• ePaper
Friday, May 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

BAADA YA HEROIN, COCAINE KUDHIBITIWA: ‘MATEJA’ WAGEUKIA DAWA ZA HOSPITALI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 16, 2026
in Habari, Kitaifa, RIPOTI MAALUMU
0
BAADA YA HEROIN, COCAINE KUDHIBITIWA: ‘MATEJA’ WAGEUKIA DAWA ZA HOSPITALI
0
SHARES
14
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IRENE MWASOMOLA

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imepata mafanikio kwa kupunguza kiasi kikubwa cha upatikanaji wa dawa za kulevya mitaani.

Dawa hatarishi kama heroin na cocaine hazipatikani kirahisi kama ilivyokuwa awali, ambapo idadi kubwa ya vijana nchini waliingia katika matumizi ya dawa hizo.

Januari 9, mwaka huu, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano kati ya DCEA, vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi.

Ameeleza mafanikio hayo yameifanya Tanzania kuondokana na taswira ya kuwa njia ya kupitisha dawa za kulevya kwenda nchi nyingine.

Amesema hata ukaguzi mkali uliokuwa ukifanywa kwa wasafiri wa Kitanzania katika viwanja vya ndege vya nje ya nchi umepungua kutokana na mafanikio hayo.

Hata hivyo, Lyimo amesema pengo lililoachwa na kukosekana kwa dawa za kulevya sasa limezua changamoto ya kijamii, ambapo vijana wengi wameingia katika matumizi ya pombe kupita kiasi.

Mbali na matumizi ya pombe kupita kiasi, idadi kubwa ya vijana hivi sasa wamebuni mbinu mpya ya kutafuta mbadala wa dawa hizo.

Uchunguzi uliofanywa na UHURU umebaini baadhi ya dawa zinazotolewa hospitali kutibu wagonjwa wa saratani, watu wenye maumivu makali, waliofanyiwa upasuaji na wagonjwa wa mafua, zinatumika kwa wingi kama mbadala wa heroin na cocaine.

Baadhi ya dawa zinazotumiwa hivi sasa na kundi hilo la vijana ni, Pethidine-hameln, Morphine, Oxycodine, Valium, Tramadol, Metaphetamine, Litalin na dawa zingine za maumivu makali ambazo hujulikana kama kundi la Opiod.

Dawa hizo zimeanza kushamiri katika vijiwe mbalimbali hasa kwa wapiga debe, ambapo huzitumia kupata ‘stimu’ ikiwa ni mbadala wa heroin na cocaine.

Kauli ya daktari bingwa

Akizungumza na UHURU, Daktari Bingwa wa Afya ya Akili wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Said Kuganda, amesema kumeibuka tabia kwa baadhi ya watu ambao siyo wagonjwa, wanatumia dawa hizo kwa manufaa binafsi.

Dk. Kuganga alionya matumizi makubwa yasiyofaa ya dawa hizo yana madhara makubwa kwa binadamu na husababisha kifo kwa mtumiaji.

Amesema mtu anayetumia dawa hizo bila kufuata mwongozo wa daktari husababisha uraibu, humletea madhara katika mfumo wa upumuaji, husababisha kifafa, huathiri ubongo na hata kifo.

“Kwa mfano dawa inaelekeza itumike kwa mils 50, lakini mtu anatumia mils 100 au badala ya kumeza kidonge kimoja, mtu anameza 10 kwa mara moja.

Pia, amedokeza madhara mengine ya dawa hizo ni utegemezi na kumwathiri mtu kisaikolojia kwa kujiona hawezi kufanya jambo lolote bila kutumia dawa hizo.

Dk. Kuganda amesema wagonjwa wengi wanaofika hospitalini hapo hivi sasa ni wale walioathirika na matumizi ya dawa hizo ukilinganisha na wanaotumia heroin na cocaine.

Daktari huyo amesema idadi kubwa ya wagonjwa walioathirika, wanakwenda wakiwa na hali mbaya baada ya kutumia dawa hizo muda mrefu.

“Wagonjwa wengi waliofika ni wale waliotumia Tramadol na kawaida dawa hiyo hutumika kutibu maumivu,”alifafanua Dk. Kuganda.

Dk. Kuganda alisema Tramadol hupewa mgonjwa mwenye maumivu makali ya saratani, mifupa na wanaofanyiwa upasuaji, ambapo hupatiwa kwa matumizi ya muda mfupi kati ya siku tano hadi saba.

Amefafanua mgonjwa aliyepafanyiwa upasuaji au mwenye maumivu ya saratani, akipatiwa dawa hizo hupona haraka maumivu.

“Ukipewa dawa hizo unajisikia vizuri, mgonjwa anakuwa katika hali ya kustarehe, sasa ile stimu baadhi ya watu wanaitumia vibaya kama dawa za kulevya,”alisema.

TMDA yafunguka

Mkurugenzi wa Udhibiti wa Dawa kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Dk. Yona Mwalwisi, amesema dawatiba hizo huingizwa na kusambazwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ambapo hospitali au zahanati zinazohitaji dawa hizo hupewa kwa kibali cha MSD.

Mkurugenzi huyo amesema TMDA inaendelea kudhibiti uuzwaji holela, ambapo imeweka watu katika vituo vya forodha, viwanja vya ndege, kukagua kuhakikisha dawa hizo haziingizwi nchini kiholela au kuchepushwa.

Daktari huyo amesema dawa hizo hutolewa kwa cheti cha daktari na hairuhusiwi kuuzwa kiholela na duka linalouza linatakiwa kutunza taarifa na nakala zinazoonesha dawa hizo ziliuzwa kwa cheti cha daktari.

