• ePaper
Saturday, August 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA ATHIBITISHA NIA YA MARIDHIANO KUELEKEA MCHAKATO WA MABORESHO YA KATIBA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 31, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA ATHIBITISHA NIA YA MARIDHIANO KUELEKEA MCHAKATO WA MABORESHO YA KATIBA
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendeleza maridhiano ya kisiasa kuelekea hatua za maboresho ya Katiba kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.

Rais Dk. Samia ameyasema hayo Julai 30, 2026, alipokutana na viongozi wa vyama 18 vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalihusu maridhiano, mageuzi ya kisiasa, uchumi, huduma za jamii, ajira, uwekezaji na ulinzi wa amani ya nchi.

Akirejea hatua ya mchakato wa maridhiano visiwani Zanzibar, Rais Dk.Samia amewaeleza viongozi hao hatua zilizofikiwa za maandalizi ya mchakato wa maridhiano kuelekea hatua zinazofuata za mapitio ya Katiba.

Amesisitiza kuwa hatua zote za mchakato huo zitafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu zilizowekwa, kwa maslahi mapana ya Taifa, na kwamba Serikali itaendelea kukutana na viongozi wa vyama vya siasa kwa mazungumzo katika kipindi cha angalau mara tatu kwa kila mwaka.

Mkutano huo, umewaleta  pamoja wenyeviti, makamu wenyeviti, makatibu wakuu na viongozi wa jumuiya za vyama vya siasa nchini, ni wa pili wa aina hiyo kuitishwa na Rais Dk. Samia tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Mkutano wa awali ulifanyika Machi 31, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam, ukiwakutanisha wagombea wa nafasi ya Rais na wagombea wenza kutoka vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumzia taswira ya uchumi wa nchi, Rais Dk.Samia amesema uchumi wa nchi umeendelea kukua kwa asilimia sita katika mwaka uliopita, huku ukuaji wa asilimia 6.3 ukitarajiwa mwaka huu.

Amesema Serikali imeweka msisitizo katika kukamilisha miradi ya maendeleo iliyokwishaaanza kutekelezwa, pamoja na kuendeleza uwekezaji katika miundombinu ya kimkakati ikiwemo reli, barabara, bandari na miundombinu mingine.

Katika uwekezaji, Rais Dk.Samia amesema maboresho yaliyofanywa katika Bandari ya Dar es Salaam yameongeza uwezo wa bandari hiyo kuhudumia biashara ya ndani na kikanda, na kubainisha kuwa Serikali inaendelea na upanuzi wa shughuli katika bandari za Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa.

Halikadhalika, Rais Dk. Samia amevitaka vyama vya siasa nchini kulinda amani, uhuru na maslahi ya nchi, akisisitiza kuwa ulinzi wa Tanzania ni wajibu wa pamoja baina ya Serikali, vyama vya siasa na wananchi wote.

Katika hatua nyingine, viongozi hao wamewasilishs  maoni yao kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa wananchi katika nyanja za siasa, maendeleo ya jamii na uchumi. Serikali imeahidi kuendelea kuyapokea na kuyafanyia kazi mapendekezo hayo kupitia majukwaa stahiki ya majadiliano na mifumo rasmi ya maamuzi.

Previous Post

SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

Next Post

RAIS DK. SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI ANGOLA

Next Post
RAIS DK. SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI ANGOLA

RAIS DK. SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI ANGOLA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AWAPA KICHEKO KARAGWE

DK. SAMIA AWAPA KICHEKO KARAGWE

10 months ago
ANNA ABDALLAH, LUBINGA, KHATIB WAUTETEA MUUNGANO

ANNA ABDALLAH, LUBINGA, KHATIB WAUTETEA MUUNGANO

3 weeks ago

Popular News

  • KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAMU, CHUNGU DABI YA K’KOO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TEC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA RAHA VIGOGO USHIRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BILIONI 30/- KUJENGA UWANJA WA KISASA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?