• ePaper
Wednesday, June 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA JENGO LA GHOROFA 10 CBE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 12, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA JENGO LA GHOROFA 10 CBE
0
SHARES
16
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb), ameeleza kuridhishwa kwake na hatua ya ujenzi wa jengo la kisasa la Vipimo na Viwango katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Machi 12, 2026, Mwanyika amebainisha kuwa mradi huo wa ghorofa 10 umefikia asilimia 93 ya utekelezaji wake, jambo linaloashiria usimamizi madhubuti na weledi katika ukamilishaji wa Jengo Jengo hilo ili kukidhi ongezeko la wanafunzi wanaodahiliwa kila mwaka.

Vilevile, Mwenyekiti huyo ametoa rai kwa uongozi wa chuo kuendelea kutoa na kuimarisha elimu ya kati (middle-level education) katika fani za biashara hususani ujasiliamali kwa kuwa ni nyenzo adhimu kwa wahitimu wanaojiandaa kuingia kwenye soko la ajira binafsi na

Kutasaidia kuongeza hadhi ya chuo na kuchochea ari ya wanafunzi wengi zaidi kujiunga na taasisi hiyo.

Amesema kuwa uimara wa chuo unategemea ubora wa mafunzo unayoyatoa na uwezo wake wa kuzalisha wataalamu wenye ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo (Mb), amefafanua kuwa mradi huo unatekelezwa kupitia bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2025/26 na unatarajiwa kuwa na uwezo wa kubeba zaidi ya wanafunzi 4,000 kwa wakati mmoja.

Aidha, amebainisha kuwa Jengo hilo la Vipimo na Viwango litakuwa kitovu cha mafunzo ya masoko na nyanja mbalimbali za kibiashara ambazo zinahitajika kwa kiasi kikubwa kulingana na mwelekeo wa sasa wa uchumi wa viwanda.

Naye Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Edda Lwoga, ameeleza kuwa mradi huo ulioanza Mei 25, 2023, umekuwa mhimili wa mabadiliko makubwa ya kitaaluma chuoni hapo. Alibainisha kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutaongeza fursa za udahili kwa wanafunzi wengi wanaohitaji masomo ya biashara na ujasiriamali, ikiwemo kozi fupi ambazo zimekuwa na mahitaji makubwa kwa wadau wa sekta binafsi.

Previous Post

WAZIRI KAIRUKI ASISITIZA MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MAWASILIANO

Next Post

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TABORA, UZALISHAJI WAANZA RASMI

Next Post
KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TABORA, UZALISHAJI WAANZA RASMI

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TABORA, UZALISHAJI WAANZA RASMI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI ATOA  AHADI KWA  DK. SAMIA

DK. NCHIMBI ATOA AHADI KWA DK. SAMIA

10 months ago
USALAMA MZURI KUWALETA NCHINI WABUNGE 2000 IPU

USALAMA MZURI KUWALETA NCHINI WABUNGE 2000 IPU

2 months ago

Popular News

  • WABUNGE WAIPONGEZA NSSF NA PSSSF KWA KUANZISHA SKIMU YA HIFADHI KWA WALIOJIAJIRI NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA NGOZI

    WABUNGE WAIPONGEZA NSSF NA PSSSF KWA KUANZISHA SKIMU YA HIFADHI KWA WALIOJIAJIRI NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA NGOZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICL

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAKAGUZI WA CAF WARIDHISHWA NA MAENDELEO YA VIWANJA VYA AFCON 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MKAKATI KUDHIBITI VIFO WAJAWAZITO WAANIKWA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WASOMI, WANASIASA WAKOSHWA TOZO KUCHANGIA BIMA YA AFYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?