• ePaper
Monday, April 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WANASIASA WATAJA FAIDA ZA MUUNGANO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 20, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WANASIASA WATAJA FAIDA ZA MUUNGANO
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na EMMANUEL MOHAMED

BAADHI ya wanasiasa nchini, wameeleza faida za miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika (Tanzania Bara) na Zanzibar.

Miongoni mwa faida ni zile za kiuchumi kwa wafanyabiashara na kuongeza wigo wa soko.

Faida nyingine ambazo zinapatikana kupitia Muungano huo ni fursa za watu wa pande zote mbili kumiliki ardhi na uhakika wa ulinzi kwa upande wa Zanzibar.

Akizungumza na UHURU, Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, alisema Muungano umewaimarisha Watanzania kiuchumi na kutumia fursa zilizopo.

“Muungano wetu umetoa fursa kwa wakazi kutoka pande zote mbili kuishi maeneo yote ya Jamhuri ya Muungano na tukumbuke kuwa, Zanzibar ardhi yake ni ndogo, hivyo wanatumia fursa hiyo kuja upande wa pili kuanzisha shughuli za kiuchumi,”alisema.

Alisema faida ya Muungano ni kwamba, Wzanzibari wanapata fursa ya kumiliki ardhi kwa shughuli za kilimo na ufugaji.

“Faida nyingine ni kutumia soko pana la kibiashara kwa Tanzania Bara, unajua idadi ya watu Tanzania Bara ni kubwa, hivi sasa wafanyabiashara wakichukua bidhaa huku na kuleta upande wa pili, wananufaika kibiashara.

“Leo ukimtazama Bakhresa, biashara yake imetanuka kutokana na Muungano, imempatia fursa ya kumiliki eneo kubwa la ardhi kwa upande wa Tanzania Bara na kuanzisha biashara nyingi,”alisema

Alisema mbali na Bakhresa, pia yupo mfanyabiashara anayeitwa Gulamali, ametumia fursa ya Muungano katika kujitanua ambayo amejikita katika shughuli za uzalishaji kupitia kilimo, ufugaji na nyingine.

“Leo hii kupitia Muungano, mtu akiona mambo magumu anakwenda upande wa pili kutafuta fursa za kiuchumi, Zanzibar hivi sasa ni kisiwa cha utalii, kuna hoteli zaidi ya 8,000, hivyo watu wanapata ajira, “alisema

JUMA ALLY KHATIB

Mwenyekiti wa ADA TADEA, Juma Ally Khatib, alisema suala la Muungano siyo tu wa kisiasa, bali ni daraja muhimu la kiuchumi.

Alisema kupitia Muungano, wafanyabiashara wa Zanzibar wanauza bidhaa zao kwa urahisi katika soko kubwa la Tanzania Bara bila vikwazo.

“Hivyo, wafanyabiashara wa Tanzania Bara wanapata fursa ya kuwekeza katika sekta za utalii, uvuvi na biashara visiwani Zanzibar,”alisema.

Pia, Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa, Muungano umewezesha uwekezaji wa pamoja katika bandari, usafiri wa baharini na sekta ya utalii, jambo linalochangia ukuaji wa uchumi wa pande zote.

“Muungano wetu ni hazina, thamani yake itaonekana zaidi pale tutakapowekeza katika ushirikiano wa kiuchumi na kuwajengea wananchi mazingira rafiki ya kufanya biashara,” alisema.

Muungano wa Tanganyika (Tanzania Bara) na Zanzibar, ulifanyika Aprili 26, 1964, ukiongozwa na waasisi Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume.

Previous Post

MWIGULU AKOMAA NA WAKANDARASI

Next Post

DAKTARI ATAJA DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU

Next Post
DAKTARI ATAJA DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU

DAKTARI ATAJA DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

BONDIA NASRA, VENE WATOA SOMO LA AMANI

BONDIA NASRA, VENE WATOA SOMO LA AMANI

1 week ago
TANZANIA YATAJWA KINARA AFRIKA MAPAMBANO USUGU WA VIMELEA

TANZANIA YATAJWA KINARA AFRIKA MAPAMBANO USUGU WA VIMELEA

5 months ago

Popular News

  • SIMBA KASI ILE ILE

    SIMBA KASI ILE ILE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DAKTARI ATAJA DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WANASIASA WATAJA FAIDA ZA MUUNGANO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AKOMAA NA WAKANDARASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AJIRA 45,000 ZANUKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?