• ePaper
Saturday, June 13, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WASOMI WADOKEZA MANUFAA YA UWEKEZAJI MAENEO MANNE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 9, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WASOMI WADOKEZA MANUFAA YA UWEKEZAJI MAENEO MANNE
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na EMMANUEL MOHAMED

BAADHI ya wasomi nchini, wamesema Tanzania itanufaika katika uwekezaji wa maeneo ya viwanda, kilimo, biashara na teknolojia.

Manufaa hayo, yatatokana na ziara ya Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam, aliyepo nchini kwa siku tatu.

Shanmugaratnam, aliwasili nchini jana kwa ziara hiyo, ambayo atahitimisha kesho.

Katika ziara hiyo, Shanmugaratnam ameongozana na mwenza wake, Jane, maofisa wakuu wa serikali na wawakilishi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Singapore.

Wasomi hao wamesema ujio wa viongozi wa kimataifa, imeonesha ni sehemu ya kuhakikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 inaanza kutekelezwa haraka kwa sababu hao ndio wadau wakubwa wa kushirikiana nao katika utekelezaji wake.

Kauli hiyo, waliitoa kwa nyakati tofauti walipozungumza na gazeti hili kuhusu ujio wa Rais wa Singapore.

DK. MOHAMED MAGUO

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk. Mohamed Maguo, alisema Singapore ni nchi yenye uzoefu mkubwa katika eneo la usimamizi wa viwanda, hivyo kinachotarajiwa kwa wafanyabiashara kutoka nchi hiyo, watavutiwa na eneo la uwekezaji wa viwanda kulingana na mazingira rafiki yaliyopo nchini.

“Sababu uchumi tulio nao hivi sasa ambao tunapigia kelele ni ule wa viwanda, hivyo matarajio yetu ni kuwa, ziara hii wafanyabiashara hao watajionea fursa za kuwekeza eneo la viwanda kwa sababu Tanzania ina sera rafiki. 

“Ziara hii, inafungua mlango kwa kampuni za Singapore kuwekeza katika viwanda Tanzania, ushirikiano huu unaweza kuongeza ajira na kuboresha miundombinu ya kiuchumi,” alisema.

Alisema katika eneo hilo la viwanda, itasaidia kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinaongezewa thamani kwa kushindana masoko ya nje.

“Tuna matumaini kuwa, wafanyabiashara hao watakutana na wafanyabiashara wa Tanzania, maana yake watabadilishana mawazo ya kuona namna gani ya kuwekeza maeneo ambayo wenzetu watavutiwa nayo na kuongeza uzalishaji na ukuaji wa uchumi,” alisema.

Dk. Maguo, alisema ujio wa viongozi wa aina hiyo, unahusiana na masuala ya diplomasia ya uchumi ambapo inaendana na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050, kwa kuhakikisha wanashirikiana nao katika maeneo ya teknolojia, biashara. 

“Yale ambayo yameainishwa katika dira hii ambayo ilizinduliwa, yanaanza kutekelezwa kwa haraka, haya yote anayoyafanya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha utekelezaji wa dira unaanza mara moja,” alisema.

DK. SYLVESTER RUGEIHYAMU

Mhadhiri wa Hisabati kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Saalam (UDSM), Dk. Sylvester Rugeihyamu, alisema ujio wa Rais wa Singapore, utasaidia kutoa fursa ya uwekezaji maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo.

Alisema sekta ya kilimo itawezesha kutoa fursa kubwa ya masoko ya bidhaa za kilimo nchini humo.

Dk. Rugeihyamu, alisema wafanyabiashara wa kilimo nchini, watanufaika na ujio wa Rais Shanmugaratnam kwa sababu Singapore inakabiliwa na uhaba wa ardhi katika shughuli ya kilimo.

Alisema hali hiyo, inawalazimu kutegemea zaidi chakula kutoka nje na wafanyabiashara wa Tanzania, watanufaika kupitia eneo hilo kwa kupeleka bidhaa hizo za kilimo.

