• ePaper
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

MIGIRO KATIBU MKUU WA  KWANZA MWANAMKE NA MIKAKATI YA KUIMARISHA MASHINA KATIKA MITAA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 18, 2026
in Makala
0
MIGIRO KATIBU MKUU WA  KWANZA MWANAMKE NA MIKAKATI YA KUIMARISHA MASHINA KATIKA MITAA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IRENE MWASOMOLA

MWANAMKE ameendelea kuwa nguzo muhimu katika kuchangia matokeo chanya, yenye kuleta mbadiliko makubwa katika nyanja mbalimbali za kisiasa na kijamii.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Asha Rose Migiro, ni mfano hai wa uwezo na mchango mkubwa wa mwanamke katika nyanja za siasa, uongozi na utumishi wa umma.

Dk. Migiro ni Katibu Mkuu wa 13 wa CCM, anaandika historia ya kwanza ya chama hicho kuongozwa na mwanamke, huku akianza kazi kwa kufanya mageuzi makubwa ya kukiimarisha Chama kuanzia ngazi ya mashina.

Balozi Dk. Migiro ni Katibu Mkuu wa 13 akitanguliwa na Piusi Msekwa aliyeongoza mwaka 1977-1981, Balozi Daudi Mwakawango 1981-1982, Rashid Kawawa 1982-1990, Horace Kolimba 1990-1995, Lawrence Gama 1995-1997, Philip Mangula 1997-2007, Yusuph Makamba 2007-2011.

Wengine ni Wilson Mukama mwaka 2011-2012,  Abdurahman Kinana 2012-2018,Dk. Bashuru Kakulwa mwaka 2018-2021, Daniel Chongolo mwaka 2021- 2023 na Dk. Emmanuel Nchimbi Januri 2024 hadi Agosti mwaka 2025.

Katibu Mkuu Balozi Dk. Migiro aliteuliwa Agosti 23 mwaka jana, akichukua nafasi ya Balozi Dk. Emanuel Nchimbi ambaye aliteuliwa kuwa Mgombea Mwenza wa Urais ambaye ndiye Makamu wa Rais wa sasa. 

Uwezo na uchapakazi wa Mwanadiplomasia Balozi Dk. Asha Rose Migiro unaendelea kuonekana, kuleta matumaini mapya kwa wana CCM wa ngazi ya chini kabisa ambao ni mabalozi wa mashina.

ZIARA YAKE YA KWANZA ILIVYOTIKISA

Kuanzia Januari saba mwaka huu Dk. Migiro alifanya ziara ya kwanza, tangu ateuliwe kuwa Katibu Mkuu katika Mkoa wa Dar es Salaam, alikutana na kufanya mazungumzo na mabalozi wa mashina katika wilaya zote za mkoa huo ndani ya siku tatu.

Akizungumza  katika Wilaya ya Ilala Balozi huyo alisema, shina ndiyo lina beba umadhubuti wa CCM, huku akiwataka viongozi wa Chama kutoka ngazi ya juu, kuanzia wa kitaifa kushiriki vikao vya mashina na kuwa sehemu ya kutatua changamoto.

Balozi Dk. Migiro alisema, CCM imejipanga kwenda kuimarisha na kuhuisha mashina katika maeneo mbalimbali ambayo viongozi hao hawapo au walifariki dunia.

Alisema uhai wa CCM uko katika mashina, kwani ndiko uongozi wa Chama unaonesha uhalali wake kwa kuwa karibu na wananchi.

Aliongeza kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya maendeleo na mashina kutokana na umuhimu wao ndani ya CCM na serikali kwa ujumla.

“Katika mashina ndipo tunapoanza kutafuta wanachama na hapo ndipo Chama Cha Mapinduzi kinaonyesha uhalali wake katika kuwatumikia wananchi,”alisema.

