• ePaper
Monday, May 4, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

RIPOTI TUME YA JAJI CHANDE NI KIUNGANISHI CHA WANANCHI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 4, 2026
in Makala
0
RIPOTI TUME YA JAJI CHANDE NI KIUNGANISHI CHA WANANCHI
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na BULUGU MAGEGE

KATIKA dunia ya haki na uongozi bora, kauli ya Albert Einstein kwamba ‘hakuna tofauti kati ya jambo dogo na kubwa inapokuja suala la ukweli na haki’ inaendelea kuwa mwanga wa fikra sahihi.

Kauli hii ya Einstein ina ujumbe kuwa, hakuna jambo dogo wala kubwa kila jambo linastahili kuangaliwa kwa uzito ule ule. Huu ndiyo msingi wa uongozi bora, pale changamoto zinapojitokeza.

Hili ndilo tunaloliona kwa vitendo kupitia uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Uamuzi wake wa kuunda Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na a Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025 haukuwa uamuzi wa kawaida, bali ulikuwa ni wa kijasiri,  kizalendo na wenye  dhamira ya kweli ya kulinda na kuunganisha taifa.

Bila shaka uongozi huo unaoitwa wa mageuzi, ni aina ya uongozi unaokubali kukabiliana na changamoto, badala ya kuzikimbia, unaotumia migogoro ikiwa darasa la kujifunza, badala ya chanzo cha mgawanyiko na unaolenga kuleta maridhiano ya kweli.

Kwa kuunda Tume hii, Rais Dk. Samia ameonesha wazi anaamini katika nguvu ya ukweli kikiwa chombo cha kuijenga Tanzania iliyo imara zaidi.

Amefungua mlango wa kitaifa wa kusikilizana, kutafakari tulipotoka na kupanga kwa pamoja tunapotaka kwenda.

Huu ni mwanzo wa safari ya kuimarisha umoja wa kitaifa na kurejesha imani ya wananchi katika kushirikiana kuijenga Tanzania.

Kwa kifupi, hapa hatuzungumzii tu Tume, bali tunazungumzia mwelekeo wa taifa. Na katika mwelekeo huo wa uongozi wa Rais Dk. Samia anasimama akiwa nguzo ya kuunganisha Watanzania wote, bila kujali tofauti zao.

TUME IMEKUJA KUUNGANISHA TAIFA

Katika falsafa ya haki na sheria kwa mujibu wa wanasheria kuna mitazamo miwili mikuu ya haki.

Kwanza ni haki ya kuadhibu ambayo hulenga kubaini kosa na kutoa adhabu stahiki.

Pili ni haki ya kurejesha uhusiano ambayo huenda hatua zaidi kwa kulenga kuponya majeraha, kurejesha uhusiano kwa jamii na kujenga upya mshikamano uliovunjika.

Kinachofanya Ripoti ya Tume hii kuwa ya kipekee na kuwa ripoti bora  ni kwamba imejengwa zaidi katika misingi ya haki ya kurejesha uhusiano.

Haikujikita tu katika swali la nani alikosea, bali pia katika swali pana zaidi na la msingi taifa liponaje baada ya tukio kama hili?

Huu ni mtazamo mpana na unapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote.

Katika hotuba yake ya uwasilishaji wa ripoti, Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande, alieleza kwa maneno yenye maana nzuri na yanapaswa kuungwa mkono

“Kubeba dhamira ya pamoja ya Taifa ya kutibu majeraha, kuwajibika kila panapostahili, lakini muhimu zaidi kujifunza na kusonga mbele.”alisema.

Kauli hii inayobeba falsafa nzima ya kujenga taifa baada ya mtikisiko. Inaonesha wazi lengo halikuwa kulipiza kisasi, bali kujenga daraja la kuelekea kesho iliyo bora zaidi.

Huo ndiyo unaoitwa mfumo wa maridhiano ya kitaifa ambao hujengwa juu ya nguzo kuu tatu ambazo ni Ukweli  wananchi wasikike, ukweli ujulikane, Uwajibikaji wahusika waliohamaisha ghasia na vurugu wawajibe kwa mujibu wa sheria, Uponyaji wa jamii taifa lirudishe mshikamano wake

Kwa mantiki hiyo, ninaitizama Tume kama haikuwa tu chombo cha uchunguzi, bali  ilikuwa ni jukwaa la kitaifa la kuponya taifa.

Na hapa ndipo tunapoona upekee wa uongozi wa Rais Dk. Samia uongozi unaotambua kuwa nguvu ya taifa haipo tu katika sheria kali, bali pia katika uwezo wa kuunganisha watu wake baada ya majeraha.

Rais Dk. Samia ni kiongozi bora na anayetufundisha kuwa umoja nguvu na utengano ni udhaifu.

UHALALI KWA MISINGI YA KITAIFA,KIMATAIFA

Miongoni mwa nguvu kubwa niliyoiona katika Ripoti ya Tume ni kwamba haikujengwa juu ya maoni au mitazamo ya kisiasa, bali juu ya misingi imara ya sheria za ndani na za kimataifa. Hii ndiyo inayoipa uhalali unaokubalika kitaifa na kimataifa.

