• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NDEJEMBI AZITAKA TAASISI ZA MUUNGANO KUIMARISHA USHIRIKIANO, HUDUMA KWA WANANCHI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 28, 2026
in Habari, Kitaifa
0
NDEJEMBI AZITAKA TAASISI ZA MUUNGANO KUIMARISHA USHIRIKIANO, HUDUMA KWA WANANCHI
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa Deogratius John Ndejembi, amezitaka Taasisi za Muungano kuimarisha ushirikiano, kubaini na kutumia fursa zilizopo pamoja na kushiriki kwa pamoja katika shughuli mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuongeza tija na kuleta manufaa zaidi kwa Watanzania.

Makamu wa Rais ametoa wito huo leo, Septemba 19, 2026 wakati akifungua kikao cha Wakuu wa Taasisi za Muungano kilichofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar, na kuhudhuriwa na wakuu wa Taasisi 39 za Muungano.

Makamu wa Rais amewataka viongozi wa taasisi hizo kuelewa kwa kina wajibu wao katika kuwahudumia wananchi na kufanya kazi kwa mtazamo mmoja wa kujenga “nyumba moja”, huku maslahi ya Watanzania yakiwekwa mbele.

Amesema matarajio ya wananchi ni kuona Muungano na taasisi zake zikitoa matokeo yanayogusa maisha yao moja kwa moja, hususan katika kuboresha hali ya uchumi, afya, elimu na maeneo mengine muhimu ya kijamii.

Amezihimiza taasisi hizo kuondoa vikwazo vinavyoweza kudhoofisha ushirikiano na badala yake kutumia fursa zilizopo katika pande zote mbili za Muungano ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aidha, Ndejembi ameahidi kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kuunga mkono jitihada za Taasisi za Muungano kwa kuratibu, kusimamia, kushauri na kuziwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi, kwa lengo la kuharakisha maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amesema kikao hicho kinalenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za Muungano na Ofisi ya Makamu wa Rais; na kuongeza uelewa wa pamoja kuhusu masuala mbalimbali ya Muungano na majukumu yanayotekelezwa na taasisi hizo, sambamba na kuweka mwelekeo wa kuimarisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi.

Kikao hicho cha Wakuu wa Taasisi za Muungano ambacho pia kimehudhiriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hamza Hassan Juma, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa Taasisi kinatoa  nafasi kwa viongozi hao kujadili namna ya kuimarisha uratibu, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja itakayoongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa manufaa ya wananchi.

Previous Post

MUSEVENI ABARIKI MCHELE TANZANIA KUUZWA UGANDA

Next Post

MAFUNZO YA ITIKADI MSINGI IMARA KATIKA KUIMARISHA UHAI WA CCM

Next Post
MAFUNZO YA ITIKADI MSINGI IMARA KATIKA KUIMARISHA UHAI WA CCM

MAFUNZO YA ITIKADI MSINGI IMARA KATIKA KUIMARISHA UHAI WA CCM

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TRILIONI 2.46/- ZATENGWA KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO YA NISHATI – HOMERA

TRILIONI 2.46/- ZATENGWA KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO YA NISHATI – HOMERA

2 days ago
RAIS DK. SAMIA AWAGUSA WENGI

RAIS DK. SAMIA AWAGUSA WENGI

10 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?