• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Makala

MAFUNZO YA ITIKADI MSINGI IMARA KATIKA KUIMARISHA UHAI WA CCM

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 29, 2026
in Makala, Siasa
0
MAFUNZO YA ITIKADI MSINGI IMARA KATIKA KUIMARISHA UHAI WA CCM
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA MUSSA YUSUPH

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza utekelezaji mfumo wa kitaifa wa Mafunzo ya Wakufunzi (TOT), unaolenga kupata wakufunzi 840 katika wilaya zote 168 za Chama.

Maudhui ya mafunzo hayo yamejikita katika muundo na historia ya CCM, misingi na itikadi, maadili katika itikadi na falsafa ya Chama, ujenzi wa makada, ujenzi upya wa imani ya wanachama na wananchi, pamoja na uwezo wa kujenga hoja na kutumia mazingira ya kidijiti katika elimu na mawasiliano ya kisiasa.

Baada ya mafunzo, makada hao watashiriki katika utoaji mafunzo kwa wanachama kwenye kata kwa kipindi cha siku 16 katika wilaya zote.

Shughuli hizo zitaambatana na ujenzi wa Chama, usajili wanachama wapya, uhamasishaji ulipaji ada, kuimarisha ushiriki wa wanachama na kusikiliza changamoto za wanachama na wananchi.

Mafunzo hayo yanayotolewa chini ya Idara ya Itikadi, Uenezi na Mfunzo inayoongozwa na Kenan Kihongosi, yanatarajiwa

kuongeza wastani wa wanachama wapya 500 kwa kila wilaya, sawa na wanachama wapya 84,000 katika wilaya zote 168 za Chama.

WASIRA ABAINISHA UMUHIMU WA MAFUNZO

Akifungua mafunzo hayo katika Chuo cha Umoja wa Vijana wa CCM, Ihemi mkoani Iringa, Septemba 15 mwaka huu, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, alisema makada hao wanapaswa kuwa sehemu ya mabadiliko yanayofanywa ndani ya Chama kwa kutumia maarifa wanayoyapata.

“Makada waliopata mafunzo haya wanapaswa kuyatumia kuwafikia wanachama ili kutoa elimu kwa usahihi,” amesema Wasira.

Alieleza kuwa CCM ina historia ndefu na nafasi yake katika siasa za Tanzania ambayo inawataka makada kuelewa kwa kina misingi na itikadi ya Chama kisha kuisimamia katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa mujibu wa Wasira, jukumu la makada hao halipaswi kuishia katika kuongeza idadi ya wanachama pekee, bali linapaswa kuhakikisha wanaojiunga CCM wanaelewa misingi, itikadi na wajibu wao ndani ya Chama.

Amesisitiza kuwa CCM itaendelea kusimamia misingi ya demokrasia nchini kwa kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya kuchagua viongozi anaowataka bila chuki, dhuluma wala vikwazo.

“Katika demokrasia kila mtu anapaswa kuwa na haki, pasipo dhuluma na chuki, na watu wachague watu wanaowataka bila changamoto yoyote,” alisema.

KIHONGOSI AANIKA MCHAKATO MZIMA

Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kihongosi, alisema makada hao hawakuchaguliwa kwa bahati, bali walipitia mchakato wa usajili na usaili uliofanyika katika kanda zote tisa za kichama.

“Kabla ya kuanza mafunzo, kila kanda ilifanya usajili na usaili wa washiriki,” alisema na kuongeza kuwa mpango huo unalenga kujenga wataalamu wa mafunzo katika kila wilaya, watakaokuwa na uwezo wa kufikisha elimu ya Chama hadi katika ngazi za chini.

“Kinachojengwa katika mafunzo haya ni utekelezaji wa mfano wa kitaifa unaolenga kujenga wataalamu wa mafunzo katika kila wilaya,” alibainisha.

Kihongosi alisema miongoni mwa malengo makubwa ya mpango huo ni kuhakikisha kila wilaya inachangia kupata wanachama wapya 500.

“Lengo ni kusajili wanachama wapya 500 kila wilaya nchini. Washiriki wanapaswa kubeba yale watakayofundishwa na kuyafikisha kwa wananchi ili kuhakikisha wanapata elimu wanayoitarajia na kujenga Chama,” alifafanua.

SIASA ZA CCM KIMATAIFA ZIPO IMARA – RABIA

Akitoa mada kuhusu nafasi ya CCM katika siasa za ndani na uhusiano wa kimataifa, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdalla Hamid, alisisitiza kuwa siasa za CCM katika mahusiano kimataifa zinaeleweka vizuri kupitia historia yake ya ukombozi wa Afrika, mahusiano ya vyama vya siasa, mshikamano wa nchi zinazoendelea na nafasi ya Tanzania katika diplomasia ya kimataifa.

Alisema CCM inasisitiza umuhimu wa kujitawala, mazungumzo, diplomasia na misingi ya umoja wa Afrika.

Alibainisha kuwa mahusiano ya kimataifa pia yanaunganishwa na masuala ya maendeleo ya uwekezaji, biashara, teknolojia, elimu, mafunzo na ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

CPA JAMAL: ITIKADI YA CCM IMEAKISI MATAKWA YA WATANZANIA

Akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo hayo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Uchumi na Fedha, CPA Jamal Kassim Ali, alisisitiza kuwa falsafa na itikadi ya CCM imeakisi matakwa ya Watanzania na ndiyo sababu imeendelea kukaa madarakani tofauti na vyama vingine vya ukombozi barani Afrika.

