• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

IGP MSTAAFU MANGU AWAASA WATANZANIA KUEPUKA VISHAWISHI VYA KUVUNJA AMANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 13, 2026
in Habari, Kitaifa
0
IGP MSTAAFU MANGU AWAASA WATANZANIA KUEPUKA VISHAWISHI VYA KUVUNJA AMANI
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

IRENE MWASOMOLA NA SIMON NYALOBI

MKUU wa Jeshi la Polisi mstaafu (IGP), Balozi Ernest Mangu, amewataka Watanzania kutokubali kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani na usalama, kwa lengo la kulinda uchumi wa nchi na kuwa na maendeleo endelevu.

Pia, ameeleza madhara yanayotokea pindi amani inapovunjika, ikiwemo kuporomoka uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa.

Akizungumza na UHURU hivi karibuni, Mangu alisema wananchi wana nafasi kubwa na muhimu ya kulinda na kutunza amani, ambayo inapovurugika mwathirika wa kwanza huwa ni mwananchi mwenyewe.

Kwa mujibu wa Mangu, amani ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa lolote duniani, kwa sababu inapokosekana wananchi wanashindwa kufanya shughuli za uzalishaji na kusababisha kudorora uchumi.

“Wananchi waache kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani, amani iendelee kutamalaki nchini fursa mbalimbali za maendeleo ziendelee kupatikana. Inapokosekana amani waathirika ni wananchi wenyewe.

“Nashauri Watanzania wapende kudumisha amani na usalama ndani ya nchi yao, kukosekana amani kunasababisha athari nyingi,” alieleza.

Pia, alitoa rai kwa Watanzania kuwa wazalendo wa kupenda nchi yao.

Alisema mtu anapokuwa mzalendo hawezi fanya uhalifu unaoleta athari kwa taifa na mwananchi mmoja mmoja.

Mangu aliwasisitiza wananchi kuendelea kupendana, huku akisema upendo ni silaha kuu ya kudhibiti vitendo vya uvunjifu wa amani na uhalifu mahali popote.

Akizungumzia madhara ya uvunjifu wa amani, IGP huyo mstaafu alibainisha kunapokosekana usalama na amani taifa linakosa mapato na serikali inashindwa kuongoza nchi kutokana na kusimama shughuli za kiuchumi.

Mangu alifafanua serikali ina wajibu wa kutoa huduma ambazo kimsingi zinategemea kodi zinazolipwa na wananchi, hivyo kutokuwepo amani na utulivu ni chanzo kikubwa cha kuleta madhara.

“Kunapokuwa na uvunjifu wa amani mwananchi anakosa fursa ya kukuza uchumi, atashindwa kufanya shughuli za kujiingizia kipato na kuleta athari za kiuchumi,”alisema.

MATARAJIO TUME YA JAJI CHANDE

Alisema ni matumani yake Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 29, mwaka jana, itatoa funzo kwa wananchi kuona walikosea wapi na watagundua madhara yaliyotokea kutokana na vurugu hizo.

“Baada ya tume kumaliza kazi yake watu wote watagundua na kujifunza madhara ambayo yametokea. Tume italeta fundisho zuri kwa wananchi wote tulikosea wapi tutajifunza,”alifafanua Mangu.

Alibainisha baada ya tume kumaliza kazi yake wananchi watajua ni wapi walitetereka na kusababisha uvunjifu wa amani.

WAMACHINGA WAFUNGUKA

Aidha, baadhi ya viongozi wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, wamesema suala la amani ni muhimu na halina mbadala wake na kusisitiza wana imani kubwa na matokeo yatakayotangazwa na tume iliyoundwa kuchunguza vurugu za Oktoba 29, mwaka jana.

Walisema amani ni tunu inayopaswa kutunzwa na kila mwananchi na wanaisubiri kwa hamu ripoti ya Tume ya Jaji Chande.

Mwenyekiti wa Machinga mkoani Dar es Salaam, Yusuph Namoto, alisema umoja huo unatambua umuhimu wa amani na ndiyo maana kabla ya uchaguzi mwaka jana, waliandaa kongamano la kulielimisha kundi hilo kutunza amani katika uchaguzi.

