• ePaper
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

KOFANE ALIVYOANDIKA HISTORIA CAMEROON AFCON MSIMU HUU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 18, 2026
in Makala, MAKALA BURUDANI, MAKALA MICHEZO
0
KOFANE ALIVYOANDIKA HISTORIA CAMEROON AFCON MSIMU HUU
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RABAT, Morocco

FAINALI za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), leo inatarajiwa kufikia tamati nchini Morocco.

Fainali hizo zilianza tangu Desemba 21, mwaka huu kabla ya kuhitimishwa leo ambapo timu mbalimbali zilishiriki na zile ambazo zilionyesha uwezo mkubwa zaidi, ndizo zitakazocheza fainali leo.

Kimsingi katika michuano ya msimu huu, tumeona ushindani wa hali ya juu ikiwemo wachezaji vijana kupewa nafasi na kuonyesha kiwango cha hali ya juu tofauti na mashabiki wengi walivyotarajia hapo awali.

Christian Michel Kofane ni mmoja wa wachezaji wenye umri mdogo zaidi waliofanya mambo makubwa na kuweka historia katika michuano ya AFCON 2025.

Kinda huyu alionyesha kiwango cha aina yake katika michuano hiyo ikiwemo kuisaidia Cameroon kutinga hatua ya robo fainali ambapo baadaye iliondolewa katika fainali hizo dhidi ya Morocco, baada ya kukubali kufungwa mabao 2-0 .

Kinda huyu alicheza mechi nne katika michuano ya AFCON 2025 na kuonyesha kiwango ambacho kitamfanya aendelee kuaminiwa zaidi katika michuano mbalimbali timu yake ya taifa itakayoshiriki.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, ndiye aliyeweka historia ya aina yake kikosini kuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mdogo zaidi kuisaidia timu kutinga hatua ya robo fainali.

Kofane alifunga bao hilo katika mechi ya hatua ya 16 bora dhidi ya Afrika Kusini ambapo Cameroon iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, ikiwemo kufunga bao jingine muhimu mechi za hatua ya makundi dhidi ya Msumbiji, Cameroon ikishinda 2-1.

Kinda huyo alionekana kunawiri zaidi katika mchezo huo wa hatua ya 16 bora Uwanja wa Al Barid, Rabat, Morocco.

Katika mchezo huo, Cameroon iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Afrika Kusini ambapo Kofane alifunga bao dakika ya 47 akipokea pasi ya Mahamadou Nagida.

Kinda huyo anayekipiga katika kikosi cha Bayer Leverkusen, alionyesha kiwango bora katika mchezo huo na kuisaidia timu kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya AFCON msimu huu.

Kofane alionekana kuchomoza katika michuano ya msimu huu akifuata nyayo za Roger Milla ambaye aliwahi kuisaidia Cameroon kubeba AFCON mara mbili mwaka 1984 na 1988 huku akiibuka mfungaji bora wa fainali za mwaka 1988.

Pia ametajwa kufuata nyayo za mchezaji wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto’o aliyebeba kombe hilo mara mbili mwaka 2000 na 2002 huku akiibuka mfungaji bora wa muda wote akifikisha mabao 18.

Wachezaji wengine waliowahi kuweka historia katika kikosi cha Cameroon ni Patrick Mboma, Vincent Aboubakar na Francois Omam-Biyik.

Kofane alianza kung’ara tangu alipopita katika timu mbalimbali za vijana ikiwemo AS Vatican na AS Nylon.

Alisema amefurahia kuisaidia timu kufanya vyema katika michuano hiyo msimu huu ikiwemo kufunga bao lililowapeleka hatua ya robo fainali msimu huu.

Alisema japokuwa hawakufanikiwa kusonga mbele hatua ya nusu fainali, amejifunza mengi katika michuano hiyo aliyoshiriki kwa mara ya kwanza na kupewa nafasi kubwa ya kucheza.

Alisema ana imani ataendelea kupambana kuhakikisha anatunza kiwango chake ili kuendelea kuitumikia Cameroon na kuisaidia kufanya vyema zaidi katika michuano ijayo.

“Nilikaa kwa muda katika kikosi cha AS Vatican kabla ya kutimkia AS Nylon ambapo niliwahi kufunga bao kwa tiki-taka na hapo ndipo nilianza kujulikana zaidi.

“Baadaye nilihamia Albacete na kuzoea mazingira mapema zaidi tofauti na wengi walivyofikiria, nimekuwa nikijifunza vitu vipya kutoka kwa wachezaji wenzangu walionitangulia, nina imani nitaendelea kufanya vizuri zaidi katika mechi zijazo za ngazi ya klabu na timu ya taifa.

“Samuel Eto’o ni mmoja wa wakongwe wa Cameroon ambao wamekuwa wakinivutia muda wote na ninajifunza vingi kupitia kwake.

“Baada ya mechi hunifuata na kuniusia mambo mbalimbali, ananilea kama mwanaye kitu ambacho kinanipa ujasiri zaidi kipindi nikiwa uwanjani,” alisema.

WASIFU:

JINA: Christian Michel Kofane

KUZALIWA: Julai 26, 2006

MAHALI: Douala, Cameroon

UMRI: Miaka 19

NAFASI: Mshambuliaji

TIMU: Bayer Leverkusen/Cameroon

Previous Post

MIGIRO KATIBU MKUU WA  KWANZA MWANAMKE NA MIKAKATI YA KUIMARISHA MASHINA KATIKA MITAA

Next Post

MWIGULU AKAZIA MAMBO NYETI

Next Post
MWIGULU AKAZIA MAMBO NYETI

MWIGULU AKAZIA MAMBO NYETI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI: NYERERE MFANO WA UADILIFU

DK. NCHIMBI: NYERERE MFANO WA UADILIFU

1 week ago
DK. SAMIA ANAVYOTAFSIRI ‘KAZI NA UTU’ KWA VITENDO

DK. SAMIA ANAVYOTAFSIRI ‘KAZI NA UTU’ KWA VITENDO

7 months ago

Popular News

  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NEEMA YAJA, MIKAKATI HADHARANI KUINUA VIJANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?