• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MASAUNI ATAKA WANAHABARI KUELIMISHA MUUNGANO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 24, 2025
in Habari, Kitaifa
0
MASAUNI ATAKA WANAHABARI KUELIMISHA MUUNGANO
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA JANE MIHANJI

WAANDISHI  wa habari nchini wametakiwa kuielimisha jamii, juu ya faida za muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar kuwarithisha vijana historia ya taifa.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Hamad Yusuf Masauni, wakati wa semina kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyolenga kutoa elimu juu ya wajibu wa vyombo vya habari katika kulinda na kuendeleza muungano.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dk. John Nchimbi, Waziri Masauni alisema ni wajibu wa vyombo vya habari kukuza uelewa na ufahamu wa historia  ya taifa kwa vijana.

“Muungano wetu umedumu karibu nusu karne, lakini kuna vijana wengi hawajui historia wala faida ya muungano huu, hivyo ni wajibu wa waandishi wa habari kutoa elimu sahihi juu ya muungano huu ambao umekuwa kichocheo cha amani, mshikamano na utulivu miongoni mwa Watanzania,” alisema.

Aliitaka jamii kuacha upotoshaji unaoweza kusababisha mgawanyiko na hivyo kuwataka wanahabari kuandika taarifa sahihi, zenye vyanzo vya uhakika, kuandaa makongamano na mijadala yenye tija  kuzungumzia mafanikio ya muungano.

Masauni alisema Ofisi ya Makamu wa Rais imeweka utaratibu wa kutoa mafunzo kwa vijana, kuhusu muungano kulinda historia ya taifa na kuwajenga katika uzalendo wa nchi yao.

Mapema akitoa mada kuhusu chimbuko, misingi na faida za Muungano, mwanasiasa mkongwe Dk. Harrison Mwakyembe, alisema kizazi kipya cha uongozi na  jamii ambayo haijashiriki au kuona nchi ilivyopata uhuru na muungano ni vema ikatambua thamani hiyo.

“Ni lazima historia ikawekwa kwa usahihi kwani madhara ya historia potofu ya nchi ni makubwa kwa vizazi na vizazi,” alisema Dk. Mwakyembe na kuongeza kuwa asilimia 70 ya vijana walizaliwa baada ya muungano, hivyo wanapaswa kujua ukweli kuhusu muungano.

Kwa upande wake, mwanahabari nguli, Salvatory Rweyemamu akitoa mada kuhusu  wajibu wa waandishi wa habari katika kulinda na kuuenzi muungano alisema waandishi wa habari wana wajibu mkubwa wa kuulinda muungano.

“Muwe waangalifu katika uandishi, uzalendo ni kitu muhimu sana, waandishi wa mataifa ya magharibi huwaoni hata siku moja wakizungumza kuhusu kuuvunja muungano wao, lakini wamekuwa wakiandika kuhusu mataifa mengine…hili ni la kujifunza,” alisema.

Aliwataka waandishi wa habari kupunguza ushabiki kwenye masuala ya muungano kwasababu hauna faida na badala yake mijadala inayoibuliwa iongozwe kwa kuwa na taarifa sahihi.

Sambamba na muungano, Rweyemamu alisisitiza pia kuyalinda Mapinduzi ya Zanzibar ambayo aliyataja kuwa ni mhimili mkuu wa Muungano.

Mafunzo hayo yamekuja huku muungano huo ukiwa na umri wa miaka 61 tangu kuasisiwa kwake Aprili 26, mwaka 1964.

Previous Post

MOURINHO WA YANGA PRINCESS AFUNGUKA

Next Post

RUNGU LA MWIGULU LASHUKA TEMESA

Next Post
RUNGU LA MWIGULU LASHUKA TEMESA

RUNGU LA MWIGULU LASHUKA TEMESA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MBAPPE AMFIKIA HENRY UFARANSA

MBAPPE AMFIKIA HENRY UFARANSA

7 months ago
CCM YAWAPONGEZA WANANCHI, YALAANI VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI

CCM YAWAPONGEZA WANANCHI, YALAANI VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI

5 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?