• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

YAJUE MATUKIO YA MICHEZO YALIYOWEKA ALAMA MWAKA 2025

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 29, 2025
in Makala, MAKALA BURUDANI, MAKALA MICHEZO
0
YAJUE MATUKIO YA MICHEZO YALIYOWEKA ALAMA MWAKA 2025
0
SHARES
18
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

MWAKA 2025 ni mwaka wa kihistoria kwa sekta ya michezo na burudani nchini kuanzia katika soka, riadha hadi katika ngumi.

Kila upande wa michezo uliandika simulizi yake kutokana na kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa, jambo ambalo liliteta heshima ya nchi baada ya kushinda makombe na medali.

Makala hii inaonyesha matukio yaliyotikisa, kushangaza na kufurahisha wadau wa michezo baada ya timu za Tanzania na wanamichezo kufanya vizuri mwaka huu.

RIADHA YANG’ARA

Septemba 15, mwaka huu, Simbu aliweka historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mbio za dunia (WAC).
Simbu aliingia katika vitabu vya historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano hayo, tukio lililopokewa kwa furaha, shangwe na pongezi kutoka kila kona ya nchi.

Katika mashindano hayo yaliyofanyika Tokyo nchini Japan, Simbu alikimbia kwa kutumia muda wa saa 02:09:48.
Katika upande mwingine, mwanariadha Gabriel Geay, aliibuka mshindi wa tatu katika mbio za Aramco Huston Half Marathoni za Marekani zilizofanyika Januari 19 mwaka huu, akitumia muda wa dakika 59.18.

Muda huo ulimfanya mwanariadha huyo kuvunja rekodi mpya ya taifa ya nusu marathoni iliyodumu miaka saba iliyowekwa na marehemu Ismail Juma kwa kukimbia muda wa dakika 59.30 katika mbio za Jamhuri ya Czech.

Mwanariadha huyo hakuishia hapo, pia Februari 23 mwaka huu, Geat alishinda nafasi ya pili katika mashindano yaliyofanyika Boston nchini Marekani kwa kutumia saa 2:06:04.

Mbali ya Simbu na Geay, yupo mwanariadha Madgalena Shauri ambaye alimaliza nafasi ya tatu katika mashindano ya mbio za Chicago.
Mbio hizo zilizofanyika Oktoba 12 mwaka huu jijini Chicago, Marekani, Madgalena alikimbia kwa muda wa saa 2:18:03 na kuwa Mtanzania wa kwanza kumaliza tatu bora katika mashindano hayo.

Mtanzania huyo alikuwa akishikilia rekodi ya taifa ya muda wa saa 2:18:41 aliyoweka mwaka 2023  katika Marathon ya Berlin.
 
CHAN 2025

Katika soka, mwaka 2025 utakumbukwa kama moja ya miaka bora kutokana na Tanzania kupata mafanikio mbalimbali.

Moja ya mafanikio hayo  ni Tanzania kuwa mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) 2024 na kutinga hatua ya robo fainali.
Tanzania ilianza michuano hiyo kwa kushirikiana na nchi za Kenya na Uganda.

Katika CHAN, Taifa Stars ilitolewa na Morocco kwa kichapo cha bao 1-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Baadaye. Morocco ikaenda kutwaa taji hilo kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Madagascar.

TWIGA STARS BINGWA CECAFA

Timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’, iliwapatia Watanzania burudani ya aina yake kwa kutwaa taji la Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) 2025.

Twiga ilitwaa taji hilo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya.
Katika mechi hiyo ilifanyika Juni 21 mwaka huu, katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, Twiga Stars ilionyesha kiwango cha hali ya juu.

JKT QUEENS BINGWA 
LIGI KUU BARA, CECAFA

Mwaka huu umekuwa bora kwa timu ya soka ya JKT Queens ambayo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, Kombe la Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake.

Timu hiyo ilitwaa ubingwa wa CECAFA baada ya kuichapa bao 1-0 timu ya Rayon Sports ya Rwanda katika mtanange wa fainali uliopigwa Uwanja wa Nyayo Kasarani, Nairobi nchini Kenya.

Kutokana na ubingwa huo, JKT Queens ilifuzu Ligi ya Mabingwa Afrika iliyofanyika nchini Algeria ambako iliishia hatua ya makundi.
AZAM FC, SINGIDA ZAFUZU MAKUNDI CAFCC

Mwaka huu pia, timu za soka za Azam FC n a Singida Black Stars kwa mara ya kwanza zilifuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).
Azam FC imetinga hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya kupata ushindi katika mechi zake zote nne ilizocheza, ikifunga mabao 13.

