• ePaper
Sunday, April 5, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA YAJIPANGA KUNUFAIKA NA GESI TRILIONI 57.54, WAWEKEZAJI WAALIKWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 22, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA YAJIPANGA KUNUFAIKA NA GESI TRILIONI 57.54, WAWEKEZAJI WAALIKWA
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

TANZANIA imeingia katika hatua mpya ya maendeleo ya sekta ya gesi asilia kufuatia kuthibitishwa kwa uwepo wa akiba kubwa inayokadiriwa kufikia futi trilioni 57.54, hatua inayotarajiwa kubadilisha mwelekeo wa uchumi wa Taifa.

Akizungumza katika mkutano wa Powering African Summit jijini Washington Dc Machi 21,2026, Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba amesema rasilimali hiyo kubwa inaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye fursa kubwa zaidi za uwekezaji katika nishati barani Afrika.

Amesema pamoja na mafanikio hayo, takribani asilimia 70 ya maeneo yenye uwezekano wa kuwa na mafuta na gesi bado hayajachunguzwa, jambo linalotoa nafasi kubwa kwa wawekezaji kushiriki katika shughuli za utafutaji na uchimbaji.

Salome amefafanua kuwa Serikali ipo katika hatua za maandalizi ya kuanzisha msimu mpya ya utoaji wa vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi ikiwa ni mkakati wa kuvutia wawekezaji wapya na kuongeza uzalishaji wa rasilimali hizo.

Aidha, ameongeza kuwa Tanzania sasa inaelekea kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya gesi ikiwemo mradi wa kuchakata Gesi kuwa kimiminika (LNG), unaotarajiwa kufungua masoko ya kimataifa na kuongeza pato la taifa.

Serikali inalenga kuhakikisha gesi asilia inatumika zaidi ndani ya nchi kwa ajili ya kuzalisha umeme, kuendesha viwanda, matumizi ya majumbani pamoja na matumizi ya usafiri ili kuongeza thamani ya rasilimali hiyo’ amesema

Aidha, uwekezaji unahitajika katika miundombinu muhimu ikiwemo mabomba ya kusafirisha gesi, vituo vya kujaza gesi na mifumo ya usambazaji ili kufanikisha matumizi mapana ya nishati hiyo safi hivyo ni fursa kwa wawekezaji kuja Tanzania na kuwekeza miradi hii ambayo si tu kwamba itanufaisha Taifa letu bali hata wawekezaji pia watanuika kuwa kama nchi tumeweka mazingira bora ya uwekezaji yenye uwazi na uhakika.

Amebainisha kuwa matumizi ya gesi asilia yatapunguza  gharama za uzalishaji viwandani na kusaidia kulinda mazingira kwa kupunguza utegemezi wa nishati chafu kama kuni na mkaa.

Hatua hizi zinatarajiwa kuiwezesha Tanzania kunufaika kikamilifu na utajiri wa gesi asilia, kuongeza ajira, na kuimarisha uchumi wa taifa katika kipindi kijacho.

Previous Post

MZEE MPILI:MIMI MZIMA SIJAFA

Next Post

SIMBA KUIUA TRA UTD

Next Post
SIMBA KUIUA TRA UTD

SIMBA KUIUA TRA UTD

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NMB YAPATA MAFANIKIO MAKUBWA, YAZINDUA MKAKATI WA MIAKA MITANO

NMB YAPATA MAFANIKIO MAKUBWA, YAZINDUA MKAKATI WA MIAKA MITANO

2 months ago
DK. NCHIMBI AMTAJA DK. SAMIA UJENZI BANDARI YA KWALA

DK. NCHIMBI AMTAJA DK. SAMIA UJENZI BANDARI YA KWALA

6 months ago

Popular News

  • CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

    CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MCHENGERWA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AELEZA FAIDA YA KULINDA TUNU YA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VIONGOZI WA DINI WAHUBIRI AMANI 

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?