• ePaper
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA, AZAM FC FAINALI YA KIBABE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 13, 2026
in Burudani, Michezo
0
YANGA, AZAM FC FAINALI YA KIBABE
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

TIMU za Yanga na Azam FC kutoka Tanzania Bara, leo zitashuka katika fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026, inayotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Miamba hiyo itavaana saa 10:30 jioni katika Uwanja wa Gombani Complex, Pemba.

Yanga imetinga fainali baada ya kuitoa TRA United kwa ushindi wa bao 1-0 wakati Azam FC ikiiondosha Simba kwa ushindi wa bao 1-0, wiki iliyopita.

Akizungumza maandalizi ya mchezo huo, Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge, alisema kikosi chake kipo tayari kwa fainali na wamejiandaa kuwa bora uwanjani kuliko wapinzani wao.

Alisema haitakuwa rahisi kwani timu zote zina ubora mkubwa, lakini lengo lao ni kupata ushindi katika mtanange huo.

“Tunajua Yanga ndiyo timu bora zaidi Tanzania hivi sasa, lakini sisi tutakuwa bora zaidi yao kwa sababu tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri na kutimiza yale malengo yetu ambayo tumejiwekea.

“Wachezaji wote wako tayari kwa mechi, pia ninawaamini watafanya vizuri,” alisema Ibenge.

Nyota wa timu hiyo, Nassor Saadun alisema kila mchezaji amejiandaa vizuri kukabiliana na Yanga katika mchezo huo, watafuata maelekezo ya walimu wao kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kutwaa kombe.

“Malengo yetu ni kuchukua ubingwa wa Mapinduzi tutahakikisha tunacheza vizuri na kuzingatia yale tuliyofundisha katika viwanja vya mazoezi, tunatambua mchezo utakuwa mgumu lakini sisi tutapambana kupata ushindi,” alisema.

Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, alisema maandalizi yako vizuri kuelekea katika fainali hiyo, pia wamejipanga kuchukua ubingwa huo ingawa mchezo utakuwa na ushindani mkubwa.

“Tunatambua fainali itakuwa na ugumu lakini tumejipanga kufanya vizuri na wachezaji wamefanya mazoezi ya kutosha kuhakikisha wanacheza katika kiwango kizuri ambacho kitatupa ushindi,” alisema.

Kocha huyo alisema haijalishi mechi itakuwa na ugumu kiasi gani, lakini watapambana kuhakikisha wanachukua ubingwa huo.

Previous Post

WASOMI WADOKEZA CHANZO WANAFUNZI KUANDIKA MATUSI

Next Post

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, MSHIKAMANO

Next Post
RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, MSHIKAMANO

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, MSHIKAMANO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

6 months ago
DK. SAMIA KUVALIA NJUGA SHIDA YA MAJI

DK. SAMIA KUVALIA NJUGA SHIDA YA MAJI

6 months ago

Popular News

  • MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

    MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?