• ePaper
Thursday, May 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MWIGULU ACHARUKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 12, 2025
in Habari, Kitaifa
0
MWIGULU ACHARUKA

WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba

0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dodoma
SELINA MATHEW NA FRED ALFRED

WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, ameiagiza Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma, kubaini maeneo yenye mianya ya rushwa ambayo yamechangia baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kujilimbikizia mali kwa udanganyifu.

Ameitaka sekretarieti hiyo kuanzisha kitengo cha taarifa za siri kuhusu mienendo isiyoeleweka ya watumishi wa umma, kisha uchunguzi wa kina ufanyike kwani wapo baadhi wamekuwa wakimiliki mali ambazo kiuhalisia haziendani na kipato au muda wa utumishi kazini.

Dk. Mwigulu ametoa maagizo hayo jijini hapa alipozungumza na viongozi wa sekretarieti hiyo ambapo alisema bado kuna kazi kubwa katika kusimamia masuala ya maadili ya utumishi wa umma, huku akisisitiza serikali haitakuwa na mzaha kwa wala rushwa.

“Hatuwezi tukaendelea na utaratibu kwamba katika nchi hii wawepo wengine wana fursa zaidi ya keki wakichukua kwa niaba ya wengine huku wengine wakawa wanaugulia.

“Kuna watumishi wa umma kazi yao zinapimika na vipato vipo sawa kama walimu, madaktari, wauguzi, vyombo vya ulinzi na usalama. Lakini kuna mtu kazi yake haipimiki sana, analipwa vizuri na bado anachukua rushwa anasababisha uwezo wa serikali uwe mdogo.”

Aliongeza: “Anzeni na maeneo ambayo viashiria vyake vipo juu katika masuala ya rushwa, hilo ndilo linakuwa namba moja. Akishajaza (fomu) nendeni mkachunguze kama kuna kilichofichwa baada ya kilichojazwa na kilichopo nje ya kipato chake.”

ATAJA MAENEO YENYE MATOBO

Alisema asilimia 75 ya bajeti ya serikali kwa mwaka inakwenda katika manunuzi ya umma na mikataba.

Alibainisha kuwa Sheria Namba 13 ya Mwaka 1995 iliyoboreshwa mwaka 2001, tamko linalotolewa kwa viongozi wa umma na watumishi wengine wa umma wanatoa hati, haiwalazimishi kuweka wazi mali zao.

“Siyo kila eneo fedha zinavuja, tuna maeneo ambayo yana matobo mengi. Inawezekana Watanzania wengine wasiyajue na inawezekana watunga kanuni na watengeneza matamko haya wanaweza wasiyajue.

“Madhara yake tunaweza tukawa tunatekeleza kikamilifu suala la matamko kwa viongozi wa umma na sheria, lakini uhalisia wake masuala ya ukosefu wa maadili yakaendelea kikalimifu,” alisema Dk. Mwigulu.

Alieleza kuwa katika eneo hilo ni muhimu lifanyiwe kazi kwani watumishi waliopo maeneo yenye chemichemi za rushwa kwa kiasi kikubwa hawalazimiki kuweka wazi mali zao na hawajazi tamko la mali na madeni.

“Kila mwaka tunakuwa hatuna utamaduni wa kujaza fomu, wengine tunajaza kila mwaka na kila mwaka ukiisha rushwa inaendelea hili lazima liangaliwe upya,” alisisitiza.

Aliagiza yabainishwe maeneo ambayo yana rekodi, vivutio au viashiria vya rushwa ambayo kwa sababu ya mapungufu katika sheria, watu wamekuwa wakikwepa.

“Wapo watu ambao tenda ikishatangazwa wanaiwekea dau na dau linakuwa linaendana na mradi. Mwingine nyumba, gari, akaunti, fedha na jambo linapangwa kuanzia bajeti ya mradi inapotengenezwa, inajumlishwa na bajeti ya rushwa.

Alibainisha: “Ikipita bajeti wanashangilia unadhani ni nzuri kumbe dili lao limepita.”

Alitaja eneo la pili ni makusanyo ambapo alisema wanaokadiria wanapandisha au kushusha, hivyo suala hilo halipaswi kuachwa likaendelea.

“Eneo lingine ni mtu anayetoa leseni, kuna baadhi ya maeneo wanapora wachimbaji wadogo, wananchi wakishagundua tu likipelekwa kwenye mfumo, wakishajua mali iliyopo, wanagawana halafu mnyonge amepoteza.

“Namshukuru Rais na Waziri wa Madini kwa kufanyia kazi maeneo haya, moja ya maeneo ambayo lazima tuendelee kutupia jicho ni kwa wanaotoa leseni za uchimbaji,” alisema Dk. Mwigulu.

Kadhalika, alitaja eneo lingine ni ardhi ambapo alisema lazima sekta hiyo itupiwe jicho la umakini.

ASHUSHA MAAGIZO

Katika hotuba yake, Dk. Mwigulu aliagiza kufanyika mapitio ya haraka katika tamko la mali na madeni kubaini maeneo mengine yenye viashiria vya rushwa.

Pili, Dk. Mwigulu aliagiza kuwa matamko hayo yawekewe madaraja ili sampuli zijikite katika maeneo yaliyoathirika zaidi na rushwa.

Aliitaka sekretarieti hiyo kuanzisha kitengo cha taarifa za siri kuhusu mienendo isiyoeleweka ya baadhi ya watumishi wa umma kisha uchunguzi wa kina ufanyike.

Vilevile, aliagiza kama kuna eneo la sheria au kanuni linahitaji marekebisho yafanyike haraka kukidhi utaratibu huo.

WAZIRI RIDHIWANI

Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, alisema Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ina kazi kubwa ya kusimamia maadili.

“Leo hii hata mimi nashutumiwa kwa mambo ambayo siyo ya kweli na ninyi mliopewa jukumu hili mmenyamaza kimya kwa sababu hamuoni kama hilo ni jukumu lenu. Tunajua kuwa mnalo jukumu kikatiba kumuita kiongozi ambaye anatajwa hadharani au kificho kueleza kuhusu taarifa hizo,” alieleza.

Alisema tume ikikaa kimya Taifa litaendela kuwa na viongozi ambao wanaonekana siyo waadilifu.

“Chombo hiki ni nguvu ya uzalendo katika nchi yetu, hivyo ni muhimu kikaendelea kufanya kazi yake kikamilifu ili tuwe na viongozi ambao ni wasafi,”  alisema.

Naye, Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi, alisema Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ilianzishwa kwa lengo la kuchunguza tabia na mienendo ya viongozi wa umma.

Alisema changamoto inayoikumba taasisi hiyo ni kukosekana ushahidi wa moja kwa moja kwa kuogopa kujulikana hasa kwa watumishi wa umma.

“Tumekuwa tukikumbana na changamoto ya ukosefu wa rasilimali fedha kwa ajili ya kuendesha uchunguzi hasa ukizingatia wingi wa malalamiko tunayoyapokea,” alisema.

Previous Post

SERIKALI YAITA WADAU KUISAPOTI TAIFA STARS

Next Post

ZANZIBAR YANG’ARA KIMATAIFA

Next Post
ZANZIBAR YANG’ARA KIMATAIFA

ZANZIBAR YANG’ARA KIMATAIFA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

5 months ago
SIMBACHAWENE AHIMIZA KUDUMISHA ZAIDI AMANI

SIMBACHAWENE AHIMIZA KUDUMISHA ZAIDI AMANI

5 months ago

Popular News

  • YANGA MBELE KWA MBELE

    YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?