• ePaper
Thursday, April 23, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 23, 2026
in Habari, Kitaifa
0
NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SELINA MATHEW, Dodoma

WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema serikali itaendelea kuimarisha sekta ya nishati nchini, kupitia mpango na bajeti ya mwaka 2026/2027, huku ikiainisha vipaumbele 10 vitakavyochochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.

Akiwasilisha mpango huo bungeni, jijini Dodoma, Ndejembi alisema maandalizi ya bajeti yamezingatia nyaraka mbalimbali muhimu, ikiwemo Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2025–2030, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mpango wa Nne wa Maendeleo ya Taifa (FYDP IV).

Ndejembi alivitaja vipaumbele hivyo ni kuimarisha uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme, kuongeza kasi ya kuunganisha umeme kwa wananchi, kuimarisha Gridi ya Taifa, kufanya matengenezo ya miundombinu ya umeme, kusambaza umeme vijijini na vitongojini.

Pia, kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia, kuimarisha uzalishaji wa gesi asilia, kuhakikisha upatikanaji wa mafuta, kuboresha miundombinu ya uhifadhi na usafirishaji wa nishati, na kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji wa nishati.

Alisema serikali itaendelea kuhakikisha Tanzania inakuwa na umeme wa kutosha kwa matumizi ya ndani na ziada ya kuuza nje, kuongeza kasi ya matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuimarisha upatikanaji wa mafuta na gesi asilia.

MIRADI MIKUBWA KUTEKELEZWA

Aidha, Ndejembi alieleza utekelezaji wa miradi mikubwa ya sekta ya nishati yenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa umeme, gesi na mafuta nchini, katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027.

Alisema serikali itatekeleza miradi mikubwa ya uzalishaji umeme ikiwemo Mradi wa Umeme wa Maji Julius Nyerere (MW 2,115) wenye gharama ya sh. bilioni 350, Kinyerezi III (MW 1,000) unaoendelea kupitia PPP, Umeme Jua Shinyanga (MW 150) wenye sh. bilioni 83.49 na Malagarasi (MW 49.5) wenye sh. bilioni 74.82.

Miradi mingine ni Kakono (MW 87.8) yenye sh. bilioni 95.19, Ruhudji (MW 358) sh. bilioni 115, Rumakali (MW 222) sh. bilioni 20 na Kikonge (MW 321) ambayo ipo katika maandalizi ya PPP.

Katika usafirishaji na uimarishaji wa umeme, alisema serikali itatekeleza miradi ikiwemo TAZA (Iringa–Sumbawanga) yenye thamani ya sh. 171.78, NEG Phase 2 (Chalinze–Dodoma) sh. bilioni 200, NEG Phase 1 (Chalinze–Mkuranga) sh. bilioni 5.05 na Nyakanazi–Kigoma yenye sh. bilioni 28.43.

Aidha, miradi ya kuimarisha Gridi ya Taifa ni Gridi Imara yenye thamani ya sh. bilioni 265, TTGRUP sh. bilioni 26.89, Benaco–Kyaka sh. bilioni 66.47 na Kituo cha Ibadakuli Shinyanga kilichotengewa sh. bilioni 20.

Kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), alisema serikali itatekeleza miradi ya umeme vijijini ikiwemo Last Mile Connectivity yenye sh. bilioni 188.8, Vitongoji awamu ya HEP IIA sh. bilioni 75, na HEP IIB sh. bilioni 20, huku kaya 200,000 zikitarajiwa kunufaika na nishati safi ya kupikia.

Katika sekta ya gesi na mafuta, alisema serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), itatekeleza miradi mikubwa ikiwemo LNG Project (maandalizi) yenye thamani ya sh. bilioni 20, bomba la gesi Ntorya–Madimba sh. bilioni 21.82 na upanuzi wa Madimba wenye thamani sh. bilioni 143.2.

Miradi mingine ni EACOP yenye sh. bilioni 100, hifadhi wa mafuta Kigamboni sh. bilioni 9.72 na TAZAMA mpya kuelekea Zambia yenye sh. bilioni tano.

Aidha, EWURA itaendelea kusimamia ubora wa mafuta na gesi na kuimarisha mifumo ya kidijitali ya udhibiti wa sekta, huku Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), ikiendelea kuratibu uagizaji na usambazaji wa mafuta kwa pamoja kupitia Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (BPS).

Alisema mfumo huo unalenga kuwezesha shughuli zote za BPS kufanyika kidijitali, ikiwemo usajili wa kampuni za mafuta, uthibitishaji wa awali wa kampuni zinazoshiriki zabuni za uletaji mafuta nchini, maoteo ya mahitaji ya mafuta, usimamizi wa zabuni, usafirishaji wa mafuta na masuala ya fedha.

Mfumo huo utasomana na mifumo ya taasisi zingine za serikali zinazoshirikiana na PBPA katika uagizaji wa mafuta huku jumla ya sh. bilioni tatu zikitengwa na PBPA kwa kazi hiyo.

Alisema serikali kupitia TPDC imeendelea kupanua mtandao wa gesi asilia nchini, ili kuongeza matumizi yake katika uzalishaji umeme, viwandani, vyombo vya usafiri, taasisi na majumbani, ambapo miradi mbalimbali mikubwa imetengewa fedha za utekelezaji katika mwaka 2026/2027.

Mradi wa usambazaji gesi asilia Dar es Salaam utahusisha ujenzi wa miundombinu Ubungo, Sinza, Mikocheni na Lugalo na kuunganisha wateja wapya 1,000, ambapo sh. bilioni sita zimetengwa kwa utekelezaji.

