• ePaper
Thursday, September 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

CARRICK KOCHA MPYA MAN UNITED

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 15, 2026
in Burudani, Michezo
0
CARRICK KOCHA MPYA MAN UNITED
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

MANCHESTER, England

UONGOZI wa Klabu ya Manchester United umemtangaza Michael Carrick kuwa kocha wa muda wa kikosi hicho hadi mwishoni mwa msimu huu.

Katika benchi la ufundi hivi sasa, Carrick atasaidiana na beki wa zamani wa England, Steve Holland, Jonathan Woodgate, Jonny Evans na Travis Binnion.

Kiungo huyo wa zamani wa United mwenye umri wa miaka 44, awali alishawahi kuiongoza timu hiyo akiwa kocha wa muda kwa mechi tatu kufuatia aliyekuwa kocha Ole Gunnar Solskjaer kutimuliwa mwaka 2021.

Anatarajiwa kurejea katika Uwanja wa Old Trafford wakati timu yake ikiikaribisha Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England, utakaofanyika keshokutwa.

Manchester United imemtangaza Carrick kuwa kocha wa muda kufuatia Ruben Amorim kutimuliwa kutokana na mwenendo mbovu wa matokeo huku Darren Fletcher akiiongoza kwa muda mechi mbili.

“Ninajisikia faraja kuteuliwa kuwa kocha wa muda na kurejea katika kikosi cha Manchester United rasmi.

“Siamini kama nimechaguliwa mimi, lakini kikubwa ninataka kuhakikisha ninafanya kazi nzuri na kutimiza majukumu yangu ili kuhakikisha ninaondoa presha ya mashabiki iliyopo hivi sasa.

“Ninataka kuonyesha uwezo wa hali ya juu na kuiongoza timu kushinda katika michuano mbalimbali tunayoshiriki msimu huu.

“Ninaamini kila mmoja anatamani kupata burudani kutoka kwa wachezaji wa Manchester United, hilo linawezekana nitarudisha imani iliyopotea kwa muda,” alisema Carrick.

Kabla ya kuteuliwa kuwa kocha wa muda, Carrick alikutana na uongozi wa Manchester United na kukubaliana mambo mbalimbali.

(BBC)

Previous Post

SHAGEMBE ATAMBA

Next Post

MWIGULU APIGILIA MSUMARI

Next Post
MWIGULU APIGILIA MSUMARI

MWIGULU APIGILIA MSUMARI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA, PRISONS KIVUMBI LEO

YANGA, PRISONS KIVUMBI LEO

6 months ago

Uchumi wa Tanzania unaendelea kukua kwa asilimia 6.8

1 year ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?