• ePaper
Wednesday, April 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

RAIS DK. SAMIA AMPA TANO SIMBU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 22, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
RAIS DK. SAMIA AMPA TANO SIMBU
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

WAKATI mwanariadha Alphonce Simbu akivuna dola za Marekani 75,000 (zaidi ya sh. milioni 195) kwa kushika nafasi ya pili katika mbio za Boston Marathon, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza Mtanzania huyo kwa hatua hiyo kubwa.

Simbu alivuna fedha hizo baada ya kushika nafasi ya pili katika mbio hizo zilizofanyika jijini Boston, Marekani.

Katika michuano hiyo, Simbu alishinda medali ya fedha baada ya kumaliza mbio kwa muda wa saa 2:02:47.

Akiandika katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, Rais Dk. Samia alimpongeza mwanariadha huyo kwa kushika nafasi hiyo.

 “Ninatoa pongezi za dhati kwa Alphonce Simbu kwa kushika nafasi ya pili na kuweka rekodi ya Taifa katika mashindano ya kimataifa ya mbio ya Boston (Boston Marathon), kwa mara ya pili mfululizo.

“Umeendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa letu, ukilitangaza jina la Tanzania kimataifa katika moja ya mashindano mashuhuri zaidi duniani, na umetuletea heshima kubwa katika ulimwengu wa michezo. Mafanikio yako ni chachu ya matumaini na hamasa kwa vijana wengi,” aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

Dk. Samia alisema Watanzania wanajivua mwanariadha huyo kutokana na jitihada alizonazo kimataifa.

WADAU WAFUNGUKA

Mwanariadha mkongwe, Juma Ikangaa, alisema Simbu ana haki ya kufanya vizuri katika mashindano hayo kutokana na maandalizi makubwa aliyoyafanya.

Alisema mwanariadha huyo amekuwa akijituma na kufanya mazoezi kwa muda mrefu jambo ambalo lilimuongezea nguvu ya kufanya vyema katika mbio hizo.

“Tanzania tunapaswa kujivunia kwa kipaji cha Simbu kwa sababu amekuwa na jitihada kubwa za kufanya mazoezi bila kuchoka, hili ndiyo linampa ushindi katika mashindano ya kimataifa,” alisema.

Kocha, Alfredo Shahanga alisema alikuwa ana imani kwamba Simbu atafanya vizuri kutokana na maandalizi bora aliyoyafanya.

Alisema jambo ambalo amefurahia kwake ni kuvunja rekodi ya kupunguza muda wa kukimbia baada ya mwaka jana kukimbia kwa muda wa saa 2:04:38 huku mwaka huu akikimbia kwa saa 2:02:47.

Previous Post

MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

Next Post

YANGA YATIMUA VUMBI CAF, SIMBA MMH

Next Post
YANGA YATIMUA VUMBI CAF, SIMBA MMH

YANGA YATIMUA VUMBI CAF, SIMBA MMH

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AWAONYA WATU WENYE NIA OVU

DK. SAMIA AWAONYA WATU WENYE NIA OVU

6 months ago
WAZIRI MKUU AGUSIA UMUHIMU WA TATHIMINI

WAZIRI MKUU AGUSIA UMUHIMU WA TATHIMINI

7 months ago

Popular News

  • DK.NCHIMBI AMTAJA ASKOFU MFUMBUSA NGUZO YA UMOJA

    DK.NCHIMBI AMTAJA ASKOFU MFUMBUSA NGUZO YA UMOJA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SITAWAANGUSHA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA YATIMUA VUMBI CAF, SIMBA MMH

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AMPA TANO SIMBU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?