• ePaper
Saturday, January 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

TASAF ILIVYOCHOCHEA KILIMO, KUBADILI MAISHA YA WANANCHI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 9, 2026
in Makala
0
TASAF ILIVYOCHOCHEA KILIMO, KUBADILI MAISHA YA WANANCHI

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Meru akiwa na viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), walipofika ofisini kwake kumsalimia wakiwa njiani kwenda kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na mfuko huo, Meru.

0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Suleiman Jongo

MOJA ya msukumo mkubwa unaowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kutanua fursa za kiuchumi kwa wananchi walioko pembezoni, hususan vijijini.

Msukumo huo unalenga kuimarisha uchumi wa wananchi, kutatua changamoto zinazokwamisha uzalishaji na kuongeza kasi ya maendeleo kupitia sekta mbalimbali kikiwamo kilimo.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ni moja ya taasisi zinazohusika moja kwa maoja katika mkakati wa kupambana na umaskini hasa kwa kaya zenye kipato duni.

Kufanikisha jitihada za kuimarisha maisha ya wananchi, TASAF imeendelea kuwa mkombozi wa kaya masknini kutokana na uendeshaji wa miradi yenye lengo la kuinua kipato na kuleta matokeo mazuri siyo kwa kaya husika tu, bali pia katika kata, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.

Kupitia miradi ya TASAF, idadi ya Watanzania wenye umaskini uliopindukia imeendelea kupungua, ingawa haijafikia asilimia 100.

Desemba mwaka jana, TASAF ilihitimisha safari ya miaka mitano ya Mkakati wa Kupunguza Umaskini iliokuwa ikiutekeleza katika mikoa mitano na kuhusisha halmashauri 33.

Akitoa maelezo kuhusu mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2020, Mkurugenzi wa Miradi TASAF, John Stephen, alisema ulitekelezwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo ambao uko chini ya Shirika la Wazalishaji na Wauzaji Wakubwa wa Mafuta Duniani (OPEC).

Stephen alisema “Tumekuwa na miradi mikubwa miwili ‘PSSN II’ ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2020 na umekwisha Septemba mwaka 2025, ule ndio mradi mkubwa kabisa ambao ulifadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) na wafadhili wengine wasiopungua 15.

“Pamoja na huo tuna mradi mwingine ambao ulifadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ambao uko chini ya Shirika la Wazalishaji Wakubwa wa Mafuta Dunia (OPEC), Mradi wa Kupunguza Umaskini Awamu ya Nne (TPRP IV) ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2020, (ulimalizika Desemba 2025)” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema utekelezaji wa mradi wa kupunguza umaskini kwa Halmashauri ya Meru mkoani Arusha ulitia fora kutokana mambo makubwa yaliyofanikisha kufikiwa kwa malengo.

“Huu mradi wa OPEC ulikuwa unatekelezwa katika mikoa mitano na hlmashauri 33, lakini katika hizo halmashauri moja ya mfano ni halmashauri ya Meru, imefanya kazi nzuri sana,” alisema.

MKURUGENZI AELEZA

Akizungumzia tathmini ya miradi ya TASAF kwa upande wa halmashauri yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru, Zainab Juma alisema kuwa, imani waliyooneshwa na wadau wa maendeleo (TASAF) imelipwa kwa vitendo.

Mkurugenzi mtendaji huyo alimshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuridhia upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi, akieleza kuwa bila ridhaa yake halmashauri hiyo isingepokea fedha hizo.

Alitaja moja ya sekta zilizonufaika na mradi huo, ni kilimo na ufugaji, ambapo halmashauri yake imepata mradi wa umwagiliaji ambao umeongeza uzalishaji wa mazao.

Aliutaja mradi huo ni Skimu ya Umwagiliaji Ngabobo, ambayo wananchi wameanza kunufaika nayo kupitia kilimo cha mazao ya bustani zikiwamo nyanya, vitunguu, kabichi na mbogamboga, hivyo kuongeza kipato na shughuli za ufugaji.

Zainab alieleza kuwa, utekelezaji mzuri wa miradi unatokana na ushirikiano kati ya halmashauri, kata na watumishi wa ngazi ya chini, ambapo kila mradi unasimamiwa kwa pamoja na kuchukuliwa ni mali ya halmashauri na wananchi, badala ya kuutazama ni miliki ya taasisi iliyofadhili.