Alisema Watanzania bado wameendelea kuiamini CCM kwa sababu ya usimamizi madhubuti wa ilani yake ya uchaguzi.

“Falsafa na itikadi ya CCM imeakisi matakwa ya wananchi wa Tanzania. Vyama vingine havina sera wala itikadi. Sera za CCM tangu kilipoasisiwa mwaka 1977 bado zimekuwa mwanga wa kufungua maono na sura kwa wananchi. Nendeni mkawafunze juu ya itikadi, misingi ya utu, wajibu na sera yake kuu ya ujamaa na kujitegemea ambayo ndiyo nguzo na dira ya CCM.

Alisisitiza: “Wakoloni hawakuiacha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nchi hii iliundwa na viongozi wenye upeo walioona msingi wa umoja ndiyo silaha ya maendeleo. CCM ni zao la vyama viwili vya ukombozi vilivyojengwa katika misingi ya utu na umoja ambavyo ni TANU na ASP.”

Kwa mujibu wa Jamal, mafunzo hayo ni hatua mpya ya CCM kuzalisha makada watakaokuwa na uelewa kuhusu itikadi ya Chama, misingi ya nidhamu kwa taifa, kujenga mshikamano kwa viongozi wa CCM na Taifa.

“Chama kinaamini kimeendaa wakufunzi mahili kuwafunza wanachama ngazi ya mashina, matawi na kata kuhusu itikadi, imani na falsafa ya CCM. Vyama vyote dunuani vilikuwa vikubwa kwa kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo mafunzo kwa wanachama wake.

“CCM ni miongoni mwa vyama vichache vya ukombozi ambacho kimeendelea kuwa madarakani na kipo madarakani siyo kwa ubabe bali ni kuaminiwa na Watanzania,” alisisitiza.

MAFUNZO KUIMARISHA UHAI WA CCM

Kaimu Katibu Msaidizi Mkuu, Idara ya Uenezi, Itikadi na Mafunzo, Avelin Mushi, alisema idara hiyo inaendelea kusimamia programu hiyo kwa karibu ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa.

“Kuanza kwa mafunzo ya Awamu ya Pili katika Chuo cha Tunguu Zanzibar kwa makada 380 kutoka mikoa 17 na wilaya 76, baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza kule Ihemi, Iringa kwa makada 460 kutoka mikoa 15 na wilaya 92, ni hatua ya utekelezaji wa programu hii.

“Mafunzo haya yana lengo la kuwajengea uwezo makada wa Chama chetu na kuimarisha uhai wa Chama katika ngazi za chini,” alibainisha.

MAKADA 1,522 WALIVYOPITIA MCHUJO

Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na Maandalizi ya Makada, Mwalimu Rajab Yusuf, alisema jumla ya makada 1,522 walifanyiwa usaili na kuchujwa ambapo makada 840 walipatikana, sawa na makada watano kwa kila wilaya.

Alisema usaili ulifanyika kwa kutumia mchakato wa pamoja wa kitaifa ulioratibiwa na Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, ukizingatia uelewa wa historia, muundo, misingi na itikadi ya Chama, uwezo wa kujenga na kuwasilisha hoja, mbinu za ufundishaji, maadili na nidhamu pamoja na uwezo wa kuendeleza elimu ya Chama.

“Mfumo huo uliwezesha kuweka viwango vinavyofanana vya uteuzi kabla ya hatua ya mafunzo. Kwa ujumla, shughuli ya usaili imekamilisha hatua muhimu ya uthibiti wa ubora kwa kuunganisha viwango vya uteuzi katika mikoa 32 na wilaya 168.

“Mwitikio wa makada waliofanyiwa usaili na kuteuliwa, ulikuwa wa kutia moyo kwa sababu walionesha utayari, uvumilivu na hamasa wakati wa walipokuwa wakisubiria kusailiwa na kupata matokeo yao, hadi usiku wa saa sita,” alisisitiza.

Mshiriki wa mafunzo hayo, Noel Chilaga alisema jukumu walilopewa ni kubwa, kwa kuwa linawataka kutokaa na elimu waliyoipata, bali kuifikisha kwa wanachama na wananchi katika maeneo yao.

“Tunatakiwa kuhakikisha elimu hii haibaki kwetu. Tukirejea kwenye maeneo yetu, tunapaswa kuwafikia wanachama na kuwaeleza kwa usahihi yale tuliyojifunza,” alisema Chilaga.

Previous Post

NDEJEMBI AZITAKA TAASISI ZA MUUNGANO KUIMARISHA USHIRIKIANO, HUDUMA KWA WANANCHI

Next Post

MSUKUMA AJITEKA,  ATAKA MILIONI 5 KUTOKA KWA NDUGU

Next Post
MSUKUMA AJITEKA,  ATAKA MILIONI 5 KUTOKA KWA NDUGU

MSUKUMA AJITEKA,  ATAKA MILIONI 5 KUTOKA KWA NDUGU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA, SIMBA KAZI KAZI

4 months ago
MPASUKO SIMBA

MPASUKO SIMBA

2 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?