• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

DK. MWIGULU MGENI RASMI MTOKO WA CHRISTINA SHUSHO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 31, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa
0
DK. MWIGULU MGENI RASMI MTOKO WA CHRISTINA SHUSHO
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la mtoko na Christina Shusho litakalofanyika wakati wa Sikukuu ya Pasaka.

Tamasha hilo, limepangwa kufanyika  katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam, msanii wa muziki wa injili, Christian Shusho alisema tamasha hilo halitakuwa na kiingilio.

“Tamasha hili, kutakuwa na waimbaji mbalimbali kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi kwa ajili kutumbuiza siku hiyo,” amesema.

Alifafanua kuwa tamasha hilo litashirikisha wasanii hao ili kutumbuiza na kuabudu Mungu siku ya sikukuu hiyo.

“Wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi watakuwepo katika tamasha hilo akiwemo Rose Muhando, Joel Lwaga, Bella Kombo, Paul Clement na wengine wengi ambao wanafanya vizuri katika muziki wa injili,” alisema.

Msanii huyo alitoa wito kwa watu mbalimbali kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha hilo kwenda kushuhudia burudani nzuri ya muziki na kuabudu Mungu kwa pamoja ndani ya Sikukuu ya Pasaka.

Previous Post

DIARRA MTEGONI TUZO KIPA BORA

Next Post

CAG APENDEKEZA WIZARA MICHEZO KUIMARISHA USIMAMIZI WA UNUNUZI

Next Post
CAG APENDEKEZA WIZARA MICHEZO KUIMARISHA USIMAMIZI WA UNUNUZI

CAG APENDEKEZA WIZARA MICHEZO KUIMARISHA USIMAMIZI WA UNUNUZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

2 months ago
SERIKALI YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NISHATI ZA DOLA BIL. 12.9

SERIKALI YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NISHATI ZA DOLA BIL. 12.9

2 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?