MRATIBU WA TASAF MERU

Mratibu wa TASAF katika Halmashauri ya Meru, Edwin Serunkuma akiuzungumzaia mradi huo wa OPEC IV, alisema umeacha alama kupitia skimu ya umwagiliaji ya Ngabobo ambayo ilijengwa katika awamu mbili.

Alisema mwaka 2022/2023 skimu hiyo ilijengwa kilometa moja kwa gharama ya sh. milioni 66.

Pia, zikajengwa kilometa 7.2 kwa gharama ya sh. milioni 401 na kufanya gharama ya jumla kwa mradi huo kuwa sh. milioni 467 kwa kilometa 8.2 zilizojengwa.

Serunkuma alisema hekta 800 zitanufaika kwa umwagiliaji kupitia skimu hiyo huku kilimo kikubwa kinachofanyika cha mbogamboga, “wanalima nyanya, vitunguu kabichi…pia mradi huo unatumika kumwagilia mazao ya chakula kama mahindi, maharage.”

Ofisa Kilimo Kata ya Ngabobo, Godvoice Mbukoi alisema wanufaika wa mradi huo kwa upande wa wakulima ni 4,482.

“Tunaishukuru serikali kwa kutuletea mradi huu kwa sababu, mwanzo kulikuwapo na changamoto nyingi, wakulima walikuwa wanalima maeneo machache kwa kuwa maji yalikuwa hayafiki kwa wakati shambani, lakini baada ya ujio wa mradi huu tija imeongezeka na kiwango cha kilimo kimepanda, kwa sababu maji yanatosheleza.

“Kabla mfreji huu kujengwa zilikuwa zikilimwa hekta 400, lakini sasa tunalima hekta 1,300 na mazao yalikuwa yakizalishwa machache, lakini sasa malori 10 hadi 12 yanatoka kila siku yakiwa na shehena ya bidhaa za shambani,” alieleza.

WAKULIMA WATOA USHUHUDA

Benjamin Kilua, mkulima katika Kijiji cha Ngabobo, alisema kabla ya kujengwa kwa mfereji huo wenye viwango bora, walikuwa wakitaabika kwa sababu kila Jumatatu walilazimika kuutengeneza mfereji uyliokuwapo awali ambao kwa kukosa viwango bora ulikuwa ukijaa mchanga na maji kutopita kwa usahihi.

“Hapo mwanzo hapa Ngabogo yalikuwa yakija magari matatu au manne kwa siku, lakini sasa ni historia, bahati nzuri hata mapato yanaonesha, yanakuja malori hadi 15 kwa siku.

“Hatua hiyo ni kutokana na wepesi wa maji kufika katika mashamba ya wakulima, maji yanaletwa kwa wakati, wakulima wanayapata kwa wakati na wanamwagilia kwa wakati, kwa sasa hakuna mashamba yaliyoathirika kwa kukosa maji,” alisisitiza.

Aliishukuru serikali chini ya Rais Dk. Samia kwa sababu Ngabobo ilikaa miaka mingi kabla ya kupata mradi huo, lakini baada ya Rais Samia kuingia madarakani ndipo wamenufaika.

“Awali tulikuwa tunaisikia tu TASAF, lakini sasa naamini hata walioanza kunufaika nayo miaka 20 iliyopita, sisi tumewapita kwa mapato ambayo tumeanza kuyapata miaka mitano tu iliyopita.

“Kwa hiyo tunaishukuru serikali, sasa unawakuta kina mama wa kimasai wako shambani wanalima wanapata mazao kwa wingi, kila kitu kimekaa vizuri, tunashukuru kwa kweli.

“Mimi ni mmoja wa wakulima wa mwanzo wa nyanya hapa Ngabobo, naijua historia vizuri, awali tulikuwa tunalima hekari mbili au tatu, kwa sasa mimi binafsi kwa mfano nalima hadi hekari 10, napata mazao mengi na faida tumeiona.

“Huko tuliko toka hata nyumba bora hazikuwepo hapa Ngabobo, lakini kwa miaka hii mitano mimi nina nyumba zaidi ya nne za matofali nimejenga kutokana na kilimo, sina kazi serikalini, mimi ni mkulima zaidi ya nyumba nne za ‘block’ (matofali) za kisasa kabisa, ukienda nyumbani utafikiri upo kwa mbunge kwa ajili ya kilimo,” alisema.

