• ePaper
Tuesday, July 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home AFYA

DAKTARI ATAJA DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 20, 2026
in AFYA, Habari, Kitaifa
0
DAKTARI ATAJA DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

DAKTARI Bingwa wa Maradhi ya Moyo wa Hospitali ya Shifaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Lulu Mageta, amesema vijana wengi hukumbwa na tatizo la shinikizo la damu kwa sababu hawana kawaida ya kupima afya zao mara kwa mara.

Dk. Lulu ametaja baadhi ya dalili za ugonjwa huo kuwa ni maumivu chini ya moyo, kuchoka kusikokuwa kwa kawaida na mapigo ya moyo kwenda haraka.

“Ukiona unatembea umbali mdogo tu unachoka sana, umbali ambao zamani ulikuwa unatembea bila shida, basi ujue umeanza kupata shinikizo la damu na ugonjwa huu hauji ghafla kama baadhi yetu tunavyodhani, unachukua muda mrefu ndiyo maana tunashauri kupima mara kwa mara,” alisema.

Amewataka vijana kupima afya zao mara kwa mara, kwa sababu idadi kubwa kwa sasa wanasumbuliwa na maradhi hayo.

Dk. Lului amesema zamani, ugonjwa huo, ulizoeleka kuwasumbua watu wenye umri mkubwa ambao walikuwa katika hatari ya kupata maradhi, lakini kwa sasa vijana wengi wenye miaka chini ya miaka 40, wanapata tatizo hilo.

Dk. Lulu, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumzia ongezeko la magonjwa ya moyo hasa kwa vijana walio chini ya miaka 40.

Alisema vijana wanatakiwa kuwa na utaratibu wa kupima afya ya moyo mara kwa mara, kujua afya zao badala ya kusubiri mpaka hali inapokuwa mbaya, ndiyo wafanye hivyo wanapofika hospitali.

“Zamani ilionekana kuwa maradhi ya shinikizo la damu, yanawashambulia watu wazima sana pekee, lakini kutokana na kubadilika kwa mtindo wa maisha, watu wengi hawafanyi mazoezi kwa hiyo, vijana wengi kwa sasa wanasumbuliwa na shida kama hiyo,” alisema Dk. Lulu.

Aliongeza: “Tusiendelee kuwa na mawazo yale yale ya zamani kwamba shinikizo la damu ni kwa wazee kwa sababu vijana wengi wanakufa ghafla kutokanana magonjwa haya, tubadili mtindo wa maisha ,tufanye mazoezi,” alisema

Aidha, alisema zamani haikuwa rahisi kumkuta kijana wa chini ya miaka 40 akisumbuliwa na maradhi ya moyo, miaka ya hivi karibuni, imekuwa kawaida kabisa kuwaona watu wa rika hilo wakisumbuliwa na moyo.

“Uzoefu wa hivi karibuni unaonesha dhahiri namna vijana wengi wanavyosumbuliwa na shinikizo la juu la damu na maradhi ya kisukari ambayo pia yanasababisha shinikizo la damu, “ alisema.

Alisema miongoni mwa sababu za ugonjwa wa shinikizo la damu ni pamoja na kuwa na uzito wa kupindukia na kukaa muda mrefu katika maeneo ya kazi bila kufanya mazoezi.

Previous Post

WANASIASA WATAJA FAIDA ZA MUUNGANO

Next Post

SIMBA KASI ILE ILE

Next Post
SIMBA KASI ILE ILE

SIMBA KASI ILE ILE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA TUNA RAIS JASIRI NA MCHAPAKAZI

TANZANIA TUNA RAIS JASIRI NA MCHAPAKAZI

4 months ago
TANZANIA YATIKISA KIMATAIFA

TANZANIA YATIKISA KIMATAIFA

5 months ago

Popular News

  • CHINA YAZIDI KUSISITIZA USHIRIKIANO KWA AFRIKA

    CHINA YAZIDI KUSISITIZA USHIRIKIANO KWA AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, SINGIDA BS MACHO ‘KAGAME CUP’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI : TAMKO LA PAMOJA CCM NA ACT-WAZALENDO LAFUNGUA NJIA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL.8/- KUISUKA AZAM FC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WADAU WAMGOMEA SAMATTA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?