• ePaper
Friday, May 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

HAKIKISHENI GESI YENU INAPIMWA KABLA YA KUNUNUA – KIHULLA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 14, 2026
in Habari, Kitaifa
0
HAKIKISHENI GESI YENU INAPIMWA KABLA YA KUNUNUA – KIHULLA
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

AFISa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Alban Kihulla amewaambia Waheshimiwa Wabunge kuwa WMA hufanya uhakiki wa mitungi ya gesi ya kupikia inayouzwa nchini ili kujiridhisha kuhusu ujazo wake kabla ya kuingia sokoni.

Akizungumza katika semina kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, kuhusu majukumu ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zake iliyofanyika Mei 13, 2026 Bungeni Dodoma, Kihulla alisisitiza kuwa jukumu la WMA ni kuhakiki na kusimamia usahihi wa vipimo katika sekta zote, ikiwemo nishati.

Hata hivyo amewahimiza wananchi wakiwemo wabunge kuchukua tahadhari zaidi wakati wa kununua gesi.

“Kabla ya kununua gesi, hakikisheni mtungi huo unapimwa na muuzaji mbele yenu ili kujiridhisha kuhusu ujazo wake. Epukeni kununua gesi kutoka kwa wauzaji wasio na mizani, kwa sababu hutaweza kujua kama gesi uliyonunua ina ujazo sahihi kama ilivyoandikwa kwenye mtungi”, alisema Kihulla.

Akitoa mwongozo wa jinsi ya kutofautisha uzito ulioandikwa kwenye mtungi, Kihulla ameeleza kuwa kila mtungi wa gesi una maelezo mawili muhimu ya uzito ambayo mwananchi anapaswa kuyafahamu ambayo ni Net Weight na Gross Weight.

“Net Weight ni uzito wa gesi pekee iliyomo ndani ya mtungi. Hii ndiyo kiasi unacholipa. Gross Weight ni uzito wa gesi pamoja na uzito wa mtungi tupu.”

Alisema wakati muuzaji anapima mtungi uliojaa gesi, mnunuzi anapaswa kuangalia kama uzito unaooneshwa kwenye mzani unalingana na jumla ya net weight iliyoandikwa kwenye mtungi pamoja na uzito wa mtungi tupu. Ikiwa mzani unaonesha chini ya jumla hiyo, basi kuna upungufu wa gesi.

Amesema changamoto iliyopo kwa sasa ni kuwa wananchi wengi bado hununua gesi kwa mazoea bila kujali kama muuzaji ana mzani na amepima mtungi huo au la.

Pia amebainisha kuwa baadhi ya wananchi huagiza vijana wa bodaboda kuwanunulia gesi ili kurahisisha usafirishaji, bila wao wenyewe kuwepo ili kujiridhisha. Hali hiyo inawafanya kukosa uhakika kuhusu ujazo halisi wa gesi wanayonunua.

Katika ufafanuzi wake, Kihulla pia amezungumzia upimaji wa tochi za barabarani zinazotumiwa na askari kupima mwendo wa magari. Amesema WMA huhakiki tochi hizo ili kuhakikisha zinapima kwa usahihi na haki inatendeka kwa wamiliki wa magari.

“Hata hivyo, nawasihi wananchi kuwa endapo mtatilia shaka au kubaini kuna tatizo la usahihi wa vipimo popote pale, msisite kuwasiliana na WMA kwa hatua za haraka,” alisema.

Awali, kupitia wasilisho la video, Kihulla alieleza kuwa WMA inasimamia matumizi sahihi ya vipimo katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, kilimo, miundombinu, madini, maji, ujenzi, nishati na usafiri.

Aidha, alisema Wakala hiyo inajiandaa kuanza uhakiki wa vipimo katika maeneo mapya ikiwemo sekta ya mawasiliano hususan kuhakiki usahihi wa bando za intaneti na dakika za simu zinazotolewa na makampuni ya mawasiliano ili kuongeza wigo wa ulinzi wa mwananchi.

Amesema, lengo ni kuhakikisha mteja anapata kiasi halisi cha data au dakika alichonunua, bila kupunguzwa au kupotea kabla ya muda wake kuisha.

Previous Post

TANZANIA, KENYA WAJADILI KUIMARISHA NJIA ZA UMEME

Next Post

TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA FORODHA KIKANDA – CG MWENDA

Next Post
TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA FORODHA KIKANDA – CG MWENDA

TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA FORODHA KIKANDA - CG MWENDA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AMLILIA ODINGA

DK. SAMIA AMLILIA ODINGA

7 months ago
DK. NCHIMBI ATANGAZA MITAA YA VIWANDA NCHINI

DK. NCHIMBI ATANGAZA MITAA YA VIWANDA NCHINI

9 months ago

Popular News

  • KIHONGOSI AKEMEA ‘WANAOVIMBA’ CCM

    KIHONGOSI AKEMEA ‘WANAOVIMBA’ CCM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MARUFUKU KUZUIA WANAFUNZI MITIHANI KISA ADA – DK. MWIGULU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA FORODHA ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA FORODHA KIKANDA – CG MWENDA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HAKIKISHENI GESI YENU INAPIMWA KABLA YA KUNUNUA – KIHULLA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?