• ePaper
Thursday, May 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Biashara

DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 5, 2026
in Biashara, Habari, Kitaifa
0
DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewataka wananchi wa Tanzania na Kenya, kulinda na kuheshimu demokrasia kwa kuzingatia utaratibu, sheria na misingi ya uendeshaji wa serikali, hivyo wasikubali ichafue  nchi na mila zao.

Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jioni, alipohutubia Jukwaa la Kibiashara kati ya Tanzania na Kenya, lililofanyika katika Kituo cha Kitaifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC).

“Neno demokrasia lisituchafulie nchi zetu, wala mila zetu. Demokrasia haina fomula, demokrasia kule mbali ni tofauti na ya kwetu. Sisi kwetu tuna mila zetu na demokrasia zetu zinazokwenda na hiyo nafasi,” alisema.

Jukwaa hilo la kibiashara pia lilihudhuriwa na Rais wa Kenya, Dk. William Ruto, ambaye alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Alisema ujenzi wa mataifa hayo, unategemea zaidi nidhamu ya kiasiasa na uwajibikaji wa wananchi katika kuheshimu sheria na taasisi za dola.

Rais Dk. Samia alisema hakuna nafasi kwa mtu au kundi litakaloruhusiwa kuvuruga demokrasia au kuhatarisha amani ya nchi hizo.

Alisema nchi za Afrika Mashariki zinapaswa kusimama imara kulinda utulivu na maadili ya jamii, dhidi ya vitendo vinavyofanywa kwa kisingizio cha kupinga demokrasia.

Alisema yeye na Rais Dk. Ruto, walijadiliana namna ya kukabiliana na vijana wanaosababisha vurugu katika mataifa ya ukanda huo wakidai wanapigania haki za kidemokrasia.

“Nikamwambia Ruto, watovu wa adabu wako tusichague, wawe Watanzania au Wakenya, wakija kwangu nachapa na mikwaju wakija kwako wachape wakae sawa, hivyo matumizi mabaya ya neno demokrasia hayapaswi kuruhusiwa kuvuruga utamaduni na misingi ya jamii za Afrika Mashariki,”alisema Rais Samia.

Alifafanua, mataifa ya ukanda huo yana wajibu wa kujenga mfumo wa demokrasia unaozingatia mazingira, utamaduni na mahitaji ya wananchi wake, badala kuiga mifumo ya nje isiyoendana na uhalisia wa Afrika Mashariki.

Aliongeza mbali na ushirikiano wa kibepari na kiuchumi, siasa za nje au teknolojia mpya zisichafue utamaduni na mila za jamii za nchi mbili.

Rais Dk. Samia alisisitiza watoto wasiotii na wenye maovu, wakijaribu kutumia jina la demokrasia kwa njia mbaya, hawatakiwi kuwa sehemu ya harakati za maendeleo ya Tanzania na Kenya.

USHIRIKIANO WA KIUCHUMI

Rais Dk. Samia alisema ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya, ni sehemu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025, ambayo sekta binafsi ni mhimili mkuu wa utekelezaji.

“Sekta binafsi ni mchezaji mkuu wakati tunatekeleza Dira yetu, mkutano wa aina hii ni muhimu sana kufungua fursa za uwekezaji na biashara,” alisema.

Aliwahakikishia wafanyabiashara kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana kwa karibu zaidi na Kenya, kufanikisha ujenzi wa miundombinu na kuweka mazingira rafiki ya biashara.

Pia, Rais Dk. Samia alisisitiza, kamati za pamoja za kibiashara zitaendelea kukaa kusuluhisha changamoto za biashara na za uwekezaji wa haraka na ufanisi.

Aidha, alionesha umuhimu wa kufuata sheria na kulipa kodi ipasavyo, kwa kuwa ndizo zitakazoboresha miundombinu na kurahisisha uwekezaji.

Pia, alizishukuru kampuni za Kenya zilizowekeza nchini na kutengeneza ajira, kulipa kodi na kusaidia maendeleo ya nchi.

Rais Samia alizipongeza kampuni za Tanzania zilizowekeza Kenya, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya biashara kwa heshima na kufuata sheria za nchi hizo.

AHIMIZA MSHIKAMANO

Aidha, Rais Dk. Samia alisisitiza mshikamano wa nchi hizo akisema Tanzania na Kenya ni nchi jirani zenye uhusiano wa kihistoria unaojengwa juu ya ushirikiano, utengamamo na mshikamano wa muda mrefu.

“Tunapaswa kushirikiana kama kiumbe chenye miguu mitatu: ikiwa kichwa kimoja kikakaidi, wote tutaanguka. Tunapaswa kuwa wamoja, kushirikiana kwa uaminifu, heshima na upendo,”  alisema Rais Dk. Samia.

 RAIS DK. RUTO

“Huwezi kugawana umaskini, lakini unaweza kugawana utajiri. Lazima tuwaruhusu wafanyabiashara wazalishe utajiri kwa sababu kuna fursa ya kugawana tulichonacho. Hatuwezi kugawana kile tusichonacho.

“Tunataka kurekebisha uhusiano wetu, kuunda upya ushirikiano wetu, kwa sababu kama ilivyosemwa hapa, Wakenya si maadui wa Watanzania, na Watanzania si maadui wa Wakenya,”alisema Rais Ruto, katika hotuba yake.

Aliongeza; “Adui yetu ni umaskini, ukosefu wa ajira na ukosefu wa maendeleo. Pia, tunaweza kukabiliana na adui huyu pamoja. Tutafanikiwa pamoja, kadri tunavyoelewa hilo mapema na haraka, ndivyo ilivyo bora kwa sisi sote na ndivyo tutakavyopata suluhisho la haraka,” alisema.

Ruto alisema uwekezaji wa Kenya nchini Tanzania, unazidi dola bilioni 1.7, ukihusisha huduma za kifedha, viwanda, mawasiliano na rejareja huku akiiweka Kenya kama chanzo cha kuaminika cha pembejeo za viwandani kwa Tanzania.

Alieleza uwekezaji wa Tanzania nchini Kenya, ni zaidi ni ya dola milioni 330 na unaongezeka, hasa katika sekta za utalii, viwanda, nishati na kilimo.

“Zaidi ya biashara na mtaji, watu wetu bado ndiyo uti wa mgongo wa ushirikiano huu. Uhuru wa kutembea kwa watu, wafanyakazi, huduma na mtaji unaendelea kufungua ubunifu, ujasiriamali na fursa za pamoja.

“Nina furaha sana leo (juzi), dada yangu Rais Dk. Samia tumekubaliana kutoa maelekezo pamoja na nia njema kutoka ngazi za juu za serikali kwa maofisa wetu kwamba, vikwazo vyote vya kibiashara visivyo vya ushuru vilivyobaki, vishughulikiwe kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Mei, tuweze kutoa fursa bila vikwazo kwa wafanyabiashara wetu kufanya kazi,” alisema Rais Dk. Ruto.

KAULI PROFESA KITILA

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, alisema Tanzania na Kenya zimekubaliana kuwa na utaratibu wa kufanya majukwaa ya uwekezaji mara kwa mara.

Previous Post

ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

Next Post

RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

Next Post
RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SINGIDA, SIMBA BALAA ZITO LEO

SINGIDA, SIMBA BALAA ZITO LEO

2 months ago
SABABU SARE AZAM, YANGA SC IKO HAPA

SABABU SARE AZAM, YANGA SC IKO HAPA

2 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS RUTO AIPONGEZA NSSF TANZANIA KWA UWEKEZAJI WA DOLA ZAIDI YA MILIONI 51 NAIROBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KAMILI AFCON 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?