Namoto alisema kutokana na hilo, wanachama waliingia katika uchaguzi bila kushawishiwa kufanya vurugu.

Mwenyekiti huyo alisema baada ya kutokea vurugu Oktoba 29 na baadaye kuwepo tetesi za kuibuka fujo kama hizo Desemba 9, mwaka jana, waliwaeleza wanachama wao wakae nyumbani kuvipisha vyombo vya dola kuwadhibiti waliotishia kuleta vurugu mara nyingine.

“Kwa sababu kulikuwa na tetesi ya kufanyika vurugu nyingine Desemba 9, mwaka jana, tuliwaambia wanachama wetu wakae nyumbani, tuwaachie polisi wafanye kazi yao.

“Tulifanya hivyo kwa makusudi tulijua wanaweza wakafanya vurugu halafu wakadai machinga tumeshiriki kumbe siyo kweli,” alifafanua.

Kwa mujibu wa Namoto, miaka ya nyuma kundi lao lilikuwa likitumiwa na baadhi ya watu wenye nia ovu na kuhusishwa na kila vurugu zinazofanywa, hivyo hivi sasa hawatakubali hilo litokee.

Alisema wamekuwa mstari wa mbele kudumisha amani kwa kuwa ndiyo chachu ya kukua kibiashara baada ya serikali kuboresha mazingira ya biashara.

Kwa upande wake, Katibu Msaidizi wa Chama cha Machinga Kariakoo (KAWASSO), Thabiti Maloka, aliwahimiza wananchi kuitunza amani iliyopo na kuacha kushawishika kuivuruga.

Maloka alisema wananchi wanapaswa kuendelezaa uzalendo maradufu na kuilinda amani ya nchi kwa gharama yoyote.

“Amani ni kitu muhimu tujifunze yaliyotokea Oktoba 29, mwaka jana, kuna msemo wa Kiswahili usemao mtoto akililia wembe mpe ukimkata ndiyo atajua ubaya wake, sisi tulilia wembe tuliona madhara yake kwa siku chache,” alisema Maloka.

Alisema alishuhudia uvunjifu wa amani Oktoba 29 ulivyoathiri maisha ya watu vikiwemo vifo, maisha ya kijamii na kuzorotesha biashara.

Katibu huyo alisema kutokana na athari zilizoshuhudiwa na wananchi wengi, hakuna anayetaka vurugu za aina hiyo zitokee.

“Kwa hali ile iliyotokea, sidhani leo hii kama yuko hata mtu ukimpa shilingi 100,000, aingie mtaani atathubutu kufanya hivyo kwa kutambua madhara yake,” alisema,

Vilevile, Maloka aliipongeza serikali kuunda tume hiyo, kwa kuwa kufanya hivyo ni kuenzi misingi ya amani na utulivu na wanasubiri ripoti.

Aliwashauri wananchi kuwa na subira kipindi hiki ambacho tume imeongezewa siku 21 za kukamilisha kazi itakayokuwa na ufanisi kwa taifa.

Novemba 20, mwaka jana, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliizindua tume ya kuchunguza vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 na kuipa siku 90 za kufanya uchunguzi huo hadi Februari 20, mwaka huu.

Hata hivyo, hivi karibuni tume hiyo iliongezewa muda kuhakikisha inaandaa na kukamilisha majukumu iliyokabidhiwa kwa ufanisi zaidi.

WAJUMBE WA TUME

Wajumbe wa tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Chande, ni Stergomena Tax, Jaji Mkuu mstaafu, Profesa Ibrahim Juma, Balozi Ombeni Sefue, Said Mwema, Balozi Paul Meela, Balozi David Kapya, Balozi Radhia Msuya na Balozi George Madafa.

Previous Post

NANAUKA AWAPA HAMASA VIJANA

Next Post

ROSTAM ANUNUA SONGO SONGO

Next Post
ROSTAM ANUNUA SONGO SONGO

ROSTAM ANUNUA SONGO SONGO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KAPIGENI KURA, NCHI SHWARI – DK. SAMIA

KAPIGENI KURA, NCHI SHWARI – DK. SAMIA

6 months ago
TAIFA STARS KUTUA MOROCCO KWA KISHINDO

TAIFA STARS KUTUA MOROCCO KWA KISHINDO

4 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?