MSINGI WA SHERIA YA KIMATAIFA

Katika ngazi ya kimataifa, haki ya kukusanyika na kufanya maandamano inatambuliwa wazi chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa.Ibara ya 21 ya mkataba huo inaeleza ‘The right of peaceful assembly shall be recognized.’

Hii ina maana kuwa kila raia ana haki ya kukusanyika na kutoa  maoni yake.

Hata hivyo, mkataba huo hauachi haki hiyo bila mipaka. Unaweka bayana kuwa uhuru huo unaweza kuwekwa mipaka pale inapolenga kulinda usalama wa Taifa.

Kwa tafsiri nyepesi tunapaswa kuelewa kuwa haki ipo ndiyo, lazima itumike kwa namna isiyohatarisha usalama wa taifa, amani kwa jamii na haki za wengine.

Ndipo Tume ilipojenga hoja yake kwa uthabiti mkubwa. Kwa kuchambua mazingira, mwenendo wa matukio  na matokeo yake, ilibainisha  yaliyotokea hayakubaki ndani ya wigo wa maandamano ya amani, bali yalivuka mipaka na kuingia katika eneo la ghasia na uvunjifu wa amani.

Kwa lugha ya wanasheria, hapa kinazungumzia kile kinachoitwa ‘principle of proportionality’ yaani uwiano kati ya haki ya mtu na athari zake kwa jamii.

Pale ambapo utekelezaji wa haki unaleta madhara makubwa kwa jamii nzima, dola ina wajibu wa kikatiba na kisheria kuweka mipaka.

Hivyo, msimamo wa Tume haukuwa wa kubana haki, bali ulikuwa wa kulinda mfumo mzima wa haki, ikiwemo haki ya kuishi kwa amani, haki ya kufanya shughuli za kiuchumi na haki ya taifa kubaki salama na imara.

Kwa mtazamo huo, Ripoti ya Tume inaipa Tanzania sura ya taifa linaloheshimu haki, pia linalozilinda kwa busara na uwajibikaji huku likiendelea kuifanya Tanzania inaendelea kubakia salama, hapa ndipo tunaposema Rais Dk. Samia ni kiongozi wa kipekee na kujivunia.

Kwa hiyo, kuipongeza ripoti hiyo ni kutambua ushindi wa ukweli dhidi ya kelele, ushindi wa uchambuzi dhidi ya hisia, na ushindi wa taifa dhidi ya mgawanyiko.

Na nyuma ya mafanikio haya kuna uongozi wa Rais Dk. Samia, kiongozi aliyethubutu kuacha taasisi zifanye kazi kwa weledi na kwa kufanya hivyo, akaweka msingi imara wa kuimarisha umoja wa taifa na imani ya wananchi kwa serikali yao.

Nikihitimisha Plato aliwahi kuandika katika The Republic alisisitiza kwamba ‘the measure of a man is what he does with power,’akimaanisha kuwa thamani ya kiongozi hupimwa kwa namna anavyotumia mamlaka aliyonayo.

Kwa muktadha huo, uongozi wa Rais Dk. Samia umejitokeza kama mfano wa matumizi ya mamlaka kwa lengo la kujenga taifa bora, siyo kuficha pia kuleta uwazi, badala ya kufunika ukweli na kuimarisha misingi ya taifa na kulinda taswira ya muda mfupi.

Kwa mtazamo mpana, Ripoti ya Tume ni mwongozo wa mageuzi ya kitaifa, daraja la kuelekea maridhiano na kioo kinachoakisi hali halisi ya jamii.

Kiini cha mabadiliko haya kinatokana na uamuzi wa uongozi uliothubutu kuchukua hatua katika mazingira magumu.

“Kupitia uamuzi huo, Rais Dk. Samia ameonesha ujasiri wa kisiasa, hekima ya kiongozi na dhamira ya dhati ya kuunganisha taifa. Jukumu la kuujenga na kuimarisha linabaki mikononi mwa taifa lote,”alisema.

Mwandishi wa Makala hii ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Previous Post

JASHO LIMEMWAGIKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

ASKOFU MNDOLWA: TUME YA JAJI CHANDE ITAIPELEKA NCHI PAZURI

ASKOFU MNDOLWA: TUME YA JAJI CHANDE ITAIPELEKA NCHI PAZURI

3 weeks ago
TANZANIA NA CHINA ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI

TANZANIA NA CHINA ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI

4 months ago

Popular News

  • RIPOTI TUME YA JAJI CHANDE NI KIUNGANISHI CHA WANANCHI

    RIPOTI TUME YA JAJI CHANDE NI KIUNGANISHI CHA WANANCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JASHO LIMEMWAGIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA JUU YA CHINA YAWA CHACHU KUKUZA UCHUMI WA KIDIJITALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?