Dk. Rugeihyamu, alisema Tanzania ina nafasi kubwa ya kunufaika kutokana na uwezo wake katika uzalishaji wa mazao ya kilimo, jambo litakalofungua masoko mapya kwa wakulima na wafanyabiashara wa ndani.
DK.TIMOTHY LYANGA

Mhadhiri wa Masuala ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu Huria (OUT), Dk. Timothy Lyanga, alisema ziara hiyo ya Rais Shanmugaratnam ni mwendelezo mzuri kwa kile ambacho kimefanyika hivi karibuni nchini Russia.

“Tumejionea viongozi mbalimbali wamekuja akiwemo Rais wa Kenya, William Ruto, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, hivi sasa anatoka Rais wa kutokea Bara la Asia, huo ni mwendelezo wa kuchukua fursa zaidi za kibiashara, kiuchumi na kiuwekezaji.

“Kiongozi wa aina hiyo anapokuja, anafuatana na wafanyabiashara ambao ni wawekezaji, hiyo ni fursa nzuri kwa watu wa Tanzania  na  Singapore, kwa kuwa ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua kubwa za maendeleo, ujio huo ni fursa kubwa kwa Tanzania,” alisema.

Dk. Lyanga, alisema ujio huo ni fursa adhimu kwa Tanzania kuongeza ushirikiano wa kibiashara na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nchi yenye uchumi thabiti kama Singapore.

“Tanzania inaweza kunufaika kwa kupata teknolojia ya kisasa ya uchakataji bidhaa za vyakula, pia kuimarisha viwango vya bidhaa zetu katika soko la kimataifa na kampuni za Singapore, zina uzoefu mkubwa wa usimamizi wa viwanda na hii ni fursa kubwa kwetu,” alisema.

Dk. Lyanga alisema ujio wa viongozi wa aina hiyo ni maono ya Rais Dk. Samia kuwa, inapoanza utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na kwamba, kupitia ziara hizo, Tanzania inajifunza kutoka katika mataifa ambayo yamepiga hatua.

“Ukiona Singapore katika kipindi ambacho tunapata uhuru kama tulikuwa tupo sawa kimaendeleo, lakini sasa hivi wenzetu wapo hatua ya juu sana ya maendeleo, kwa hiyo tunapokwenda kutekeleza dira hiyo, manaa yake tunakwenda kujifunza kwa wenzetu ambao wameishafika, sisi tunaelekea kuyafikia,” alisema.

Akihojiwa katika mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC 1, Balozi wa Tanzania nchini Singapore mwenye makao yake Indonesia, Macocha Tembele, alisema Singapore haina ardhi ya kutosha ya shughuli za kilimo.

“Kulikuwa na programu zamani, baadaye waliibadilisha, unajua janga la COVID – 19 liliwafundisha somo moja kubwa, wao walikuwa wakiagiza vyakula, baada ya ugonjwa huo kutokea na usafirishwaji ulivyositishwa, walipata shida kidogo,”alisema

Alisema miongoni mwa mafunzo waliyopata kutokana na COVID 19 ni kuhakikisha wanaongeza wigo wa kuagiza vyakula kutoka nchi mbalimbali.

“Hivi sasa, Tanzania tunaweza kuungana nao katika kuzalisha vyakula nchini na kutumia teknolojia walizo nazo kusafirisha nchini kwao,” alisema.

Alisema katika eneo la kilimo, kuna fursa kubwa ya wafanyabiashara wa sekta hiyo kunufaika kupitia ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Singapore.

“Tayari kutakuwa na jukwaa la kibiashara litafanyika, tayari wafanyabiashara wengi wa Singapore ambao wapo katika sekta ya kilimo, kwa hiyo inategemea watachangamkia fursa hii kwa kushirikiana nao eneo la kilimo,” alisema 

Previous Post

YANGA, SIMBA ZATOA MSIMAMO LIGI KUU BARA

Next Post

RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA KEMKEMU

Next Post
RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA KEMKEMU

RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA KEMKEMU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

3 weeks ago
MAAGIZO MATATU KWA DK. NCHEMBA

MAAGIZO MATATU KWA DK. NCHEMBA

7 months ago

Popular News

  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NI MWENDO WA KIDIGITALI, SUKARI SASA KUCHANGIA BIMA YA AFYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?