• ePaper
Sunday, June 28, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA YASISITIZA KUTUMIA AKILI UNDE KUKABILI MAAFA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 11, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA YASISITIZA KUTUMIA AKILI UNDE KUKABILI MAAFA
0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU, Zimbabwe

TANZANIA imesema itaendelea kutumia teknolojia ya Akili Unde (AI) katika kuimarisha mifumo ya usimamizi wa maafa nchini kwa nia ya kuongeza ufanisi wa utoaji tahadhari za mapema na kupunguza madhara yatokanayo na na majanga.

Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dk. Jim Yonazi, wakati wa mkutano wa maandalizi ya mkutano wa sita wa kawaida wa kamati ya mawaziri wanaohusika na usimamizi wa maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Mei 11, 2026 mjini Masvingo, Zimbabwe.

Alisema matumizi ya AI yatasaidia uchakataji na ufuatiliaji wa taarifa zinazoripotiwa kuhusu masuala ya maafa nchini, hatua inayolenga kuongeza uwezo wa serikali katika kufanya uamuzi wa haraka wakati wa majanga.

“Matumizi ya teknolojia ya Akili Unde yatawezesha uchambuzi wa taarifa kwa haraka, kutabiri hatari zinazoweza kujitokeza na kusaidia hatua za mapema za kukabiliana na maafa,” alisema Dk. Yonazi.

Alisema serikali inaendelea kuweka mkazo katika maeneo muhimu yatakayosaidia kuwa na usimamizi wenye tija wa maafa ikiwemo utafiti wa kisayansi, matumizi sahihi ya Akili Unde, ushirikiano katika uhifadhi wa taarifa za matukio pamoja na matumizi ya menejimenti ya maarifa.

Aidha, alisema Tanzania imeendelea kuwa mfano katika ukanda wa Kusini mwa Afrika kutokana na uwezo wake wa kuratibu na kusimamia maafa kwa mafanikio ikiwemo huku kuendelea kuzuia, kupunguza madhara, kujiandaa na kurejesha hali pindi majanga yanapotokea.

Katibu mkuu huyo alifafanua mafanikio hayo yamechangiwa na uwepo wa Kituo cha Ufuatiliaji wa Mwenendo wa Majanga na Tahadhari ya Mapema ambacho hufanya kazi saa 24 kupokea, kufuatilia na kuchambua taarifa za majanga kwa wakati halisi.

“Kituo cha operesheni ya maafa kimekuwa msaada mkubwa, kwani kimerahisisha upatikanaji wa taarifa za mapema, uchambuzi wa takwimu za wakati halisi na upangaji wa mikakati ya kurejesha hali pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na maafa,” alisisitiza Dk. Yonazi.

Previous Post

HATI YA MAKUBALIANO YA KUANDAA AFCON 2027 YASAINIWA

Next Post

CG MWENDA ASISITIZA USALAMA, BIASHARA NA MAPATO KATIKA MKUTANO WA WCO ESA

Next Post
CG MWENDA ASISITIZA USALAMA, BIASHARA NA MAPATO KATIKA MKUTANO WA WCO ESA

CG MWENDA ASISITIZA USALAMA, BIASHARA NA MAPATO KATIKA MKUTANO WA WCO ESA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

JASHO LIMEMWAGIKA

JASHO LIMEMWAGIKA

5 months ago
ATCL YARUDISHA WATANZANIA 236

ATCL YARUDISHA WATANZANIA 236

4 months ago

Popular News

  • HAKUNA MJADALA AMANI, USALAMA WA NCHI-MWIGULU

    HAKUNA MJADALA AMANI, USALAMA WA NCHI-MWIGULU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VIJANA 400  WAAGWA KWENDA KUFANYA KAZI NJE YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘NAFUU YA MAFUTA KUANZA KUONEKANA JULAI’ NDEJEMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZOTE KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL-NINO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?