• ePaper
Friday, May 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA FORODHA KIKANDA – CG MWENDA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 14, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA FORODHA KIKANDA – CG MWENDA
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda, amesema Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika masuala ya forodha ili kuongeza ufanisi wa biashara na kulinda uchumi wa nchi.

Ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa 32 wa Baraza la Uongozi la Shirika la Forodha Duniani Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (WCO ESA) uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar.

Akizungumza katika mkutano huo, Kamishna Mkuu Mwenda amesema Tanzania imeendelea kuwa lango muhimu la biashara na kitovu cha kuaminika kwa wawekezaji na washirika wa kimataifa, akieleza kuwa mabadiliko ya biashara ya dunia yanayochochewa na teknolojia, biashara za mtandaoni na akili mnemba (AI) yanahitaji mifumo imara ya forodha yenye uwezo wa kurahisisha biashara na kulinda uchumi wa nchi.

Aidha, ameeleza kuwa TRA imepiga hatua kubwa katika mageuzi ya kidijitali kupitia Mfumo wa Elektroniki wa Ushirikiano wa Forodha Tanzania, ambao umeboresha uwazi, kasi ya huduma na uratibu wa taasisi mbalimbali katika mnyororo wa biashara.

Mwenda pia amesisitiza kuwa licha ya maendeleo hayo, bado kuna umuhimu wa kuendelea kuimarisha uwezo wa kiusalama mipakani kwa kutumia teknolojia za kisasa kama skana za mizigo, ndege zisizo na rubani (drones) na mifumo ya ufuatiliaji wa hatari ili kudhibiti magendo na biashara haramu.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu Mwenda, majadiliano hayo ni fursa muhimu ya kuimarisha mshikamano wa kikanda na kuboresha utendaji wa taasisi za forodha ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii katika ukanda wa ESA na dunia kwa ujumla.

Previous Post

HAKIKISHENI GESI YENU INAPIMWA KABLA YA KUNUNUA – KIHULLA

Next Post

WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA FORODHA ZANZIBAR

Next Post
WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA FORODHA ZANZIBAR

WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA FORODHA ZANZIBAR

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA : KASI YA MAENDELEO HAITASINANA

DK. SAMIA : KASI YA MAENDELEO HAITASINANA

8 months ago
DK. SAMIA, AWAAHIDI WATANZANIA NEEMA  AKICHAGULIWA OKTOBA 29

DK. SAMIA, AWAAHIDI WATANZANIA NEEMA AKICHAGULIWA OKTOBA 29

8 months ago

Popular News

  • KIHONGOSI AKEMEA ‘WANAOVIMBA’ CCM

    KIHONGOSI AKEMEA ‘WANAOVIMBA’ CCM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MARUFUKU KUZUIA WANAFUNZI MITIHANI KISA ADA – DK. MWIGULU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA FORODHA ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA FORODHA KIKANDA – CG MWENDA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HAKIKISHENI GESI YENU INAPIMWA KABLA YA KUNUNUA – KIHULLA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?