• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIDAIWA KUIBA MALI ZA SH. BILIONI 1.5

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 13, 2025
in Habari, Kitaifa
0
WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIDAIWA KUIBA MALI ZA SH. BILIONI 1.5
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Mwandishi Wetu

WAKAZI wawili wa Kinyerezi, Dar es Salaam, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha kisha kujipatia vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. bilioni 1.5

Washitakiwa hao ni Tumaini Moshi (33) na Gaspar Mmari (24) ambapo walifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya.

Akiwasomea shtaka hilo, Wakili wa Serikali, Frank Rimoy alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 28915/2025 ambalo ni shtaka la unyang’anyi wa kutumia mawe, fimbo na nondo ili kujipatia vitu hivyo.

Ilidaiwa kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo Oktoba 29 mwaka huu katika Klabu ya The Voice Tz Limited iliyopo Kinyerezi ambapo walifanya unyang’anyi kwa kutumia silaha kisha kuiba vitu vilivvokuwepo ndani va klabu hivo.

Wakili Rimoy alidai kuwa wakiwa katika eneo hilo waliiba viti 350 vya mbao na plastiki vyenye thamani ya sh. Milioni 150, vifaa vya ofisini wenve thamani va sh. milioni 40 na runinga 57 zilizokuwa na thamani ya sh. milioni 480.

Pia, inadaiwa washitakiwa hao waliiba seti ya muziki yenye thamani ya sh. milioni 250, mshine ya mfumo wa malipo (POS) yenye thamani ya sh. milioni 80 na vyombo wa iikoni wa thamani va sh.milioni 25.

Kadhalika, ilidaiwa waliiba vifaa wa baa yenye thamani ya sh. milioni 15 vinywaji mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 518 na fedha taslimu kiasi cha sh.

milioni 16.9.

Washitakiwa hao ilidaiwa kabla na baada ya wizi huo waliwatishia Jammy Galus, Masoud Ahmed na Benedict Katarunga kwa kutumia mawe, fimbo na nondo.

Baada ya maelezo hayo, Wakili Rimoy alidai upelelezi wa haujakamilika, hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Lyamuya, aliahirísha kesi hiyo hadi Desemba 22 mwaka huu kwa kútajwa, hivyo washitakiwa walirudishwa rumande kwani shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Previous Post

ZANZIBAR YANG’ARA KIMATAIFA

Next Post

‘MSAUZI’, MHISPANIA WACHUANA UKOCHA SIMBA

Next Post
‘MSAUZI’, MHISPANIA WACHUANA UKOCHA SIMBA

‘MSAUZI’, MHISPANIA WACHUANA UKOCHA SIMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TABORA, UZALISHAJI WAANZA RASMI

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TABORA, UZALISHAJI WAANZA RASMI

1 month ago
KARDINALI PENGO AACHA SIMANZI

KARDINALI PENGO AACHA SIMANZI

2 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?