Aidha, mradi wa Kisemvule–Mbagala utahusisha ujenzi wa bomba la gesi hadi kituo cha Gesi Asilia (CNG) Mbagala na maeneo ya viwanda Zakhiem, ambapo serikali imetenga sh. bilioni 8.23.

Katika mikoa ya Lindi na Mtwara, serikali itatekeleza mradi wa kusambaza gesi katika maeneo ya Mtwara Mjini, Soko la Samaki, Shangani, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na taasisi mbalimbali za Serikali, ambapo sh. bilioni 5.2 zimetengwa.

Vilevile, serikali kupitia TPDC itajenga vituo vya CNG vinavyohamishika Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma pamoja maandalizi ya vituo vingine Tanga, Kilimanjaro na Arusha, ambapo sh. bilioni 22.06 zitatumika.

Alisema katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, mradi wa gesi asilia utahusisha ujenzi wa kituo cha kupokea gesi, mtandao wa usambazaji na kituo cha kujazia gesi kwenye magari, ambapo sh. bilioni 14.4 zimetengwa kwa utekelezaji wake.

Kwa upande wa usafirishaji wa gesi kwenda nchi jirani, alisema serikali itaendelea na maandalizi ya bomba la gesi kutoka Dar es Salaam kwenda Uganda na Kenya, ambapo sh. bilioni 4.18 zimetengwa kwa upembuzi yakinifu na utaratibu wa utekelezaji.

AJIRA MPYA, MAFUNZO, TAASISI KUIMARISHWA

Ndejembi alisema ajira mpya 1,439 zitatolewa katika sekta ya nishati, watumishi 5,207 watapatiwa mafunzo na 933 watapandishwa vyeo kwa kuongeza ufanisi wa kazi.

Alisema taasisi za TANESCO, REA, TPDC, EWURA na nyinginezo zitaendelea kuimarishwa ili kuongeza ufanisi wa huduma na kuhakikisha sekta ya nishati inachangia kikamilifu uchumi wa taifa.

SHILINGI TRILIONI 2.53

Katika utekelezaji wa mpango huo, aliliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya sh. trilioni 2.5 kwa wizara hiyo na taasisi zake, ambapo asilimia 97.5 sawa na zaidi ya sh. trilioni 2.46 zitaelekezwa katika miradi ya maendeleo, huku asilimia 2.5 (zaidi ya sh. bilioni 63) zikitumika kwa matumizi ya kawaida.

LIVINGSTON LUSINDE

Mbunge wa Mbunge wa Mtera, Livingston Lusinde, alisifu mwelekeo wa bajeti ya serikali, akisema kwa mara ya kwanza sehemu kubwa ya fedha imeelekezwa katika miradi ya maendeleo, badala ya matumizi ya kawaida.

Lusinde alisema hatua hiyo inaonesha dhamira ya dhati ya serikali kuwaletea wananchi maendeleo.

Akichangia mjadala wa bajeti bungeni, Lusinde alisema takribani asilimia 97 ya bajeti ya wizara imeelekezwa katika maendeleo.

Alisema hatua hiyo ni ishara ya wazi ya ushirikiano kati ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, waziri wa sekta husika na watendaji wa wizara kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kasi inayotarajiwa.

“Kwa uzoefu wangu bungeni, hii ni bajeti ya aina yake. Unapokuwa na asilimia 97 ya fedha zote kwenda kwenye maendeleo, ni wazi serikali imeamua kujenga taifa kwa vitendo,” alisema Lusinde.

Alibainisha kati ya sh.trilioni 1.5 zilizotengwa, sh. bilioni 63 pekee zinazotokana na wafadhili wa nje, akisisitiza sehemu kubwa ya fedha hizo ni za ndani ya nchi.

Pia, aliipongeza serikali kwa kusambaza umeme vijijini, lakini akashauri kuwepo kwa uwekezaji wa umeme mkubwa vijijini utakaowezesha shughuli za uzalishaji kama viwanda vidogo, usagaji na umwagiliaji kufanyika bila changamoto za kukatika kwa umeme.

Alisema kuwa sasa ni wakati wa kuhakikisha umeme wa vijijini hauishii kwenye matumizi ya mwanga pekee bali unakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi.

Aidha, alizungumzia umuhimu wa nishati safi ya kupikia, akisisitiza kuwa upatikanaji wa gesi safi nchini utaondoa utegemezi wa mkaa na kusaidia kulinda mazingira, huku akipongeza juhudi za serikali katika sekta hiyo.

Mbunge huyo alipendekeza taasisi za serikali kuboresha ushirikiano wa kiutendaji, akitoa mfano upimaji wa mita za umeme, kuna umuhimu wa kuhakikisha zinapimwa kabla ya kufungwa kwa watumiaji kuepuka malalamiko ya upotevu wa mapato na malipo yasiyo sahihi.

Alionya mita zisizopimwa zinaweza kusababisha changamoto kwa wananchi na serikali, akisisitiza uwazi na usahihi katika mifumo ya ukusanyaji mapato.

Pia alitoa wito wa kuimarishwa kwa viwanda vya ndani vinavyotengeneza vifaa vya umeme, akisema hatua hiyo itapunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje na kuimarisha uchumi wa ndani.

Previous Post

MWIGULU ATOA MAAGIZO ALAT

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WADAU MICHEZO WAMTUMIA SALAMU WAZIRI MAKONDA

WADAU MICHEZO WAMTUMIA SALAMU WAZIRI MAKONDA

3 months ago
YANGA YARIDHISHWA UUZAJI WA JEZI

YANGA YARIDHISHWA UUZAJI WA JEZI

8 months ago

Popular News

  • NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

    NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU ATOA MAAGIZO ALAT

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIPOTI YA KUPONYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWANDAAJI MISS WORLDTZ AITAJA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, MAFUNZO HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?