Josephine Naiso, mkazi wa Ngabobo, alisema awali walikuwa na changamoto kubwa ya maji, mferji uliokuwapo ulikuwa mchafu hali iliyosababisha maji kusumbua kuingia shambani.

“Pia tulikuwa tunakabiliwa na changamoto ya bei ndogo ya mazao, unaweza ukatumia sh. milioni moja kuandaa shamba, lakini ukaja ukapata sh. 200,000 au 300,000,” alibainisha.

Alitaja changamoto nyingine ni mazao kubaki shambani kwa kutopata wanunuzi, lakini sasa hali ni shwari, mavuno yameongezeka kwa kuwa mazao yananawiri.

Aliwasihi wananchi wenzake kuulinda mradi huo uendelee kutuoa tija katika kilimo.

ALICHOSEMA MKURUGENZI MTENDAJI

Akizungumza kuhusu utekelezaji wa miradi unaofanywa na TASAF, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Shadrack Mziray alisema Mradi wa Kupunguza Umaskini Awamu ya Nne (TPRP IV) umekuwa na mafanikio makubwa.

Mziray alisema mdari huo umechangia kwa kiwango kikubwa kuendeleza ajenda ya maendeleo ya taifa, hususan kupunguza umaskini, kuboresha huduma na kuwezesha jamii nchi nzima.

“Tangu kuanza kwa mradi huu Januari 2020, TPRP IV imejikita kimkakati kupunguza umaskini katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Njombe, Geita na Simiyu.

“Lengo kuu lilikuwa kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii na fursa za kuongeza kipato, hii imefanyika kwa kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu lengwa, mradi umewezesha ujenzi na ukarabati wa madarasa, vituo vya afya na vyanzo vya maji ambavyo sasa vinahudumia kaya za walengwa na jamii kwa ujumla.

“Uwekezaji huu umeongeza upatikanaji wa huduma, umepunguza umbali wa kufikia huduma za afya na maji, na kuimarisha mazingira wezeshi kwa ustawi wa jamii,” alieleza.

Pia, alisema mradi huo umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ustahimilivu wa kiuchumi kwa kuwa kaya zilisaidiwa kutanua wigo wa vyanzo vya kipato kupitia shughuli kama ajira binafsi katika sekta mbalimbali kikiwamo kilimo, ufugaji na shughuli nyingine za uzalishaji.

Alitaja matokeo ya mradi huo ni familia nyingi kuongeza kipato cha kaya, kuboresha usalama wa chakula na kuimarisha uwezo wa kukidhi mahitaji ya msingi.

Kwa mujibu wa Mziray, tathmini ya karibuni inaonesha kuwa mradi wa TPRP IV umenufaisha kaya takriban 200,007 kwa kiwango cha mwitikio wa asilimia 96.7, jambo linalothibitisha wigo mpana na faida kwa afua za mradi.

Previous Post

DK. SAMIA ATEUA, ATENGUA VIGOGO

Next Post

KATIBU MKUU CCM AWATAKA WANACHAMA KUSHIRIKI KIKAMILIFU VIKAO VYA MASHINA

Next Post
KATIBU MKUU CCM AWATAKA WANACHAMA KUSHIRIKI KIKAMILIFU VIKAO VYA MASHINA

KATIBU MKUU CCM AWATAKA WANACHAMA KUSHIRIKI KIKAMILIFU VIKAO VYA MASHINA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. MWINYI ANADI FURSA Z’BAR

RAIS DK. MWINYI ANADI FURSA Z’BAR

1 month ago
WASIRA ATABIRI RUNDO LA KURA KWA DK. SAMIA

WASIRA ATABIRI RUNDO LA KURA KWA DK. SAMIA

4 months ago

Popular News

  • SIMANZI WATOTO WAKIFIA NDANI YA SWIMMING POOL

    SIMANZI WATOTO WAKIFIA NDANI YA SWIMMING POOL

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AONYA WAVURUGA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA NA CHINA ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MRADI WA UMEMEJUA KISHAPU KULETA MAPINDUZI SEKTA YA NISHATI – MAKAMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KATIBU MKUU CCM AWATAKA WANACHAMA KUSHIRIKI KIKAMILIFU VIKAO VYA MASHINA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?