndani ya wiki hii.

“Tupo katika upangaji wa orodha ya mabondia ambao watapanda ulingoni katika pambano la ‘Boxing On Boxing Day’, pia wiki ijayo Watanzania watafahamu mpinzani wa Mwakinyo, ambaye atakuwa (main card),”alisema.

Meja huyo aliongeza kuwa milango ya kudhamini pambano hilo, ipo wazi kwa kampuni, taasisi za umma na binafsi.

Previous Post

AZAM, SINGIDA BS UTAMU UPO HAPA

Next Post

TUMEJIPANGA

Next Post
TUMEJIPANGA

TUMEJIPANGA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA, SIMBA ZAANZA KUCHONGA 

YANGA, SIMBA ZAANZA KUCHONGA 

5 months ago
CHOBWEDO ATIKISA

CHOBWEDO ATIKISA

5 days ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?