• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

VIONGOZI WA DINI WAHUBIRI AMANI 

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 4, 2026
in Habari, Kitaifa
0
VIONGOZI WA DINI WAHUBIRI AMANI 
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na WAANDISHI WETUI

VIONGOZI wa madhehebu mbalimbali wamekemea vitendo vinavyohatarisha amani, huku wakisisitiza kuwa haki ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa na kuonya upotoshaji wenye lengo la kuvuruga utulivu uliopo.

Pia, wataka kukomeshwa ukatili dhidi ya watoto ukiwemo unaohusu ukeketaji, utumikishwaji na kusisitiza umuhimu wa watoto kupata elimu bora.

Nasaha hizo zilitolewa katika ujumbe wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika makanisa mbalimbali nchini na maombi ya pamoja kuombea nchi na viongozi.

Akiongoza maombi maalumu kuombea taifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Makanisa Mkoa wa Arusha (UKAMA), yaliyofanyika katika viwanja vya Jimbo Kuu Katoliki Parokia ya Mtakatifu Teresa wa Moyo wa Yesu, jijini Arusha, Katibu Msaidizi wa UKAMA, Profesa Julius Laizer, alisema wanawaombea viongozi ili Mungu azidi kuwapa hekima, maarifa, upendo na mshikamano waongoze taifa kwa haki na uadilifu.

“UKAMA tumejumuika hapa kwa ibada ya Ijumaa Kuu ambayo inatukumbusha mateso aliyoyapitia Yesu Kristo pale msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na kuwaombea viongozi wa taifa letu wakiongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Dk. Emmanuel Nchimbi, Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, baraza la mawaziri, vyombo vya ulinzi na usalama na serikali nzima kuanzia ngazi ya mkoa hadi vitongoji,” alisema. 

Pia, alisema wanaombea ustawi wa taifa katika upangaji wa mipango ya maendeleo, utekelezaji na uwajibikaji wa sekta mbalimbali zikiwemo za uchumi, huduma za jamii, miundombinu, usalama, siasa, elimu na afya. 

Maombi hayo pia yalijikita kuombea ustahimilivu wa kuonya kukemea kufundisha dhidi ya mambo yanayopotosha maadili ya taifa na uzalendo. 

“Tunapingana na dhana zote potofu za kukwamisha ustawi wa Taifa, Tunaangusha ngome zote za adui kutoka ndani na nje ya nchi zinazopingana na ustawi wa taifa letu.

“Tunawaombea viongozi wetu Mungu awasaidie kukuza nia thabiti ya kutumia rasilimali watu na rasimali za asili zilizopo nchini kwa lengo la kuinua uchumi wa taifa na mwananchi mmoja moja ili kuhakikisha maendeleo ya nchi katika nyanja zote yanaimarika,” alisema. 

Mshamu Askofu Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac Aman, alisisitiza kuwa upendo ndiyo msingi wa ukombozi wa binadamu, hivyo aliwahimiza wananchi kuthamini uhuru wa nchi na kulinda maisha yao kwa kuzingatia maadili mema.

Awali akizungumza katika ibada hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amosi Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, aliwashukuru viongozi wa UKAMA kwa kuombea taifa na kushirikiana na viongozi wa serikali katika mambo balimbali.

“Serikali ni kiungo kati ya viongozi wa dini na wananchi. Tunawashukuru kwa kujumuisha madhehebu yote ya dini zote hali inayoimarisha mshikamano wa kitaifa,”

Kwa mujibu wa Mkunde hakuna sababu ya uhasama kati ya serikali na viongozi wa dini, kwa kuwa shughuli zao zinaungwa mkono na serikali na zina mchango mkubwa katika ustawi wa jamii.

Mkude amewahakikishia waumini na wananchi wote wa mkoa na wilaya ya Arusha kuwa ulinzi utaimarishwa kikamilifu katika kipindi chote cha sikukuu ya Pasaka.

UJUMBE WA KKKT

Kwa upande wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), liliwataka waumini wake kusimamia haki wakitafakari kifo cha Yesu Kristo huku likitoa msimamo wa kupinga adhabu ya kifo.

Askofu Msaidizi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, (DMP) Chediel Lwiza, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waumini katika misa ya Ijumaa Kuu, iliyofanyika katika Kanisa la Azania Front, jijini Dar es Salaam.

Askofu huyo alisema wanapinga adhabu hiyo iwe kwa kunyongwa au kwa njia yoyote, huku akitoa sababu nne ya kupinga kwao.

“Mpendwa Yesu Kristo alikufa msalabani kifo cha aibu, lakini hawa wawili Yosefu wa Matayo na Nikodemas mwanafunzi wa Yesu kuna mambo wanatukumbusha.

“Kwanza walitumia nafasi zao vizuri, hawakuogopa, pili wanatufundisha hawakukubaliana na kupinga kifo cha msalabani, kwa sisi taifa letu la Tanzania bado Kanisa halikubali na linapinga adhabu ya kifo,” alisema.

Akitaja sababu za kupinga adhahi hiyo, mchungaji huyo alisema kwanza, uwezekano wa kuwepo kwa ushahidi wa uongo.

“Kama ilivyokuwa kwa Yesu Kristo, kutokana na ushahidi wa uongo, Yesu akafa, isingekuwa Mungu mwenye uwezo wa kumfufua nini kingetokea,” alisema.

Alisema ikiwa adhabu ya kifo imetolewa kwa mtu yeyote na ikawa imetolewa kimakosa na mtu akahukumiwa kunyongwa na akauawa kwa namna yoyote, hapatakuwa na namna ya kumfufua hadi siku ya ufufuo.

