• ePaper
Thursday, September 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 14, 2026
in Habari, Kitaifa
0
UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU, DODOMA

KATIBU wa Bunge, Baraka Leonard, amesema mchakato wa uchaguzi wa wajumbe watatu watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) umeanza rasmi, huku zoezi hilo likitarajiwa kufanyika wakati wa Mkutano wa Tatu wa Bunge unaoendelea jijini Dodoma.

Amesema kupitia taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma cha Ofisi ya Bunge, nafasi hizo tatu zinahusisha wagombea wawili kutoka Tanzania Bara na mmoja kutoka kundi la wanawake, wote kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha uwakilishi wenye usawa na kuzingatia makundi maalum katika uongozi wa kikanda.

Aidha, amesema mchakato huo utafuata taratibu zote za kisheria na kidemokrasia, ikiwemo kutoa fursa sawa kwa wagombea wote wenye sifa kushiriki katika uchaguzi huo muhimu kwa taifa.

Amesema tangazo la nafasi hizo litachapishwa katika Gazeti la Serikali kwa mujibu wa sheria, ambapo wagombea watatakiwa kuwasilisha majina yao ndani ya muda uliopangwa ili kuhakikisha uwazi na uhalali wa mchakato mzima.

Kwa mujibu wa ratiba, amesema uteuzi wa wagombea utafanyika Aprili 30, 2026 kuanzia saa 4:00 asubuhi, huku uchaguzi ukipangwa kufanyika Mei 4, 2026 kuanzia saa 11:00 alfajiri, mara baada ya kipindi cha maswali bungeni.

Vilevile, amesema wagombea wote wanatakiwa kukidhi vigezo vilivyowekwa na chama husika pamoja na kuwa na sifa za uongozi, uzoefu na uwezo wa kuwakilisha maslahi ya Tanzania katika ngazi ya kikanda kupitia EALA.

Katika hatua nyingine, amesema wagombea watakaopitishwa na chama chao watalazimika kujaza fomu maalum za uteuzi kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza na kuziwasilisha kwa Katibu wa Bunge kwa ajili ya kuthibitishwa kabla ya kushiriki uchaguzi huo.

Previous Post

TUME ILIYOUNDWA NA RAIS DK. SAMIA ILIVYOBEBA MATUMAINI YA AMANI

Next Post

SERA USIMAMIZI MALI ZA UMMA, KICHOCHEO CHA UKUAJI UCHUMI

Next Post
SERA USIMAMIZI MALI ZA UMMA, KICHOCHEO CHA UKUAJI UCHUMI

SERA USIMAMIZI MALI ZA UMMA, KICHOCHEO CHA UKUAJI UCHUMI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA INAYO HIFAHI YA KUTOSHA YA MAFUTA

TANZANIA INAYO HIFAHI YA KUTOSHA YA MAFUTA

6 months ago
SAFARI KUMALIZA CHANGAMOTO UMEME IRINGA, DODOMA YAIVA

SAFARI KUMALIZA CHANGAMOTO UMEME IRINGA, DODOMA YAIVA

8 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?