Pia Katibu Mkuu huyo, aliwataka mabalozi wa mashina kuendelea kuweka kumbukumbu za wanachama, kujua wanafanya nini wanajihusisha na nini na kwamba, mashina ni sehemu ya usalama kwa taifa.

Balozi huyo aliwataka mabalozi wa mashina, kuendelea kuenzi alama za CCM, ikiwemo bendera za Chama.

“Viongozi wa ngazi za wilaya na ngazi mbalimbali,  tukiwa katika mashina lazima  tushiriki katika vikao, viongozi wa mashina, matawi na kata tuwe madhubuti kuwavuta viongozi wenzetu washiriki mikutano mbalimbali na utatuzi wa yale tunayopitia katika mashina na matawi yetu,”alisema.

Hata  hivyo, aliwataka Makatibu wa Itikadi na Uenezi kushirikiana na viongozi wa mashina katika madarasa ya itikadi, kwa kuwa mashina ndiyo madarasa ya kwanza ya itikadi na wananchama wanajifunza misingi ya CCM kupitia hapo.

Kwa mujibu wa Balozi huyo, ni dhamira ya Rais Dk. Samia kuhakikisha Chama kinakuwa madhubuti kuanzia ngazi ya shina.

Vile vile aliwataka, viongozi wa mashina kushirikiana na madiwani katika kufuatilia miradi inayotekelezwa na vitega uchumi vya CCM.

Ni muhimu viongozi wa shina na ngazi nyingine kufanya kazi kwa kuzingatia utu wa Mtanzania.

SIRI UBORA WA CCM

Akizungumza na mabalozi wa mashina wa Wilaya ya Ilala alisema ubora wa CCM unatokana na siasa zake safi, kushawishi wananchi kwa hoja na namna inavyojenga imani ya kudumu.

Alisema itikadi ya CCM itabaki katika kuthamini utu na kwamba chama  kitaendelea kukubalika zaidi kuliko chochote nchini.

“Ubora wa CCM unatokana na siasa yake, siasa yetu ni kuhamasisha wananchi, kuwashawishi kwa hoja na kujenga imani ya kudumu, ndiyo maana bado CCM kitanabaki kuwa Chama kinachokubalika zaidi kuliko vyama vyote kutokana na siasa yake,”alisema.

Akizungumzia dola alisema nia ya kushika dola ni kujenga utu wa Mtanzania na kwamba CCM itaendelea kujenga utu huo kupitia huduma za afya, elimu, ujenzi wa miundombinu na ukuaji wa uchumi.

Pia alisema CCM imejengwa kwa misingi ya umoja na inatoa maendeleo yasiyo na ubaguzi na kwamba ndiyo maana kila Mtanzania ana fursa sawa.

“Chini ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mtanzania awe mwa na CCM asiwe mwana CCM wote tunakuwa na fursa sawa ya kufanya biashara, kugombea na kupata uongozi, kusoma na kuwekeza katika nchi yetu,” alisema.

Alisema umoja wa wana CCM ndiyo ushindi wa mambo mbalimbali, ikiwemo maendeleo na taifa kuwa na amani.

Balozi Dk. Migiro alisema, CCM itaendelea kuimarisha mahusiano na wana chama na wasio wanachama kwa lengo la kuleta maendeleo jumuishi.

“Tumeambiwa kuwa mashina ni sehemu muhimu ya usalama wa jamii yetu na usalama wa taifa letu, hivyo tutakuwa na wajibu wa kuhakikisha watu ambao tunaishi nao, tunajua wanafanya nini na tunajua yale wanayoyafanya yanakuwa salama kwa taifa, 

Tunajua hivi sasa balozi wa shina anaweza kuwa na nyumba nyingi sana, hivyo kupitia vikao vyetu tutaangalia ni namna gani balozi wa shina, apate mzigo ambao anaweza kuubeba twende pamoja kuhakikisha chama chetu kinaendelea kuwa chama kiongozi na kinaendelea kushika dola kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa jumla,” alisema.