Kwa mujibu wa takwimu za michuano hiyo inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Azam FC iliyofunga mabao 13, haijaruhusu bao lolote.

Katika hatua ya kwanza, miamba hiyo ilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Al Marreikh Bentiu ya Sudan Kusini kabla ya kushinda mabao 2-0 dhidi ya KMKM katika mchezo wa kwanza wa hatua ya pili. 

Katika mchezo wa marudiano dhidi ya KMKM, Azam FC ilipata ushindi wa mabao 7-0.
Singida Black Stars ilifunga mabao Saba na kuruhusu mabao matatu.

Singida ilianza kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda kabla ya kushinda mabao 4-2 ilipocheza na Flambeau du Centre kutoka Burundi.
 
MASUMBWI

Katika masumbwi ya ridhaa, timu ya taifa ya mchezo huo ilitwaa medali 18 katika mashindano ya ngumi barani Afrika.

Katika mchanganuo huo, Tanzania ilishinda medali moja ya dhahabu, nne za fedha na 13 za shaba huku ikishika nafasi ya nne katika mashindano hayo.
Mbali ya timu hiyo kukusanya medali nyingi, lakini nahodha Yusuph Changalawe alitwaa medali ya dhahabu na kuandika historia nyingine katika mchezo huo kutokana na rekodi kubwa aliyoifanya.

Upande mwingine mabondia wa ngumi za kulipwa, Juma Choki, Yohana Mchanja, Ibrahim Mafia, Salmini Kassim, Lupakisyo Shoti ‘Sakuveda King’, Pius Mpenda, Abdulrahman Magoma na Frank Shagembe walifanya vyema.

Mabondia hao walifanya vyema mwaka huu katika mapambano yao ya kimataifa ambayo yameipa sifa nchi kutokana na umahiri wao wa kurusha makonde wakiwa ulingoni.
 
Upande wa bondia, Juma Choki alipata nafasi ya kushiriki mashindano ya ya dunia ya ngumi ya Riyadh Grand Prix yaliyofanyika nchini Saudi Arabia.
 
Choki alikuwa Mtanzania pekee aliyepata fursa ya kushiriki mashindano hayo, ambapo aliishia hatua ya 16 bora baada ya kupoteza kwa pointi dhidi ya Bekizizwe Maitse raia wa Afrika Kusini.

Mabondia kutoka Mafia Boxing Promotion ambao ni Ibrahim Mafia, Yohana Mchanja (mkanda wa WBO Global Afrika), Salmini Kassim (Ubingwa wa WBO) na Abdulrahamn Magoma(ubingwa wa UBO) nao waling’ara baada ya kutwaa mikanda ya ubingwa.
 
Upande wa bondia Shoti anayesimamiwa na Fayheroes Sports Promotion mwaka huu, aling’ara katika boxrec baada ya kutwaa mkanda wa ubingwa wa alishinda mkanda wa IBO.

Shoti alishinda mkanda huo akiwa nchini Romania na kumchakaza kwa pointi mpinzani wake, Daniel “Magic Dan” Buciu katika pambano la raundi 10.
 
TEMBO WARRIORS
 
Timu ya taifa ya soka kwa watu wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’, ilishika nafasi ya pili katika mashindano ya Afrika Mashariki ambayo yalifanyika Septemba 14, mwaka huu.
 
Katika mashindano hayo yaliyofanyika nchini Burundi, Tembo Warriors ilionyesha kiwango kikubwa licha ya kukosa taji.

Previous Post

MSUVA NA REKODI YA MAANA AFCON

Next Post

JOSHUA APATA AJALI NIGERIA

Next Post
JOSHUA APATA AJALI NIGERIA

JOSHUA APATA AJALI NIGERIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MBETO : HAKUNA WA KUZUIA USHINDI WA CCM ZANZIBAR 2025-2030

MBETO : HAKUNA WA KUZUIA USHINDI WA CCM ZANZIBAR 2025-2030

9 months ago
DK. SAMIA AHIMIZA UPIGAJI KURA OKTOBA 29

DK. SAMIA AHIMIZA UPIGAJI KURA OKTOBA 29

7 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?