• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

AZAM FC,TRA UTD KAZI IPO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 29, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
AZAM FC,TRA UTD KAZI IPO
0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

TIMU za Azam FC na TRA United zinatarajiwa kuonesha kazi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex,Dar es Salaam.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa saa 3:00 usiku ambapo Azam watakuwa nyumbani kuwakaribisha TRA United.

Akizungumza Dar es Salaam, Kocha Msaidizi wa Azam, Addis Worku alisema  hawakuwa na  muda wa kutosha kujiandaa baada ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC), lakini wapo tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya TRA United.

“Wachezaji wamejipanga vizuri kuhakikisha wanafanya vizuri, wanatambua mchezo utakuwa mgumu kwa sababu TRA United wana timu nzuri,” alisema.

Kocha huyo alifafanua kuwa ana imani watafanya vizuri kutokana na uzoefu wa kikosi chake.

“Wachezaji wetu wana uzoefu wa uwanja wetu, hivyo tuna imani watafanya vizuri kwa sababu wapinzani mara nyingi wamekuwa wakijilinda,” alisema.

Mwakilishi wa wachezaji wa Azam FC, Nathaniel Chilambo alisema wanajua umuhimu wa mchezo wa leo na watapambana kuhakikisha wanapata pointi tatu katika mechi hiyo mbele ya TRA United.

“Wachezaji wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri ili kupata pointi tatu,tunawaomba mashabiki wa Azam waje kwa wingi kutupa hamasa,” alisema.

Kocha wa TRA United, Etienne Ndayiragije alisema kikosi kimesafiri salama kutoka mkoani Tabora na wapo sawa wakisubiri kupambana ili kupata matokeo mazuri.

“Tunategemea baraka za Mungu hivi sasa timu inabadilika na tunaendelea kuzoeana na vijana wanaendelea kuwa na nguvu ya kupambana,” alisema Ndayiragile.

Mchezaji wa TRA United, Omari Yusuf alisema Azam FC ni timu kubwa na wao ni wakubwa pia na wanatarajia mchezo mzuri leo.

“Tumejipanga na wachezaji wana morali ya kutosha kuhakikisha tunafanya vizuri na kupata matokeo katika mchezo wa leo,” alisema.

Previous Post

KOCHA SIMBA AIPANIA MASHUJAA

Next Post

NI SIKU 100 ZA MAFANIKIO YA UTOAJI TIBA BORA JKCI

Next Post
NI SIKU 100 ZA MAFANIKIO YA UTOAJI TIBA BORA JKCI

NI SIKU 100 ZA MAFANIKIO YA UTOAJI TIBA BORA JKCI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MSD YABAINISHA DHAMIRA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SEKTA YA AFYA BINAFSI

MSD YABAINISHA DHAMIRA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SEKTA YA AFYA BINAFSI

3 months ago
AELEZA CCM ITAKAVYO JENGA UCHUMI JUMUISHI

AELEZA CCM ITAKAVYO JENGA UCHUMI JUMUISHI

11 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?