• ePaper
Saturday, June 6, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

KIBADENI, MANARA, MAYAY WAFUNGUKA MANUFAA YA AMANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 11, 2026
in Burudani, Kitaifa, Michezo
0
KIBADENI, MANARA, MAYAY WAFUNGUKA MANUFAA YA AMANI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WACHEZAJI wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, Abdallah Kibadeni, Sunday Manara na Ally Mayay, wamesema kuwa ni vyema kuitunza amani ya nchi kwani ndiyo msingi wa umoja na mshikamano.

Waliyasema hayo katika hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Nyota wa zamani wa Simba, Kibadeni, alisema kuwa amani ni jambo la msingi katika nchi, pia linaongeza morari kwa wanamichezo kuweza kufanya kazi zao kwa uhuru na mshikamano.

“Niwaambie tu Watanzania na wanamichezo wote kwa ujumla, amani ni jambo la msingi katika nchi hivyo inapaswa kudumishwa ili kuendeleza mpira wetu wa miguu katika anga za juu zaidi.

Naye nyota wa zamani wa Yanga, Manara alisema kuwa kila Mtanzania anatakiwa kudumisha, kuilinda amani nchini.

Alisema kuwa endapo amani ikikosekana hata mpira hauwezi kuchezekeka ambao ndiyo ajira ya vijana wengi hapa nchini inayowasaidia kuwaingizia kipato.

“Niseme tu kuwa kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa kuilinda na kuithamini amani katika nchi yetu, ikikosekana amani hakuna kitu ambacho kitafanyia ndani ya nchi na hata nchi jirani pia wataogopa kuja kuwekeza na kucheza soka hapa kwetu,” alisema Manara.

Kwa upande wake nyota wa zamani wa Yanga, Mayay alisema kuwa kila mmoja anajua umuhimu wa amani nchini, hivyo Watanzania wanapaswa kuilinda kwa hali na mali.

Alisema kuwa ili wachezaji waweze kuwa huru na kwenda kucheza katika mataifa mbalimbali lazima nchi wanayotoka iwe na amani ili waweze kupata kibali cha kwenda nchi nyingine.

“Tumekuwa tukiheshimika na kuthaminiwa kutokana na Tanzania kujulikana na nchi yenye amani na utulivu, hivyo ni jukumu letu kuilinda kwa hali na mali ili kusitokee na machafuko ambayo yataiharibia sifa nchi yetu,” alisema Mayay.

Previous Post

KOCHA YANGA AIPANIA AZAM MAPINDUZI CUP

Next Post

NANAUKA AJA KIMKAKATI NEEMA YAZIDI KUWASHUKIA VIJANA

Next Post
NANAUKA AJA KIMKAKATI NEEMA YAZIDI KUWASHUKIA VIJANA

NANAUKA AJA KIMKAKATI NEEMA YAZIDI KUWASHUKIA VIJANA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MIGIRO AWATAKA MAWAZIRI KUHUDHURIA VIKAO VYA MASHINA

DK. MIGIRO AWATAKA MAWAZIRI KUHUDHURIA VIKAO VYA MASHINA

4 months ago
DK. NCHIMBI ATAJA FAIDA UKARABATI RELI TAZARA

DK. NCHIMBI ATAJA FAIDA UKARABATI RELI TAZARA

7 months ago

Popular News

  • MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

    MWANZA KINARA USIMAMIZI MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WFP KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA USIMAMIZI WA MAAFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HESHIMA KUBWA KWA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU: MAMBO MAZURI YANAKUJA, AIPA TANO SERENGETI BOYS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERENGETI BOYS HESHIMA KILA KONA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?