• ePaper
Friday, May 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 4, 2026
in Habari, Kitaifa
0
CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

UONGOZI wa Chama Cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA), umewataka Watanzania kudumisha amani ya nchi kwani ndiyo nguzo muhimu ya kukuza siasa, uchumi na michezo.

Kauli hiyo, imetolewa jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa CHAMUDATA, Angel Bushoke alipozungumza na UHURU kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuiunga mkono serikali.

“Unajua serikali yetu inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan  inafanya mambo mengi makubwa,  inapambana kwa nguvu zote kuhakikisha taifa linakuwa na amani, hivyo watanzania wanapaswa kuungana na kuwapuuza watu wenye kutaka vurugu,”alisema.

Angel alifafanua kuwa viongozi wa CHAMUDATA wana imani kubwa na i Tume Huru ya Uchunguzi ya Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu. uliofanyika Oktoba 29, mwaka jana.

 Rais Dk. Samia aliunda tume hiyo, Novemba 18, mwaka jana kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi ya mwaka 2023 (Sura ya 32) ambapo tume hiyo inaongozwa na Mwenyekiti, Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande Othman.

“Tuseme kweli nchi ikiwa haina amani hakuna jambo litakalo fanyika, hivyo wananchi tunapaswa kushikamana na kama zipo changamoto zitatuliwe kwa hoja na si fujo.

“Wito wangu kwa Watanzania ni vyema tukaendelea kudumisha amani ya nchi yetu maana Tanzania tunasifika kuwa wakarimu ndiyo maana kuna baadhi ya watu wanatoka nchi zao na kuja hapa kwetu kuwekeza,” alisema.

Makamu Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa siku zilizopita zipo baadhi ya timu ziliomba kuja kucheza michezo yao hapa nchini kutokana na nchi zao kukosa amani.

“Hakuna jambo zuri kuona nchi yetu mwakani inakuwa moja ya  nchi waandaji wa michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2027, hii yote imetokana na kuwepo utulivu na amani,”alisema.

Previous Post

MCHENGERWA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

Next Post

RAIS DK. SAMIA SULUHU MWANADEMOKRASIA WA KISIASA

Next Post
RAIS DK. SAMIA SULUHU MWANADEMOKRASIA WA KISIASA

RAIS DK. SAMIA SULUHU MWANADEMOKRASIA WA KISIASA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

HATMA YA MANGUNGU BAADA YA SIMBA, ATLETICO

HATMA YA MANGUNGU BAADA YA SIMBA, ATLETICO

3 months ago
MZEE MALECELA ASEMA  HAKUNA UTALII BILA AMANI

MZEE MALECELA ASEMA  HAKUNA UTALII BILA AMANI

4 weeks ago

Popular News

  • YANGA MBELE KWA MBELE

    YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?