• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. MWIGULU AKERWA MICHANGO SHULENI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 14, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. MWIGULU AKERWA MICHANGO SHULENI
0
SHARES
25
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IRENE MWASOMOLA

WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, amekerwa na tabia kuwachangisha fedha wazazi katika baadhi ya shule za umma kwa lengo la kuwalipa walimu wa kujitolea, hivyo ameziagiza halmashauri kubeba jukumu hilo kwa kutumia mapato ya ndani.

Pia, amesema maeneo ambayo kuna mahitaji ya walimu hao wa ziada, serikali za mitaa zibebe jukumu badala ya kuwapa mzigo huo wazazi.

Waziri Mkuu Dk. Nchemba aliyasema hayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe mkoani Katavi, jana, alipokuwa akizungumza na wananchi na kumhoji Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Shami Mwariko, kwa nini wazazi ndani ya eneo lake wanachangishwa fedha za kuwalipa walimu wa kujitolea.

Dk. Mwigulu alisema jukumu la kuajiri walimu ni la serikali na kwamba pale halmashauri zinapokuwa na mahitaji katika maeneo mengine hutumia mapato ya ndani, basi iwe hivyo hivyo kufanikisha malipo ya walimu wanaojitolea.

“Kila halmashauri tuna mapato ya ndani, tutumie mapato ya ndani kuhakikisha tunaendelea kuboresha haya mazingira. Palipo na mahitaji ya walimu serikali zetu za mitaa zichukue jukumu tusiwape wazazi kazi ya kufanya jukumu la serikali,” alisema.

Hata hivyo, Dk. Nchemba alionya kuwa, baada ya tamko hilo asisikie walimu wa kujitolea wameondolewa katika halmashauri hiyo.

Akizungumza kuhusu ujenzi wa vyoo, Waziri Mkuu Dk. Nchemba alisema baada ya miezi sita ya bajeti hataki kusikia shule yoyote ina upungufu wa matundu ya vyoo.

Alisema Mkurugenzi atakayeshindwa kujenga hata matundu ya vyoo atakuwa hatoshi katika jukumu hilo.

KUHUSU UKOSEFU WA DAWA

Aidha, Waziri Mkuu Dk. Mwigulu alimuagiza Kamanda wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi, kufanyia uchunguzi suala la ukosefu wa dawa katika hospitali zinazosema dawa hazipo haliyakuwa zipo.

Waziri Mkuu Nchemba alihoji kuwa duka la mtaani linatoa wapi dawa ambayo serikali inaikosa.

“Kamanda wa TAKUKURU fanya uchunguzi kwenye huu mchezo, usikute wananchi wanalazimishwa kununua dawa nje, serikali inaleta dawa hapa lakini hazipo, usikute kule mnakosema zipo wakanunue ni maduka yenu.

“Serikali imekuwa ikitoa fedha za ununuzi wa dawa na maeneo mengine nikipita naambiwa utesholevu wa dawa ni zaidi ya asilimia 90, lakini inatokea kila mwananchi akienda kutibiwa anaambiwa aende akanunue dawa maduka mengine.”

Alisema serikali imeendelea kutoa fedha za ununuzi wa dawa, ambapo zaidi ya sh. bilioni 1.8 zimetolewa kununua dawa na vifaa tiba ndani ya mkoa huo.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Dk. Mwigulu, amepata taarifa hata wale ambao kwenye sheria zetu wamepata msamaha wanaambiwa wakanunue dawa.

Pia, Waziri Mkuu Dk. Mwigulu aliagiza apate taarifa zote kuhusu wataalamu wa afya ambao walishindwa kufahamu dawa fulani ipo hospitalini kwa kushindwa kutambua  kutokana na kuandikwa jina la kampuni badala ya jina la dawa, badala yake wakawa wana waambia wananchi kuwa dawa hiyo haipo wakati ipo.

Alimuagiza Kamanda wa TAKUKURU na vyombo vingine mkoani humo kufuatilia migogoro yote na kujua nani alikuwa na maslahi binafsi na kusababisha migogoro katika mkoa huo.

Katika tukio lingine, Dk. Nchemba alimtaka Mtendaji wa Kijiji cha Majimoto kumtafutia eneo lingine mama ambaye serikali ya kijiji imechukua eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa zahanati.

Waziri Mkuu alielekeza watendaji kutochukua maeneo ya wananchi bila kutoa fidia kwa kigezo cha kutekeleza miradi ya maendeleo.

Katika tukio lingine Waziri Mkuu alikagua daraja la Sitalike katika mto Katuma, ambapo aliwataka watendaji kutekeleza majukumu yao na kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Alisema ujenzi wa daraja hilo unakwenda kubadilisha historia ya usafiri katika maeneo hayo. “Daraja hili limeweka tofauti na lile lililokuwepo awali ambalo halikuwa imara na lilikuwa likisababisha changamoto kwa wananchi na wasafirishaji,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Mwigulu daraja la Sitalike ni sehemu ya miradi ya madaraja inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuokoa maisha ya wananchi, kurahisisha usafiri na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi.

Pia alimwagiza Waziri wa Madini, Anthony Mavunde kufika katika Kata ya Sitalike kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge, kushughulikia kero ya uchimbaji, kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi ya masuala ya uchimbaji madini.

KASEKENYA

Akizungumza katika mkutano huo mbele ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, alisema serikali itakamlisha barabara ya Kibaoni wilayani Mlele mkoani humo kwa kiwango cha lami.

Alisema kukamilika kwa barabara hiyo kutakuwa kumeunganisha mkoa wa Katavi na Rukwa kwa asilimia 100.

KWAGILWA

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kwagilwa Reuben alisema idadi ya madaktari bingwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi imeongezeka kutoka wawili hadi kufikia 13.

Pia Kwagilwa alisema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amefanikiwa kujenga majengo ya utawala katika Halmashauri 143 kati ya 184 yaliyopo kote nchini.

MKUU WA MKOA

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwamvua Mrindoko, alisema serikali imejenga hospitali mpya za halmashauri nne na kufanya mkoa huo kuwa na jumla ya hospitali tano za halmashauri.

Aliongeza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa katika mkoa huo ni asilimia 92.

Vilevile alisema serikali chini ya Rais Dk. Samia imejenga shule mpya 150 kati ya hizo 107 za msingi na 43 ni za sekondari.

WANANCHI

Aidha katika tukio hilo baadhi ya wananchi wamewasilisha malalamiko yao kwa Waziri Mkuu, kuhusu baadhi ya watendaji katika wilaya hiyo kutofanya kazi zao kwa weledi hivyo kukwamisha maendeleo.

Fainel Maganga alisema kutowajibika kwa baadhi ya watendaji imekuwa ikisababisha kupungua kwa imani ya wananchi kwa baadhi ya watumishi wa umma, huku akisisitiza umuhimu wa watendaji hao kuwajibika ipasavyo, kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati na kwa usawa.

Naye Christopher Luhamba aliiomba serikali kushughulikia changamoto ya kimazingira inayotokana na wachimbaji kumwaga kemikali kwenye mto, hali inayohatarisha usalama wao.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA AWALILIA WATUMISHI WALIOFARIKI AJALI YA BOTI KIGOMA

Next Post

AZAM, YANGA MECHI YA KISASI, HESHIMA

Next Post
AZAM, YANGA MECHI YA KISASI, HESHIMA

AZAM, YANGA MECHI YA KISASI, HESHIMA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TUME YAUNDWA KUBAINI TUHUMA UZIMAJI X -RAY

TUME YAUNDWA KUBAINI TUHUMA UZIMAJI X -RAY

4 months ago
DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

7 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?