• ePaper
Sunday, April 5, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

RUFANI YA SENEGAL KUSIKILIZWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 27, 2026
in Burudani, Kimataifa, Michezo
0
RUFANI YA SENEGAL KUSIKILIZWA
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

DAKAR, Senegal

MAHAKAMA ya Usuluhishi wa Kesi Michezoni (Cas), imesema itatolea uamuzi rufaa ya timu ya taifa ya Senegal haraka iwezekanavyo baada ya miamba hiyo kupokwa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Senegal iliondolewa hadhi ya ubingwa wa AFCON 2025 na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya kuvunja kanuni za mashindano kufuatia kutoka uwanjani wakati wa fainali dhidi ya Morocco.

Katika mchezo huo, Senegal ilitoka uwanjani ikigomea penalti iliyopewa Morocco dakika za mwisho kipindi cha pili kabla ya kurejea tena uwanjani na mkwaju huo ulikoswa na Brahim Diaz na mechi kwenda katika dakika 30 za nyongeza.

Katika dakika 30 za nyongeza, Senegal ilipata bao kupitia kwa Pape Gueye ambao lilidumu hadi mpira ulipomalizika (1-0) na Simba hao wa Teranga kutwaa taji hilo.

Hata hivyo, hivi karibuni CAF iliiondolea timu hiyo hadhi ya ubingwa na kuipa Morocco ushindi wa mabao 3-0 hatua ambayo imeifanya Senegal kukata rufaa Cas kupinga uamuzi huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Cas, Matthieu Reeb alisema: “Tunaelewa kwamba timu na mashabiki wanataka kujua uamuzi wa mwisho, na tutahakikisha kwamba taratibu za usuluhishi zinafanyika haraka iwezekanavyo, wakati tukiheshima haki za pande zote katika usikilizwaji wa kiungwana,”.

Hata hivyop, taarifa hiyo haijaeleza kwamba uamuzi huo utachukua muda gani hadi kukamilika.

(BBC)

Previous Post

MRADI WA BILIONI 18.9/- BUKOBA WAMPA SIFA RAIS DK. SAMIA

Next Post

LUKUVI KUAGWA MIKOA MITATU

Next Post
LUKUVI KUAGWA MIKOA MITATU

LUKUVI KUAGWA MIKOA MITATU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TAKWIMU ZAMBEBA MNIGERIA ALIYEKANDWA NA MWAKINYO

TAKWIMU ZAMBEBA MNIGERIA ALIYEKANDWA NA MWAKINYO

3 months ago
ONDOENI HOFU

ONDOENI HOFU

4 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA SULUHU MWANADEMOKRASIA WA KISIASA

    RAIS DK. SAMIA SULUHU MWANADEMOKRASIA WA KISIASA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MCHENGERWA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AELEZA FAIDA YA KULINDA TUNU YA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?