“Wakaguzi wakija waone uwiano wa dawa na vyeti vilivyopo na zilingane na dawa zilizopo kama ni dawa 10 ziliuzwa na vyeti viwe 10 wakienda kinyume Baraza la Famasia huchukua hatua,”amesema.

Vilevile, Dk. Mwalwisi amesema utaratibu wa kuuza dawa hizo zinaelekeza kuwe na mazingira wezeshi ya kutunzwa.

Pia, Dk. Mwalwisi amesema dawa hizo zina rejesta maalumu na mfamasia anatakiwa kuingiza kiasi kilichotoka na kuingia.

Vilevile, amefafanua ni lazima chupa na mabaki ya dawa hizo viteketezwe kwa kushuhudiwa na wataalamu mbalimbali.

Mkurugenzi huyo alikiri dawa hizo zisipotumika kwa kufuata mwongozo wa wataalamu, zina madhara makubwa licha ya kwamba zinauzwa kwa gharama ndogo.

Takwimu

Akizungumzia takwimu, Dk. Mwalwisi, amesema ndani ya mwaka huu wamekamata Pethidine vichupa 1,045 vyenye ujazo wa milligrams 100 kwa kila mililita mbili.

Pia, amesema walikamata vichupa 440 vya dawa hiyo yenye ujazo wa miligramu 50 kwa kila mililita.

Amesema kuanzia Julai mwaka jana hadi sasa, wamekamata dawa aina ya Morphine vichupa 3,010.

Dk. Mwalwisi ameongeza kipindi cha mwaka 2023, walikamata Pethidine vichupa 3,080 na mwaka 2021 walikamata vichupa vya dawa hizo 2,160.

Kwamujibu wa Dk. Mwalwisi  dawa hizo zilikamatwa katika maeneo ya mipakani ukiwemo mpaka wa Lusumo.

DCEA

Kwa upande wake Kamishina wa Kinga, Tiba na Huduma za Utengamao kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dk. Peter Mfisi, amesema matumizi ya dawatiba hizo ambazo zina asili ya kulevya, zimeanza kutumika vibaya baada ya dawa heroin na cocaine kudhibitiwa.

Amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikishirikiana na TMDA kufanya operesheni mbalimbali za kuhakikisha dawa hizo zinauzwa kwa cheti cha daktari.

“Dawa kama heroin upatikanaji wake umepungua kwa kiasi kikubwa katika jamii, sasa matokeo yake watu waliokuwa wakitumia dawa hizi wamejiingiza katika dawa tiba zenye asili ya kulevya kupunguza arosto wanayoipata,”alisema.

Pia, amesema katika uchunguzi wao walibaini siyo watu wote wanaotumia dawatiba zenye asili ya kulevya, kwamba awali waliwahi kutumia dawa za kulevya kama heroin.

Dk. Mfisi amesema utafiti unaonesha watu wanaotumia dawa hizo bila kufuata ushauri wa daktari wana nafasi kubwa ya kupata madhara katika figo na ini.

Ametaja madhara mengine ni kusababisha utegemezi, kupunguza uwezo wa kufikiri na matatizo mengine ya afya ya akili.

Dk. Mfisi amesema DCEA inaendelea na jitihada za kutoa elimu za madhara ya matumizi ya dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali ikiwemo shuleni.

Mfamasia Mkuu wa Serikali

Mfamasia Mkuu wa Serikali Dk. Daud Msasi, alisema baada ya kuanza huduma ya Bima ya Afya kwa Wote, serikali imejipanga kusajili maduka ya dawa yote katika mfumo wa E- Prescription (kutoa dawa kwa maagizo ya daktari).

Alisema kuanza mfumo huo kutasaidia wauzaji wa maduka ya dawa kuona dawa ambazo mgonjwa ameandikiwa na daktari.

Pia, alisema miongoni mwa dawatiba zenye asili ya kulevya inayopatikana kwa kibali cha MSD ni Ketamain.

Alisema dawa aina ya Tramadol inatolewa kwa cheti cha daktari na serikali inaendelea kudhibiti kwa kuzingatia sheria na kanuni.

Nini Kifanyike

Dk. Mfisi ameshauri kuendelea kudhibiti uchepushwaji wa dawa hizo na jamii iendelee kupewa elimu ya madhara ya matumizi mabaya ya dawa hizo.

Daktari huyo ameshauri wauzaji wa maduka ya dawa wahakikishe wakishatoa huduma mteja ahakikishe anatia saini katika cheti cha daktari ili kudhibiti ununuaji holela kwa matumizi yasiyofaa.

Previous Post

MAFWELE NA WENZAKE 42 KUTOA USHAHIDI KESI YA KUGHUSHIVIBALI VYA KUMILIKI SILAHA

Next Post

MELI KUBWA NNE ZA MIZIGO KUIFUNGUA TANZANIA KIUCHUMI

Next Post
MELI KUBWA NNE ZA MIZIGO KUIFUNGUA TANZANIA KIUCHUMI

MELI KUBWA NNE ZA MIZIGO KUIFUNGUA TANZANIA KIUCHUMI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KIKWETE AWATOLEA UVIVU WAZUSHI, ASEMA UTEUZI WA DK. SAMIA ULIFUATA KATIBA YA CCM

KIKWETE AWATOLEA UVIVU WAZUSHI, ASEMA UTEUZI WA DK. SAMIA ULIFUATA KATIBA YA CCM

8 months ago
MIILI YA WALIOFARIKI AJALI YA HELKOPTA YATAMBULIWA

MIILI YA WALIOFARIKI AJALI YA HELKOPTA YATAMBULIWA

4 months ago

Popular News

  • YANGA MBELE KWA MBELE

    YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?