• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

WAJUE WAKALI WA MABAO AFCON 2025

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 5, 2026
in Burudani, Kimataifa, MAKALA BURUDANI, MAKALA MICHEZO, Michezo
0
WAJUE WAKALI WA MABAO AFCON 2025
0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RABAT, Morocco

MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), inazidi kunoga ambapo sasa ipo katika hatua ya 16 bora.

Katika michuano hiyo, tayari timu za Senegal na Mali zimeshatinga robo fainali.

Senegal iliitoa Sudan kwa ushindi wa mabao 3-1 wakati Mali ikiitoa Tunisia kwa ushindi wa penalti 3-2 baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mbali na vita ya kuwania ubingwa, vita nyingine kubwa katika michuano hiyo ni kuwania kiatu cha ufungaji bora wa mashindano hayo.

1: RIYAD MAHREZ

Nyota huyo wa Algeria ndiye kinara wa mabao akiwa amepachika mabao matatu katika mashindano hayo hadi sasa.

Mahrez ambaye amecheza mechi mbili za makundi, amefunga mabao mawili dhidi ya Sudan katika mtanange wa kwanza kabla ya kufunga bao moja dhidi ya Burkina Faso katika mechi ya pili.

2: EL KAABI

Straika wa Morocco, Ayoub Al Kaabi naye ni kinara wa mabao akiwa amefunga magoli matatu katika mechi tatu za michuano hiyo.

El Kaabi amepachika mabao hayo katika mechi dhidi ya Comoros moja  na Zambia mawili.

3: BRAHIM DIAZ

Mchezaji mwingine kinara wa mabao katika michuano hiyo ni Brahim Diaz kutoka Morocco, ambaye amepachika mabao matatu katika mechi tatu.

Diaz amefunga mabao hayo dhidi ya Comoros moja, Mali moja na dhidi ya Zambia bao moja.

4: LASSINE SINAYOKO

Mchezaji mwingine anayetikisa katika vita ya mabao ni Lassine Sinayoko kutoka timu ya taifa ya Mali ambaye amepachika mabao matatu.

Nyota huyo amepachika mabao mawili katika hatua ya makundi na moja hatua ya 16 bora.

Sinayoko alifunga bao moja dhidi ya Zambia, moja dhidi ya Morocco katika makundi na juzi alifunga bao moja dhidi ya Tunisia katika hatua ya 16 bora.

SALAH, LOOKMAN

Waliofunga mabao mawili katika michuano hiyo ni Mmisri Mohamed Salah, Mnigeria Ademola Lookman, Lyle Forster wa Afrika Kusini, Gael Kakuta wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Ibrahim Maza wa Algeria.

Wengine ni Nicolas Jackson wa Senegal, Geny Catamo wa Msumbiji, Cherif Ndiaye wa Senegal, Raphael Onyedika wa Nigeria, Amad Diallo wa Ivory Coast, Pape Gueye wa Senegal, Oswin Appollis kutoka Afrika Kusini na Elias Achouri wa Tunisia.

MSUVA, OSIMHEN

Miongoni mwa wachezaji waliofunga bao moja katika michuano hiyo ni Simon Msuva, Feisa l Salum ‘Fei Toto’ kutoka Tanzania pamoja na Victor Osimhen wa Nigeria, Sadio Mane wa Senegal na Charles M’Mombwa kutoka Tanzania.

Pia wapo Amad Diallo wa Ivory Coast, Pape Gueye wa Senegal, Oswin Appollis kutoka Afrika Kusini na Elias Achouri wa Tunisia.

Wengine waliofunga bao moja katika michuano hiyo msimu huu ni Denis Omedi wa Uganda, Tshepang Moremi wa Afrika Kusini, Mtunisia Ali Abdi, Bazoumana Toure wa Ivory Coast na Evann Guessand kutoka Ivory Coast.

Wengine ni Mzimbabwe Knowledge Musona, Paul Onuachu wa Nigeria, Jean-Philippe Krasso wa Ivory Coast, Habib Diallo wa Senegal, Omar Marmoush kutoka Misri, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Cedric Bakambu wa DRC.

MSUVA NA REKODI BAB KUBWA

Bao dhidi ya Uganda hivi karibuni limemfanya Msuva kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Taifa Stars katika AFCON, ambapo awali alikuwa sawa na Thuweni Waziri kila mmoja akiwa na mabao mawili.

Msuva ambaye sasa ana mabao matatu katika michuano hiyo, amejiwekea rekodi hiyo dhidi ya Thuweni ambaye alifunga mabao mawili katika fainali zilizofanyika miaka 45 iliyopita nchini Nigeria.

Katika fainali za 1980, Thuweni alifunga bao moja dhidi ya Misri katika kichapo cha mabao 2-1 na bao moja dhidi ya Ivory Coast katika sare ya bao 1-1.

Kwa upande wa Msuva amefunga katika fainali tatu zilizopita ambazo Taifa Stars imeshiriki.

Nyota huyo alifunga bao moja katika kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya Kenya (2019), bao lingine katika sare ya bao 1-1 dhidi ya Zambia (2023) na bao moja dhidi ya Kenya juzi.

Wachezaji wengine waliofunga mabao katika michuano ya AFCON ni Fei Toto (1), Mbwana Samatta (1), Mommbwa (1), Juma Mkambi (1).

SAFARI YA MABILIONI

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), michuano ya AFCON inatarajiwa kutumia dau la dola za Marekani milioni 32 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 78.3 za Tanzania kwa ajili ya zawadi pekee.

Katika mchanganuo wa fedha hizo, bingwa wa michuano hiyo anatarajiwa kuvuna dola za Marekani milioni saba ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 17.1.

Timu itakayoshika nafasi ya pili itavuna dola za Marekani milioni nne ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 9.7 za Tanzania.

Timu mbili zitakazoishia hatua ya nusu fainali, kila moja itaondoka na dola za Marekani milioni 2.5 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 6.1 za Tanzania.

Timu nne zitakazoishia hatua ya robo fainali zitavuna dola za Marekani milioni 1.3 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 3.1 za Tanzania.

CAF pia imeeleza kwamba, miamba minane itakayoishia hatua ya 16 bora itavuna dola za Marekani 800,000 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 1.9 za Tanzania.

Timu zitakazoishia nafasi ya tatu katika kundi, kila moja itaondoka na dola za Marekani 700,000 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 1.7 wakati zile zitakazoburuta mkia katika kila kundi zitavuna dola za Marekani 500,000 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 1.2 za Tanzania.

Previous Post

TANZANIA ILIVYOWEKA HISTORIA AFCON 2025

Next Post

HOFU YA WANAUME KUOA WANAWAKE WAREMBO IKO HAPA

Next Post
HOFU YA WANAUME KUOA WANAWAKE WAREMBO IKO HAPA

HOFU YA WANAUME KUOA WANAWAKE WAREMBO IKO HAPA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

USHIRIKIANO WA CHINA NA AFRIKA KATIKA UJENZI WA RELI YA TAZARA

USHIRIKIANO WA CHINA NA AFRIKA KATIKA UJENZI WA RELI YA TAZARA

3 weeks ago
KOCHA SIMBA AJITETEA, MASHABIKI WACHARUKA

KOCHA SIMBA AJITETEA, MASHABIKI WACHARUKA

4 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?