• ePaper
Saturday, May 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAFWELE NA WENZAKE 42 KUTOA USHAHIDI KESI YA KUGHUSHIVIBALI VYA KUMILIKI SILAHA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 16, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MAFWELE NA WENZAKE 42 KUTOA USHAHIDI KESI YA KUGHUSHIVIBALI VYA KUMILIKI SILAHA
0
SHARES
31
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KAMISHNA  Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ( SACP), Faustine Mafwele na wenzake 42, wanatarajiwa kutoa ushahidi,  katika kesi ya kughushi vibali vya kumiliki silaha, inayowakabili watu tisa wakiwemo maofisa wa polisi.

Pia,  kutakuwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo maelezo ya onyo ya washitakiwa, vibali vya kumiliki silaha, fomu za maombi ya kumiliki silaha na hati ya ukamataji mali.

Wakili wa serikali, Cathibert Mbiling’i, amedai  hayo  leo Machi 16, 2026, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Geofrey Mhini, shauri lilipopelekwa kuwasomea washitakiwa hoja za awali.

Katika  kesi hiyo, washitakiwa  ni Fedrick Malekela, Kalemwa Kaunga,  John Kaposwe, Edger Mlogo, Robert Titus  na  Julieth Moshi, ambao ni  maofisa wa polisi.

Wengine  ambao siyo maofisa wa polisi  ni mkulima Damson Mnyilenga, mfanyabiashara Simon Aloyce na Venrand Liberio ambao wote wanakabiliwa na kesi hiyo.

Baada ya washitakiwa kusomewa hoja za awali, walikiri taarifa zao binafsi, ambazo ni majina yao, umri, makazi na kazi yao, huku wakikana kutenda kosa.

Hakimu Mhini, baada ya kusikiliza hoja hizo, amesema kesi hiyo itasikilizwa siku tatu mfululizo kuanzia Aprili 8 hadi 10, mwaka huu na washitakiwa wapo nje kwa dhamana.

Katika kesi hiyo ,washitakiwa hao wanadaiwa kughushi vibali 16 vya kumiliki silaha vyenye majina ya watu mbalimbali.

Ilidaiwa kuwa, vibali hivyo vilikuwa na majina ya Ahmed Abdallah, Ahmed Sandrudin, Omary Abdallah, Robart Koka na Arafathi Ally.

Wengine ni Mohamed Salim, Suleman Mbewa, Mickdadi Chakindo, Irfan Nafiri, Gulamabas Najafi, Ismail Ismail, Salim Salim, Marwaan Habretsh, Maurice Kutiwe na Said Mohamed.

Previous Post

MBARAWA AIPONGEZA TASAC KUSIMAMIA NA KUDHIBITI USAFIRI MAJINI KWA UFANISI

Next Post

BAADA YA HEROIN, COCAINE KUDHIBITIWA: ‘MATEJA’ WAGEUKIA DAWA ZA HOSPITALI

Next Post
BAADA YA HEROIN, COCAINE KUDHIBITIWA: ‘MATEJA’ WAGEUKIA DAWA ZA HOSPITALI

BAADA YA HEROIN, COCAINE KUDHIBITIWA: ‘MATEJA’ WAGEUKIA DAWA ZA HOSPITALI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI YAIPA TANO YANGA

SERIKALI YAIPA TANO YANGA

8 months ago
DCEA YAKAMATA SHEHENA YA MIRUNGI KUTOKA KENYA, YAKAMATA BOTI BAGAMOYO

DCEA YAKAMATA SHEHENA YA MIRUNGI KUTOKA KENYA, YAKAMATA BOTI BAGAMOYO

3 weeks ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?