• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

USALITI WA UHUSIANO CHANZO CHA UKATILI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 24, 2026
in Habari, Kitaifa, Makala, RIPOTI MAALUMU
0
USALITI WA UHUSIANO CHANZO CHA UKATILI
0
SHARES
24
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na EMMANUEL MOHAMED

WADAU wa masuala ya saikolojia na haki za binadamu wametaja sababu zinazochangia matukio ya ukatilii nchini, ikiwemo afya ya akili na usaliti katika uhusiano.

Sababu zingine ambazo zinachangia matukio hayo ya kikatili ni msongo wa mawazo na historia za familia.

Akizungumza na UHURU, Mwenyekiti wa Kamati Endelevu ya Taaluma kutoka Chama Cha Wanasaikolojia Tanzania (TAPA), Jesusa Malewo, alisema ukatili kwa lugha nyepesi ni mtu kuelezea maumivu kwa njia isiyofaa.

“Maumivu hayo yanatokana na hali mbalimbali za kimaisha, kwa mfano, historia ya familia inaweza kumsababishia mtu kuwa mkatili. Mtu amekuwa akiona wazazi wake wakipigana, ni rahisi kufanya ukatili kwa mtu mwingine kutokana na kuwa amekuwa kwa kuviona vitendo vya kikatili,

“Kwa hiyo hali hii imekaa katika akili yake, hivyo ni rahisi kumfanyia mtu mwingine ukatili, kikubwa ni yale maumivu ambayo anayapitia wakati huo,”amesema.

Malewo alitaja sababu nyingine ni changamoto za kimaisha, ambazo hufanya baadhi ya watu kuwa na msongo wa mawazo.

“Kwa hiyo, kuwa na msongo wa mawazo inaweza kuwa ni kisababishi cha mtu kufanya ukatilii kutokana na kuwa kuna mambo mengi yanamsonga, kuna mambo yanampa wasiwasi, kuna mambo mengi hayajakaa vizuri kwenye maisha yake, kwa hiyo hata namna ya kuyatatua bado hajui atumie stadi zipi,”amesema.

Alisema kwa upande mwingine, sababu nyingine ya kuongezeka kwa matukio hayo ni usaliti katika uhusiano ambao wahusika wanashindwa kuelezeana ukweli wa mambo ambayo hayajitoshelezi katika uhusiano wao.

“Kwa mfano, kwa hawa waliopo katika uhusiano unakuta mtu alitendwa, yale maumivu ya hisia anahama nayo kwenda kwa mtu mwingine ambaye hana hatia,”amesema Malewo.     

NINI KIFANYIKE

Mbali na hilo, alitaja jambo la kwanza ambalo linapaswa kufanywa kukabiliana na tatizo hilo; ni watu kuyatambua maumivu yao ya kisaikolojia.

“Siku ya mwisho watu waelewe na waone kawaida kutokuwa sawa lakini pia, watafute msaada wakati wanapojiona hawawezi kusimama, kwa hiyo wanahitaji msaada kutoka nje,”alisema.

Alisema ufumbuzi mwingine ni kujifunza stadi mbalimbali za maisha, ukiwemo ujuzi wa kutatua matatizo mbalimbali.

“Hatua ya kwanza kabisa ni kutambua tatizo, kwa hiyo kuna stadi mbalimbali ambazo mtu anaweza kujifunza kutokana na nini anachokihitaji,”alisema.

Alisema jambo lingine ni mtu kujijenga katika ukomavu wa kihisia ambao utamsaidia kutambua hisia zake, za mtu mwingine na pia kuzimudu.

DK. HENGA

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Anna Henga, alisema miongoni mwa mambo ambayo yanachangia ni kuwepo mfumo wa maisha ambao unawachanganya watu wengi.

Mkurugenzi huyo alisema, sababu nyingine ni watu kutofahamu haki za wengine kutokana na kuhisi wanawamiliki wenzao.

“Unakuta mwanaume anahisi huyu mke wangu ninammiliki, kama ni mtoto wangu ninammiliki, kwa hiyo anahisi anaweza kumfanyia chochote kwa sababu yeye hafahamu kuwa kila mtu ana haki yake,”alisema Henga.

Dk. Henga alisema kuna haja ya kuwaelimisha watu masuala ya haki za binadamu, kwani yatawasaidia  kuheshimu haki zao bila kuvunja za wengine.

“Ninachoona ni kuwa watu pia wasikubali haki zao kuvunjwa, ukiona watu wanaonewa watu wakaripoti katika kituo cha polisi, itasaidia kupunguza matukio hayo,”alisema.     

TAKWIMU ZA NBS

Kwa mujibu wa Ripoti ya Takwimu za Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania, ya Mwaka 2024 kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ukatili umeongezeka katika jamii huku Mkoa wa Dar es Saalam ukiongoza.

Ripoti hiyo inaonyesha idadi kubwa ya waathirika waliripotiwa katika Mkoa wa Dar es Saalam, ambao  katika mwaka 2023 walikuwa 10,391 sawa na asilimia 27.7 ya waathirika wote, ukifuatiwa na Arusha wenye waathirika 4, 565 sawa na asilimia 12.2.

Previous Post

MAHITAJI YA UMEME YAONGEZEKA KWA WASTANI WA 10-15% KILA MWAKA

Next Post

WADAU WAUNGA MKONO MSISITIZO WA RAIS DK. SAMIA KUHUSU MAADILI

Next Post
WADAU WAUNGA MKONO MSISITIZO WA RAIS DK. SAMIA KUHUSU MAADILI

WADAU WAUNGA MKONO MSISITIZO WA RAIS DK. SAMIA KUHUSU MAADILI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

CHOBWEDO ATIKISA

CHOBWEDO ATIKISA

5 days ago
SARE ZA SHULE ZISIWE KIKWAZO – MARC

SARE ZA SHULE ZISIWE KIKWAZO – MARC

3 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?