• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

ZANZIBAR YANG’ARA KIMATAIFA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 12, 2025
in Habari, Kitaifa
0
ZANZIBAR YANG’ARA KIMATAIFA
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa taasisi na wadau wa sekta ya utalii kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha Tanzania, ikiwemo Zanzibar, inaendelea kunufaika na tuzo na fursa za kimataifa katika sekta ya utalii.

Rai hiyo imetolewa leo tarehe 12 Desemba 2025, Ikulu Zanzibar, baada ya Rais Dk. Mwinyi kupokea Tuzo ya Africa’s Best Corporate Retreat Destination 2025, ambayo Zanzibar imeshinda kwenye Mashindano ya Dunia ya Utalii wa Safari (World Travel Awards 2025) yaliyofanyika nchini Bahrain.

Tuzo hiyo imewasilishwa kwa Rais na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hamad Hassan Chande.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa Zanzibar, baada ya kushindana na mataifa manne: Kenya, Afrika Kusini, Morocco na Botswana.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Rais Dk. Mwinyi amesema ushindi huo ni heshima kubwa kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, na unadhihirisha kiwango kikubwa cha maendeleo ya sekta ya utalii nchini. Amesisitiza umuhimu wa kuongeza ubora wa huduma, kuimarisha vivutio vya utalii, na kutumia tuzo hizo kama chachu ya kushindana kimataifa, hasa katika eneo linalokua kwa kasi la utalii wa mikutano na matukio.

Ameeleza kuwa utalii ni “sekta mama” ya uchumi wa Zanzibar, hivyo mipango thabiti na ushirikiano wa karibu miongoni mwa wadau inahitajika ili kuongeza thamani na mapato yatokanayo na sekta hiyo. Aidha, ametumia nafasi hiyo kuhimiza maandalizi ya pamoja kuelekea Tanzania kuwa mwenyeji wa World Travel Awards Grand Finale 2026, akiwataka wadau waongeze ubunifu na kuboresha bidhaa na huduma za utalii.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Chande amesema ushindi wa Zanzibar ni hatua kubwa inayoliweka taifa katika ramani ya dunia kama kitovu kipya cha utalii wa safari barani Afrika. Amebainisha kuwa Tanzania imeibuka na tuzo tano kwenye mashindano hayo, ikiwemo tuzo kubwa ya Tanzania World’s Leading Safari Destination.

Previous Post

MWIGULU ACHARUKA

Next Post

WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIDAIWA KUIBA MALI ZA SH. BILIONI 1.5

Next Post
WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIDAIWA KUIBA MALI ZA SH. BILIONI 1.5

WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIDAIWA KUIBA MALI ZA SH. BILIONI 1.5

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA ALIVYOIPAISHA MICHEZO

RAIS DK. SAMIA ALIVYOIPAISHA MICHEZO

3 months ago
UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

4 weeks ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?