MABALOZI  WA MASHINA

Kwa upande wake, Balozi wa Shina namba nne Temeke Abdu Selemani Bilali, alimshukuru Balozi Dk. Migiro kwa kuona haja ya kuzungumza na  mabalozi wanaofanya kazi kubwa usiku na mchana ya kukijenga Chama.

Mjumbe wa Shina namba moja Mtaa wa Mbezi Kati Wilaya ya Kinondoni Obedi Ndasipa, aliomba Chama kuona haja ya kupitia upya idadi ya nyumba wanazoziongoza  zipungue kutoka 100 angalau ziwe 20.

Mjumbe wa Shina namba tano Tawi la Mzimuni  Rosemary Kambena, aliomba CCM kuona namna ya kuwapa semina za mara kwa mara kuongeza ufanisi katika utendaji.

Mjumbe wa Shina namba mbili Kibamba Hospitali Norbert Mbena, aliomba chama kuwapatia vitambulisho maalumu vitakavyo watambulisha na kuwasaidia kupata huduma mbalimbali serikalini.

KIHONGOSI

Kwa upande wake,  Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Kihongosi alisema mkoa huo uko imara na utekelezaji wa Ilani unaendelea.

“Dar es Salaam iko salama kweli kweli kwa sababu ya umoja na mshikamano wa viongozi na wana chama wao katika kukijenga chama.”alisema.

Alimpongeza Katibu Mkuu kwa kuamua kushuka chini katika mashina na kwamba hatua hiyo inathibitisha kuwa amedhamiria kufanya mageuzi makubwa ndani ya CCM.

MWENYEKITI CCM DAR ES SALAAM

Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Juma Simba Gaddafy, alimpongeza Katibu Mkuu Dk. Migiro kuanza ziara yake mkoani humo na dhamira ya kukutana na wajumbe wa mashina ina dhamira njema ya kuendelea kukijenga chama.

Gadafi, alisema ziara ya Katibu Mkuu huyo, inatoa darasa la itikadi na kukumbusha umuhimu wa mabalozi wa mashina.

Alisema mabalozi wa mashina ndiyo wanaweza kusaidia vyombo vya usalama, katika suala la ulinzi na usalama, hivyo mabalozi wana umuhimu mkubwa kwa chama na serikali.

Gadafi alisema, CCM Dar es Salaam iko tayari kwenda kuhuisha mabalozi, wa mashina katika maeneo ambayo hayana mabalozi hao kwa sasa.

DK. MIGIRO NI NANI

Balozi Dk. Migiro ni mwanasiasa na mwanadiploamasia aliyezaliwa mwaka 1956, huko Songea mkoani Ruvuma.

Amefanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi, ikiwemo nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 2007-2012.

Pia Balozi Dk. Migiro aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza mwaka 2016.

Katika utumishi wa umma Balozi huyo, aliandika historia ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa kwanza mwanamke aliyeongoza wizara hiyo. Mwaka 2015 Balozi Dk. Migiro aliandika historia kwa kuonyesha nia ya kugombea Urais kupitia CCM katika uchaguzi ambao Dk. John Magufuli ambaye sasa ni marehemu aliibuka mshindi.

Previous Post

SAFARI KUMALIZA CHANGAMOTO UMEME IRINGA, DODOMA YAIVA

Next Post

KOFANE ALIVYOANDIKA HISTORIA CAMEROON AFCON MSIMU HUU

Next Post
KOFANE ALIVYOANDIKA HISTORIA CAMEROON AFCON MSIMU HUU

KOFANE ALIVYOANDIKA HISTORIA CAMEROON AFCON MSIMU HUU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMBA HESABU KALI, YANGA NI USHINDI TU

SIMBA HESABU KALI, YANGA NI USHINDI TU

2 months ago
KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA JENGO LA GHOROFA 10 CBE

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA JENGO LA GHOROFA 10 CBE

1 month ago

Popular News

  • MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

    MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?