• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK.NCHIMBI AMTAJA ASKOFU MFUMBUSA NGUZO YA UMOJA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 22, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK.NCHIMBI AMTAJA ASKOFU MFUMBUSA NGUZO YA UMOJA
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

MAKAMU wa Rais, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema taifa litaukumbuka mchango mkubwa alioutoa marehemu Askofu Bernadin Mfumbusa, enzi za uhai wake ukiwemo kuwa kiungo muhimu wa Kanisa Katoliki na dini zingine.

Balozi Dk. Nchimbi alisema hayo, baada ya kushiriki ibada ya kumuaga na kumwombea Askofu wa Jimbo Katoliki Kondoa, Mfumbusa, iliyofanyika Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba , Jimbo Kuu Katoliki Dodoma.

Alisema Askofu Mfumbusa alijitolea katika kuunganisha dini na madhehebu zifanye kazi kwa kuheshimiana, kushirikiana na kupendana.

Kwa mujibu wa Balozi Dk. Nchimbi, taifa litakumbuka mchango wake katika kuhamasisha elimu, kusimamia ujenzi na uendelezaji wa huduma za afya wilayani Kondoa na taifa kwa ujumla.

Makamu wa Rais alisema Askofu Mfumbusa alitoa mchango katika sekta ya mawasiliano na habari, akiwa mbobezi na mwalimu katika fani hiyo.

Nchimbi alisema Askofu Mfumbusa atakumbukwa kwa kutimiza wajibu wake kwa binadamu, kwa kutambua maisha ya kutimiza wajibu kwa Mungu.

SALAMU ZA RAIS

Pia, Balozi Dk. Nchimbi aliwasilisha salamu za pole za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, alizotoa kwa kanisa, waumini na familia na kuiombea familia nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Makamu wa Rais aliwashukuru viongozi wa Kanisa Katoliki kwa malezi ya Askofu Mfumbusa ambayo yalimfanya kuwa mtume wa taifa zima.

IBADA

Ibada hiyo, iliongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Mhashamu Wilbroad Kibozi na kuhudhuriwa na maaskofu mbalimbali, mapadre, watawa, viongozi  wa serikali na wananchi.

Previous Post

SITAWAANGUSHA

Next Post

SHILOLE AMSHUKURU RAIS DK. SAMIA

Next Post
SHILOLE AMSHUKURU RAIS DK. SAMIA

SHILOLE AMSHUKURU RAIS DK. SAMIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

ZANZIBAR MPYA YA DK. MWINYI YAVUTIA WANANCHI

ZANZIBAR MPYA YA DK. MWINYI YAVUTIA WANANCHI

11 months ago
WASOMI, VIONGOZI WA DINI WAGUSIA UZALENDO, AMANI  

WASOMI, VIONGOZI WA DINI WAGUSIA UZALENDO, AMANI  

9 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?