Sababu ya pili alisema hakuna ushahidi kwamba adhabu hiyo inapunguza makosa ndani ya nchi, huku sababu ya tatu akisema adhabu hiyo ni kinyume na neno la Mungu.

Aliendelea kutaja sababu ya nne ya kanisa hilo kupinga adhabu ya kifo ni kwamba, kifo chochote cha mazingira ya adhabu kinajenga chuki, hasira na kisasi.

MALEZI BORA

Kutoka mkoani Dodoma, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Beatus Kinyaiya, aliwataka wazazi kuwa na utaratibu wa kuwaonya watoto wao wanapokosea na kuwajenga kimaadili.

Akizungumza wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Inyasi wa Loyola, Miyuji Dodoma, Askofu Kinyaiya, alisema malezi bora huanzia katika familia.

Alibainisha kwamba kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wazazi kushindwa kuwakemea watoto wao wanapofanya makosa, jambo ambalo linaweza kuchangia kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii.

“Kuna wazazi hawawakemei watoto wanapokosea, mkiendelea kuwaacha wataharibika. Wazazi wakemeeni watoto wenu wajue wanapokosea, siyo kuwaacha,” alisema.

Pia, aliwataka wazazi kuwa karibu na watoto wao kufuatilia mienendo yao na kuwasaidia kukua katika misingi sahihi ya maadili na heshima.

Alisisitiza kuwa malezi yenye nidhamu na maonyo ya wakati sahihi yatawasaidia watoto kuwa raia wema na wenye mchango chanya kwa jamii.

KUTOKA TABORA

Waumini wa madhehebu ya Kikristo na jamii kwa ujumla wametakiwa kuwa na hofu ya Mungu mioyoni mwao na kufanya ibada zenye mguso wa nguvu za Mungu, waishi maisha ya ushindi na kumpendeza Mungu.

Askofu Julius Tibuhinda wa Kanisa la Tanzania Assemblies (TAG), Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, alieleza hayo katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la TAG Kitete, mjini Tabora.

Alisisitiza umuhimu wa waumini wa makanisa ya kipentekoste na madhehebu mengine kufanya ibada zenye mguso wa nguvu za Mungu na maombi ili roho wa Mungu atawale maisha yao na kuwa na hofu mioyoni.

Alisisitiza kuwa ibada na maombi ni mapacha na kwamba hiyo ndiyo silaha ya ushindi kwa muumini, hivyo kila mkristo anayemwamini Yesu Kristo ni lazima ashiriki ibada na maombi.

UPENDO

Katika hatua nyingine, waumini wa dini ya Kikristo, wamehimizwa kuendeleza upendo na kutambua umuhimu wa kusimamia ukweli, amani, mshikamano na kushirikiana na jamii.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Mhashamu Stephano Musomba, alieleza hayo katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la Katoliki Jimbo la Bagamoyo, Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kermeli, Bunju Dar es Salaam.

Alisema upendo na mshikamano ni msingi wa kuunda jamii imara, yenye mshikamano thabiti na inayochangia maendeleo endelevu kwa wote.

“Tupendane kama Yesu Kristo alivyotupenda, tunapaswa kujua kuwa kuishi kwa amani na kuheshimiana kunasaidia kupunguza migongano, kuimarisha mahusiano ya kijamii na kukuza ushirikiano katika familia, makanisa na jamii kwa ujumla.

“Niwasihi kushirikiana kwa kina katika shughuli za kijamii na kusaidia wanyonge kuhakikisha kila mmoja anapata haki na fursa sawa za maendeleo,”alisema.

Aidha, jamii inapaswa kuendelea kusimamia ukweli na kukubali kwa kila hatua kwa kuwa ukweli husaidia kumweka huru mtu.

Pia, aliwasihi kuendelea kulinda amani kwa kuwa ni msingi wa maisha ya kijamii na maendeleo kwa ujumla.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Henry Mchamungu, amewataka waumini wa dini ya Kikristo kutumia Ijumaa Kuu kuonyesha upendo badala ya chuki.

Akizungumza katika Ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa Kuu la Mt. Yosefu Jimbo Kuu la Dar es Salaam, jana,  Askofu Mchamungu, alisema kupitia mateso ya Yesu Kristo waumini wanapaswa  kupendana na siyo kuchukiana.

Alisema jamii inapaswa kubadilika na kutumia siku ya Ijumaa Kuu kupendana na kuendelea kumuenzi Yesu Kristo ndani ya mioyo yao.

“Tumesikia simulizi ya mateso ya kristo, niwaombe kutumia siku hii maalumu kupendana na tusikubali kuchukiana sisi wenyewe,” alisema.

Walioandika ni Allan Kitwe (Tabora), Lilian Joel (Arusha), Rehema Mohamed, Hawa Ngadala, Ziana Bakari (Dar).

Previous Post

BILIONI 400/- KUJENGA ARENA YA KISASA

Next Post

UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

Next Post
UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. BASHIRU AELEZEA UJASIRI WA DK. SAMIA

DK. BASHIRU AELEZEA UJASIRI WA DK. SAMIA

7 months ago
SIMBA MZUKA UMEPANDA

SIMBA MZUKA UMEPANDA

1 month ago

Popular News

  • KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

    KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MUYUNGI ASISITIZA WANANCHI KUFANYA BIASHARA YA KABONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KAMATI YA UTALII, BIASHARA NA KILIMO BARAZA LA WAWAKILISHI YADHAMIRIA MAMLAKA YA VIPIMO ZANZIBAR IFIKIE VIWANGO VYA WMA BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • LAZARUS CHAKWERA AMALIZA ZIARA YA SIKIU 9 NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?